SEMINA YA VIJANA KANISA LA WAADVENTISTA MBEZI LUIS TAREHE 17/8/2014.
semina ya vijana iliyofanyika kanisani Mbz Luis tar 17 08 2014 saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni.
Wednesday, 20 August 2014
Friday, 15 August 2014
JE, UNAVIFAHAMU VITU ALIVYOVITUMIA NABII MAMA ELLEN G WHITE?
Hivi
ni baadhi ya vifaa alivyotumia mama Ellen G. White, mwanamke
anayeaminiwa na kanisa la waadventista wasabato kama nabii wa
Mungu...vifaa vilivyobaki kama makumbusho katika nyumba aliyopata kuishi
huko nchini Marekani.
Endelea kufuatana nasi ili ujifunze kitu.
Kibao kinachoonesha nyumba aliyoishi Mama Ellen na Mume wake James White mwaka 1856-1863 Nyumba waliyoishi wawili hao
Kitanda alichokuwa analalia Enzi za Uhai wake.
Meza na Kiti alichokuwa akitumia wakati akiandika Njozi mbalimbali alizokuwa akipokea
Kalamu na Taa aliyokuwa akitumia kuandika.
Meza na Taa yake
Saturday, 9 August 2014
MCHUNGAJI DR BLASIUS RUGURI AFIKA MWANZA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI WA JENGO LA KIRUMBA SDA CHURCH.
Dr. Ruguri akihutubia washiriki katika kambi la Kirumba Mwanza mara baada ya kuweka jiwe la msingiKutoka kushoto ni Ndugu Mayani mhazini wa konferensi ya nyanza kusini, Ndugu Gideon Msambwa mkurugenzi wa idara ya mawasiliano union konferensi ya kaskazini wa Tanzania na Ndugu Eliamini Kisimbo mhazini wa Shule ya Sekondari ya Nyanza iliyopo jijijni Mwanza wakiimba wimbo katika ibada ya Kambi la mtaa wa kirumba mara baada ya Dr. Blasious Ruguri kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo jipya la kanisa la Kirumba
Dr. Blasious Ruguri akifungua jiwe la msingi wa jengo la kanisa la kirumba Mwanza
Dr. Ruguri (wapili toka kushoto waliovaa kofia) akionyeshwa ramani ya jengo ya jipya la kanisa la Kirumba
MAKAMBI 2014 - HATIMAYE BWANA KAJITWALIA ROHO ZA WATU KWA NJIA YA UBATIZO HUKO MOROGORO.
Kupitia
mikutano ya makambi inayoendelea sehemu mbalimbali, hatimaye watu wengi
wameendelea kumpokea Yesu kama BWANA na Mwokozi wao kwa njia ya ubatizo
baada ya watu wapatao 32 kubatizwa katika mitaa miwili iliyopo mkoani Morogoro yaani mtaa wa Misufini na Kihonda.
Wakati mtaa wa Misufini chini ya Mch. D. Mmbaga na kwaya ya Ubungo Hill ukibatiza watu wapatao saba (7), mtaa wa Kihonda chini ya Mch. S. Singo na kwaya ya Yombo Dovya ulibatiza watu Ishirini na tano (25).
Makambi yote haya yanategemewa kuhitimishwa Jumamosi ya tarehe 09/08/2014 kwa sherehe kubwa.
Mch. Mndambi akiendelea na huduma ya ubatizo.Mch. Mndambi akiendelea na huduma ya ubatizo
Wanafamilia wakifurahia matendo makuu ya Mungu baada ya mmoja wa familia yao kupokea Yesu kwa njia ya ubatizo
Friday, 8 August 2014
Dr Blasious Ruguri:
Maelfu ya washiriki wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato toka Nyanda za juu kusini mwa Tanzania waliojitokeza kumsikiliza Kiongozi wa Kanisa hilo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Dr Blasious Ruguri hapa ilikuwa ni Iganzo, Mbeya Agosti 3, mwaka huu, Kiongozi huyo jana aliweka jiwe la msingi katika kanisa la Waadventista Wa Sabato Kirumba na kesho anatarajiwa kuwa mkoani Geita kabla ya kuelekea huko Kigoma katika kuisimika Konferensi mpya ya Magharibi mwa Tanzania

Friday, 1 August 2014
Dr. Blasious Ruguri yuko jijini
Mbeya:
Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato,Dr. Blasious Ruguri yuko jijini Mbeya kwa ziara ambapo atashiriki ufunguzi wa Jengo la Makao Makuu ya Konferensi ya Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania iliyoko Iganzo,Shule ya Sekondari ya Mbeya Adventist (MASS) iliyojengwa huko Forest,atatoa Semina kwa Viongozi wa Makanisa ambapo siku ya Sabato ya Agosti 2,mwaka huu washiriki wote wa makanisa ya Waadventista Wa Sabato jijini Mbeya na wajumbe toka makanisa mbalimbali ya Konferensi hii watasali Iganzo ambapo Dr Ruguri atahutubu.

Subscribe to:
Posts (Atom)