Subscribe:

Saturday, 9 August 2014

MAKAMBI 2014 - HATIMAYE BWANA KAJITWALIA ROHO ZA WATU KWA NJIA YA UBATIZO HUKO MOROGORO.

 Kupitia mikutano ya makambi inayoendelea sehemu mbalimbali, hatimaye watu wengi wameendelea kumpokea Yesu kama BWANA na Mwokozi wao kwa njia ya ubatizo baada ya watu wapatao 32 kubatizwa katika mitaa miwili iliyopo mkoani Morogoro yaani mtaa wa Misufini na Kihonda.
Wakati mtaa wa Misufini chini ya Mch. D. Mmbaga na kwaya ya Ubungo Hill ukibatiza watu wapatao saba (7), mtaa wa Kihonda chini ya Mch. S. Singo na kwaya ya Yombo Dovya ulibatiza watu Ishirini na tano (25).
Makambi yote haya yanategemewa kuhitimishwa Jumamosi ya tarehe 09/08/2014 kwa sherehe kubwa.

                                            Mch. Mndambi akiendelea na huduma ya ubatizo.

                                      Mch. Mndambi akiendelea na huduma ya ubatizo
 Mch. Mndambi akiendelea na huduma ya ubatizo na watu wakishuhudia.

 Wanafamilia wakifurahia matendo makuu ya Mungu baada ya mmoja wa familia yao kupokea Yesu kwa njia ya ubatizo

0 comments:

Post a Comment