Subscribe:

Friday, 10 June 2016

KAMBI LA VIJANA MASASI LIKIWA LINAENDELEA KWA KASI:

Mungu wetu ni mwema sana kwa makuu ambayo anazidi kuwatendea vijana hawa wa kanisa la Waadventista Wasabato ambao wameamua kabisa na kudhamiria kuifanya kazi ya Mungu kwa juhudi kubwa sana.
Mafunzo ambayo wanayapata wawapo huko MASASI ni mazuri ambapo wanakuwa wakakamavu na makini pale ambapo wanaifanya kazi ya Mungu kwa sababu kazi ya Mungu haifanywi kwa ulegevu.
Tuzidi kuwakumbuka katika Maombi sana.





WANA MKUTANO WA TAiN-DODOMA WAKIWA KATIKA ZIARA YA BUNGENI:

Wana TAiN Wakiwa Nje ya Ukumbi wa Bunge hii Leo Baada yakusikiliza Mjadala wa Wizara ya Fedha Uliyo kuwa ukiendelea.
Mikutano Ya TAiN iliyo anza tarehe 05/06/2016 inategemea kuisha kesho na hatimaye Jumapili watu watakuwa wakitawanyika kuelekea Pande Nne za Nchi ya Tanzania.
 Endelea kutuombea sana..
 




Thursday, 9 June 2016

MKUTANO WA TAiN-DODOMA WAFANYA JAMBO KUBWA KWA JAMII:
 


Zawadi hii imetolewa na Mchungaji David Makoye(aliye kulia) Katibu mkuu wa Unioni ya kusini mwa Tanzania na Watatu kutoka kulia ni Mchungaji Rabson Nkoko Katibu Mkuu wa Unioni ya kusini mwa Tanzania Mr
Haggai Abuto IT Manager wa Division

Ndugu Paulo ametokea Kanisa la Mugaja Bunda Mkoa wa Mara kama mkuu wa mawasiliano wa kanisa.
 
 
 Zawadi hii imetolewa na Mchungaji David Makoye(aliye kulia) Katibu mkuu wa Unioni ya kusini mwa Tanzania na Watatu kutoka kulia ni Mchungaji Rabson Nkoko Katibu Mkuu wa Unioni ya kusini mwa Tanzania Mr
Haggai Abuto IT Manager wa Division
 
UPELEKAJI WA INJILI WA SIKU ZA MWISHO KWA NJIA YA MABAWA:
MNENAJI: MCH MARK WALWA MALEKANA.


Ameyasema hayo mapema leo katika mkutano wa wanahabari na mawasiliano wa Tain ambapo alianza kwa utangulizi wa kusema nini maana SIKU ZA MWISHO.
Siku za mwisho zinaanza baada ya siku 1260 (538-1798) na akigusia tabia ya siku za mwisho Mchungaji Malekana alifafanua kwa kusoma Daniel 12:4 na siku hizo zinatabia kama;-
1. Watu wataenda mbali huku na huko 
2. Maarifa yataongezeka

 
Historia ya Dunia inaonesha kuwa teknolojia ilibadilika mara baada ya kalne ya 19 na mapinduzi ya viwanda yalibadilika na ilipiga hatua kwa kasi huku ikiongezeka.
Na leo kwa njia ya teknolojia ufahamu wa utaongezeka na hii huonekana wazi katika baadhi ya mafungu ya kitabu cha Daniel ikitaja maneno "Mabawa (uwepesi wa neno kwenda kwa kasi) na Sauti kuu (Injili ihubiriwe kwa nguvu zote)"

 
Mchungaji Malekana kwa kusisitiza somo hili alisema sasa ni wakati wa kurusha ujumbe wa kupaa kama neno mabawa lilivyotumika kwenye kitabu cha Biblia na kumalizia kwa kusema ni vyema washiriki kuvitumia vifaa vya teknolojia visivyoshikika(soft copy) na pia bila kusahau vitabu vinavyoshikika(Hard copy) hasa vitabu vitabu vya Biblia na Roho ya unabii.

Wednesday, 8 June 2016

TAARIFA YA HALI YA HATARI {ZAHAMA}:
MNENAJI: MCH STEVEN BINA.



* Sisi kama wanahabari tunajukumu kubwa katika kuweza kutoa taarifa.

ZAHAMA: Ni hali ambayo inaweza kuhatarisha maisha pamoja na mali za watu.

*Tunapaswa kuchukua hatua za mara kwa mara kuweza kuepuka zahama.
*Kuwa na mwitikio ambao unapaswa kuwa nao pale ambapo unajiandaa kupambana na zahama.
*Zahama inahusika katika uendeshaji wa kanisa.

KABLA YA ZAHAMA:
1. HISI ZAHAMA.
2. BAINI WASEMAJI WAKUU WA ZAHAMA.
3. KUWA NA MAFUNZO YA WANAHABARI NA USOMAJI. 
4. KUWEKA MIFUMO YA KUEPUKA ZAHAMA.
5. TASMINI HALI YA ZAHAMA.

KANISA KUJITOSHELEZA KUWA NA WATAALAMU WA NYANJA MBALIMBALI:
MNENAJI: MCH MARK WALWA MALEKANA.


Askofu Mkuu wa kanisa la Waadventista Wa Sabato Jimbo kuu la Kusini mwa Tanzani Mchunga Mark Warwa Malekana ametoa rai Kwa waumini wote Tanzania Kufanya kazi Siku sita na siku ya saba Yaje kanisani kwa Ibada na Mapumziko tena bila kusahau Zaka na Sadaka kama shukrani kwa Mungu mpaji.

Mchungaji Marekana Amesema Sasa kanisa Tanzania na Afrika limejitoshereza kwa kila Taaluma Kama wanahabari walio bobea tunao, Wahasibu wenye CPA tunao, Wahandisi Tunao, Wanatheolojia Tunao Shida ni Waamini wengi Ni udumavu wa Kiroho.

Mchungaji Marekana Amesema hayo hii leo wakati akiusalimu Mkutano wa TAiN Unao endelea Mjini Dodoma.
AINA ZA MAWASILIANO:
MNENAJI: MCH RICHARD KANIKI

 Mkutano unaoendelea katika kanisa la Dodoma Sda na ikiwa ni siku ya tatu tangu kuanza rasmi kwa mkutano huu wa mawasiliano na habari. Leo ibada ya ufunguzi imeletwa na Mchungaji Kaniki ambaye alifafanua aina za mawasiliano ambazo.


NJIA ZA MAWASILIANO NI:

 1. Maandishi

Hapa ni machapisho mbalimbali ambapo alisisitiza kuwa njia ya maandishi ndio ilisaidia kuipeleka injili mbele kwenye kipindi kama cha nabii Mama White watu walitoa machapisho yake mbalimbaliambayo pia yalisaidia injili kwenda mbele.
2. Mawasiliano kwa njia ya mdomo
mwanzo 1:28-20
- Mawasiliano haya yanamuhm sana kwa wanandoa na kwa nyanja nyingine ya watumiaji wa mawasiliano.
1Petro3:7
3.Mawasiliano ya kimya
 - Muonekano wa sura yake na vitendo vyake zinaashiria ujumbe au taarifa fulani juu jambo fulani.

Mwanzo 4:5-6
Dalili za mawasiliano ya mdomo
1. Usikilizaji
2 Mzungumzaji
3.Utawala wa mazungumzo.