UPELEKAJI WA INJILI WA SIKU ZA MWISHO KWA NJIA YA MABAWA:
MNENAJI: MCH MARK WALWA MALEKANA.
Ameyasema
hayo mapema leo katika mkutano wa wanahabari na mawasiliano wa Tain
ambapo alianza kwa utangulizi wa kusema nini maana SIKU ZA MWISHO.
Siku
za mwisho zinaanza baada ya siku 1260 (538-1798) na akigusia tabia ya
siku za mwisho Mchungaji Malekana alifafanua kwa kusoma Daniel 12:4 na
siku hizo zinatabia kama;-
1. Watu wataenda mbali huku na huko
2. Maarifa yataongezeka
Historia
ya Dunia inaonesha kuwa teknolojia ilibadilika mara baada ya kalne ya
19 na mapinduzi ya viwanda yalibadilika na ilipiga hatua kwa kasi huku
ikiongezeka.
Na
leo kwa njia ya teknolojia ufahamu wa utaongezeka na hii huonekana wazi
katika baadhi ya mafungu ya kitabu cha Daniel ikitaja maneno "Mabawa
(uwepesi wa neno kwenda kwa kasi) na Sauti kuu (Injili ihubiriwe kwa
nguvu zote)"
Mchungaji
Malekana kwa kusisitiza somo hili alisema sasa ni wakati wa kurusha
ujumbe wa kupaa kama neno mabawa lilivyotumika kwenye kitabu cha Biblia
na kumalizia kwa kusema ni vyema washiriki kuvitumia vifaa vya
teknolojia visivyoshikika(soft copy) na pia bila kusahau vitabu
vinavyoshikika(Hard copy) hasa vitabu vitabu vya Biblia na Roho ya
unabii.
0 comments:
Post a Comment