Dr Blasious Ruguri:
Maelfu
ya washiriki wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato toka Nyanda za juu
kusini mwa Tanzania waliojitokeza kumsikiliza Kiongozi wa Kanisa hilo
katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Dr Blasious Ruguri hapa
ilikuwa ni Iganzo, Mbeya Agosti 3, mwaka huu, Kiongozi huyo jana aliweka
jiwe la msingi katika kanisa la Waadventista Wa Sabato Kirumba na kesho
anatarajiwa kuwa mkoani Geita kabla ya kuelekea huko Kigoma katika
kuisimika Konferensi mpya ya Magharibi mwa Tanzania
Friday, 8 August 2014
Friday, 1 August 2014
Dr. Blasious Ruguri yuko jijini
Mbeya:
Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato,Dr. Blasious Ruguri yuko jijini Mbeya kwa ziara ambapo atashiriki ufunguzi wa Jengo la Makao Makuu ya Konferensi ya Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania iliyoko Iganzo,Shule ya Sekondari ya Mbeya Adventist (MASS) iliyojengwa huko Forest,atatoa Semina kwa Viongozi wa Makanisa ambapo siku ya Sabato ya Agosti 2,mwaka huu washiriki wote wa makanisa ya Waadventista Wa Sabato jijini Mbeya na wajumbe toka makanisa mbalimbali ya Konferensi hii watasali Iganzo ambapo Dr Ruguri atahutubu.

Tuesday, 22 July 2014
Monday, 7 July 2014
Ilivyokuwa Tarehe 6/7/2014 katika kanisa la MSINGWA tulipokusanyika Mtaa wa MBEZI LUIS kufanya changizo kwa ajili ya kujenga Nyumba ya Mchungaji wa Mtaa.
Washiriki wakiwa katika utulivu kanisani
Kwaya ya Uinjilisti Mbezi Luis wakimtukuza Mungu katika Ibada kuu.
Washiriki wakiwa katika usikivu wa pekee katika Ibada
Kwa usikivu wa hali ya juu katika Ibada.
Kwaya ya MSINGWA ikimtukuza Mungu kwa njia ya Nyimbo katika darasa la Watoto.

Sunday, 15 June 2014
MATUKIO YA WABATIZWA KWENYE MKUTANO WA INJILI MBEZI LUIS 13/6/2014 AMBAPO TULIBATIZA WATU 35.
Umakini kusikiliza maelekezo kwa Mchungaji.
Uhakiki wa majina ukifanyika kwa wabatizwa kabla ya kula kiapo.
Wabatizwa wakisikiliza kwa umakini maelekezo kutoka kwa Mzee wa kanisa.
Wabatizwa wakila kiapo katika Mkutano wa Neno la Mungu
Wakiwa ndani ya Gari tayari kwa kwenda kubatizwa.
Mchungaji Tirumanywa akitoa maelekezo kwa wabatizwa kabla ya kuanza kuwabatiza.
Wakiwa wamepanga foleni tayari kwa kuingia kwenye maji na kubatizwa.
Mchungaji Tirumanywa akifanya huduma ya Ubatizo Msasani katika bahari ya Hindi.
Mbatizwa akitoka ndani ya maji.

Wednesday, 4 June 2014
BRAZIL:KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO NCHINI BRAZIL KUTOA HUDUMA ZA KIROHO NA KIJAMII WAKATI WA KOMBE LA DUNIA.
Makanisa mahalia ya Waadventista Wa Sabato nchini Brazil yatashiriki kutoa huduma za kiroho na kijamii kwa maelfu ya mashabiki wa mchezo wa soka wakati wa mashindano ya kombe la dunia yanayotarajiwa kuanza nchini humo juni 12,mwaka huu.
Shirika la Habari la Kanisa la
Waadventista Wa Sabato Duniani (ANN) limeeleza kuwa ,Kanisa la Waadventista Wa
Sabato nchini Brazil limepanga kuwatumia vijana na watu wazima wa kanisa hilo
katika majiji 12 inakofanyika michuano hiyo kwa kutoa huduma ya maji,matamasha
ya uimbaji,maonesho ya masuala ya afya na kujitolea damu.
Mpango huo unaoitwa Tumaini kwa Brazil
unalengo la kuwafikia watu toka nchi mbalimbali duniani watakaokuwa Brazil kushuhudia mashindano hayo pia utahusisha usambazaji wa vipeperushi na
uuzaji wa beji nchini humo ambako shule zitakuwa zimefungwa kwa muda wa siku 32
za michuano hiyo.
Hata hivyo kutakuwa na ugawaji wa
vitabu milioni moja vya
Tumaini Pekee kilichoandikwa na mwinjilisti wa Alejandro Bullón,magazeti yanayozungumzia
matatizo ya biashara ya ngono.
Areli Barbosa, ambaye ni Mkurugenzi wa
Vijana wa Divisheni ya Amerika ya Kusini katika kanisa la Waadventista Wa
Sabato amesema mpango huo si kwa ajili ya kuunga mkono michuano ya soka ya
Kombe la Dunia bali ni kutoa huduma kwa jamii.
Subscribe to:
Posts (Atom)