BRAZIL:KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO NCHINI BRAZIL KUTOA HUDUMA ZA KIROHO NA KIJAMII WAKATI WA KOMBE LA DUNIA.
Makanisa mahalia ya Waadventista Wa Sabato nchini Brazil yatashiriki kutoa huduma za kiroho na kijamii kwa maelfu ya mashabiki wa mchezo wa soka wakati wa mashindano ya kombe la dunia yanayotarajiwa kuanza nchini humo juni 12,mwaka huu.
Shirika la Habari la Kanisa la
Waadventista Wa Sabato Duniani (ANN) limeeleza kuwa ,Kanisa la Waadventista Wa
Sabato nchini Brazil limepanga kuwatumia vijana na watu wazima wa kanisa hilo
katika majiji 12 inakofanyika michuano hiyo kwa kutoa huduma ya maji,matamasha
ya uimbaji,maonesho ya masuala ya afya na kujitolea damu.
Mpango huo unaoitwa Tumaini kwa Brazil
unalengo la kuwafikia watu toka nchi mbalimbali duniani watakaokuwa Brazil kushuhudia mashindano hayo pia utahusisha usambazaji wa vipeperushi na
uuzaji wa beji nchini humo ambako shule zitakuwa zimefungwa kwa muda wa siku 32
za michuano hiyo.
Hata hivyo kutakuwa na ugawaji wa
vitabu milioni moja vya
Tumaini Pekee kilichoandikwa na mwinjilisti wa Alejandro Bullón,magazeti yanayozungumzia
matatizo ya biashara ya ngono.
Areli Barbosa, ambaye ni Mkurugenzi wa
Vijana wa Divisheni ya Amerika ya Kusini katika kanisa la Waadventista Wa
Sabato amesema mpango huo si kwa ajili ya kuunga mkono michuano ya soka ya
Kombe la Dunia bali ni kutoa huduma kwa jamii.
0 comments:
Post a Comment