Subscribe:

Tuesday, 18 August 2015

MAKAMBI MTAA WA MBEZI LUIS MWAKA 2015: 
MOTTO: AMKA PIGA HATUA KUELEKEA JUU
NENO KUU: Akaenda pamoja na Mungu, Naye akatoweka maana Mungu alimtwaa  "MWAMZO 5:24."
WIMBO MKUU: 73

Mungu anazidi kuwa mwema tena katika makambi haya tunazidi kubarikiwa na watumishi wa Mungu...

  Mchungaji ASTON MMAMBA akizungumza na watu wa Mungu.

  Kwaya ya UVUVIO wakifanya huduma ya Uiimbaji katika makambi

  Watoto nao wamo wakiweka usikivu wa hali ya juu wakijifunza ukuu wa Mungu.
 
 Kwaya ya KWEMBE  wakifanya huduma ya Uiimbaji katika makambi


  Mch Abrahamu Youze akizungumza machache na watu wa Mungu.

 Kwaya ya Uinjilisti Mbezi Luis  wakifanya huduma ya Uiimbaji katika makambi

 Kwaya ya Malamba mawili wakifanya hududma ya Uiimbaji katika makambi

  Washiriki wakiweka usikivu wakati wa Ibada kuu.

Sunday, 16 August 2015

MAKAMBI MTAA WA MBEZI LUIS MWAKA 2015: 
MOTTO: AMKA PIGA HATUA KUELEKEA JUU
NENO KUU: Akaenda pamoja na Mungu, Naye akatoweka maana Mungu alimtwaa  "MWAMZO 5:24."
WIMBO MKUU: 73

Ni Ufunguzi wa Makambi na huu utakuwa ni mwendelezo wa takribani wiki nzima yaani siku 7.
njoo uweze kubarikiwa na watumishi wa Mungu waliojiandaa kuzungumza nasi.
Mnenaji mkuu Mch Aston Mmamba aliweza kuzungumza na watu wa Mungu katika siku ya leo ya tarehe 16/8/2015 na akagusia juu ya LUKA 15:1-20 .




    Mch Aston Mmamba akinena na watu wa Mungu katika Makambi .


      "Kwaya ya Waadventista wasabato MBEZI LUIS UINJILISTI wakimsifu Mungu kwa njia ya Uimbaji"
 
      
      "Kwaya ya Waadventista wasabato TEMBONI wakimsifu Mungu kwa njia ya Uimbaji"

  
"Kwaya ya Waadventista wasabato MALAMBA MAWILI  wakimsifu Mungu kwa njia ya Uimbaji"


      "Kwaya ya Waadventista wasabato MSINGWA wakimsifu Mungu kwa njia ya Uimbaji"




      "Kikundi cha Friends Of Jesus wakimsifu Mungu kwa njia ya Uimbaji"

 
      "Kwaya ya Waadventista wasabato UVUVIO wakimsifu Mungu kwa njia ya Uimbaji"

Sunday, 9 August 2015

MKUTANO WA MAKAMBI MTAA WA MBEZI LUIS 2015:


Panga kubarikiwa sana unapojielekeza kuwepo katika huu Mkutano wa neno la Mungu kwa takribani siku 7 kuanzia Tarehe 16 -22 August 2015.
Waweza kufuatilia hapa yale yatakayokuwa yanajiri kupitia....http://mbeziluischurch.blogspot.com/
Asante sana.

Monday, 20 July 2015

Yanayojiri katika kanisa la waadventista wasabato Mbezi luis jijini Dar es salaam ni Ujenzi wa choo cha kisasa.Washiriki wakiwa wamejitolea kusaidiana na mafundi kuweza kujenga choo hicho cha kisasa.Mungu aendelee kuwa nasi tunapoendelea kujitoa kufanya kazi yake.












Thursday, 9 July 2015

  SAN ANTONIO 2015: HAWA NDIO VIONGOZI WENYEVITI WA DIVISHENI ZOTE 13 ZA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO.6 WAKIWA NI WAPYA KABISA NA WAZAMANI MMOJA WAPO NI MCHUNGAJI DR BLASIOUS RUGURI



BLASIOUS Ruguri, East-Central Africa Division, incumbent
Michael Kaminski, Euro-Asia Division
Mario Brito, Inter-European Division
Israel Leito, Inter-American Divison, incumbent
Daniel Jackson
, North American Division, incumbent
Jairyong Lee
, Northern Asia-Pacific Division, incumbent
Erton Carlos Kohler
, South American Division, incumbent
Paul Ratsara, Southern Africa-Indian Ocean Division, incumbent
Glenn Townend
, South Pacific Division
Leonardo Asoy
, Southern Asia-Pacific Division
Raafat Kamal
, Trans-European Division, incumbent
Elie Weick-Dido
, West-Central Africa Division
Ezras Lakra, Southern Asia Division

Saturday, 4 July 2015

KWAYA DAY ndivyo unavyoweza kuiita hivyo.Ambayo imefanyika Tarehe 4/7/2015.Ni katika Ibada ambayo imefanyika katika kanisa la waadventista wasabato KWEMBE jijini Dar es salaam.Ambapo tukio hili lilisindikizwa na kwaya mbalimbali za waadventista wasabato.Lengo lilikuwa ni kuweza kupata Milion 100 kuweza kununua vyombo vya kwaya hiyo.Mwinjilisti BENSON IZOKA alikuwa Mnenaji mkuuu na aliweza kutuweka karibu na miguu ya Yesu katika somo lililokuwa linasema "NITAMBULISHE YESU"

                                     Mwinjilisti BENSON IZOKA akuhubiri

Kwaya ya Uinjilisti MBEZI LUIS

Kwaya ya TABATA KINYEREZI wakiimba wakati wa Ibada kuu


 Mzee wa kanisa Ndugu Togolani Mnkeni akiongoza zoezi la uchangiaji katika siku hiyo.

 Mkurugenzi wa Elimu & Mawasiliano katika Konferensi ya SEC Ndugu Abraham Youze na familia yake wakisikiliza neno la Mungu.


                                        Kwaya ya KWEMBE wakiimba na kumsifu Mungu
SAN ANTONIO -2015 PATA KUFAHAMU HISTORIA YA MCH TED.C.WILSON


Kikao cha 60 cha Konfrensi kuu ya kanisa la Waadventista Wasabato Ulimwenguni kimepitisha jina la Mchungaji Ted N C Wilson kuliongoza kanisa la Waadventista Wasabato kama kiongozi wa juu kabisa ngazi ya dunia kwa mara ya pili mfululizo, ambapo atamaliza uongozi wake mwaka 2020.

Kwa mara ya kwanza kuchaguliwa katika nafasi hiyo ilikuwa mwaka 2010 huko Atlanta, Georgia na kuwa kiongozi wa 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo 1863.
Alizaliwa mwezi Mei 10, 1950 huko Takoma Park, Maryland Marekani, na baba yake ambaye ni Rais mstaafu wa kanisa hilo Mch. Neal C Wilson pamoja na mkewe Mama Elinor E Wilson.

Mchungaji Ted, ameishi kipindi chake cha utoto nchi Misri na alianza shughuli za kanisa kama mchungaji mwaka 1974 katika Konferensi ya Greater New York.

Mwaka 1976-1981, Alihudumu kama Mkurugenzi msaidizi na baadae kama Mkurugenzi mkuu wa huduma za Kimetropolitian huko New York.

Mwaka 1990 alienda katika divisheni ya Africa-bahari ya hindi Abidjan na Coted'Ivoire kama mkurugenzi wa idara na baadaye kama Katibu (executive secretary).
Kufuatia nafasi yake hiyo katika Magharibi mwa Afrika, Alihudumu kwa miaka miwili (2) katika makao makuu ya Kanisa huko Silver Spring Maryland Marekani kama Katibu (Associate Secretary).

Mwaka 1992 hadi 1996 alikubali nafasi ya Rais wa divishen ya Ulaya Asia huko Moscow, Urusi na kabla  na uteuzi wa kuwa rais wa Kanisa hili duniani mwaka 2010 alihudumu ka Makamu Mwenyekiti.

Mch. ted na mkewe mama Nancy, wana mabinti Watatu (3) na wajukuu nane (8).
Ni Daktari wa Philosophia katika Elimu ya Dini ya Chuo Kikuu cha New York (Doctor of Philosophy degree in Religious Education), Master of divinity ya chuo kikuu cha Andrews na Master of Science in Public Healthy ya Chuo kikuu cha Tiba cha Loma Linda.
Ukiachilia mabali lugha ya Kingereza pia anazungumza Kifaransa na Kirusi.