Subscribe:

Saturday, 4 July 2015

SAN ANTONIO -2015 PATA KUFAHAMU HISTORIA YA MCH TED.C.WILSON


Kikao cha 60 cha Konfrensi kuu ya kanisa la Waadventista Wasabato Ulimwenguni kimepitisha jina la Mchungaji Ted N C Wilson kuliongoza kanisa la Waadventista Wasabato kama kiongozi wa juu kabisa ngazi ya dunia kwa mara ya pili mfululizo, ambapo atamaliza uongozi wake mwaka 2020.

Kwa mara ya kwanza kuchaguliwa katika nafasi hiyo ilikuwa mwaka 2010 huko Atlanta, Georgia na kuwa kiongozi wa 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo 1863.
Alizaliwa mwezi Mei 10, 1950 huko Takoma Park, Maryland Marekani, na baba yake ambaye ni Rais mstaafu wa kanisa hilo Mch. Neal C Wilson pamoja na mkewe Mama Elinor E Wilson.

Mchungaji Ted, ameishi kipindi chake cha utoto nchi Misri na alianza shughuli za kanisa kama mchungaji mwaka 1974 katika Konferensi ya Greater New York.

Mwaka 1976-1981, Alihudumu kama Mkurugenzi msaidizi na baadae kama Mkurugenzi mkuu wa huduma za Kimetropolitian huko New York.

Mwaka 1990 alienda katika divisheni ya Africa-bahari ya hindi Abidjan na Coted'Ivoire kama mkurugenzi wa idara na baadaye kama Katibu (executive secretary).
Kufuatia nafasi yake hiyo katika Magharibi mwa Afrika, Alihudumu kwa miaka miwili (2) katika makao makuu ya Kanisa huko Silver Spring Maryland Marekani kama Katibu (Associate Secretary).

Mwaka 1992 hadi 1996 alikubali nafasi ya Rais wa divishen ya Ulaya Asia huko Moscow, Urusi na kabla  na uteuzi wa kuwa rais wa Kanisa hili duniani mwaka 2010 alihudumu ka Makamu Mwenyekiti.

Mch. ted na mkewe mama Nancy, wana mabinti Watatu (3) na wajukuu nane (8).
Ni Daktari wa Philosophia katika Elimu ya Dini ya Chuo Kikuu cha New York (Doctor of Philosophy degree in Religious Education), Master of divinity ya chuo kikuu cha Andrews na Master of Science in Public Healthy ya Chuo kikuu cha Tiba cha Loma Linda.
Ukiachilia mabali lugha ya Kingereza pia anazungumza Kifaransa na Kirusi.

0 comments:

Post a Comment