HISTORIA YA MAREHEMU JOSHUA KAJULA:
                           MAREHEMU MCH JOSHUA KAJULA
KUZALIWA KWAKE
Mchungaji Joshua Kamenya Kajula alizaliwa tarehe 28 Disemba
1939; huko Maeneo ya Majengo wilaya ya Mbeya Mjini katika Mkoa wa Mbeya. Yeye
ni mtoto wa Pili kuzaliwa kati ya watano kwa mama yake. Baba yake alikuwa na
wake wawili.Kwa  upande  wa 
mama  yake  ambaye 
ndiye  alikuwa  mke  wa
ndoa kwa baba walizaliwa wanaume watano. Alikuwa na ndugu  wengine wawili waliozaliwa na baba yake kwa
mke mwingine  ambaye  alirithiwa 
na  baba  yake 
baada  ya  kufiwa na 
kaka  yake.  Hivyo, 
kwa  ujumla  anatoka 
katika  familia  ya  watoto saba kwa baba na kwa mama watano.
ELIMU YAKE
Marehemu mchungaji Kajula alipata elimu yake ya awali katika
Shule ya kati (Middle School) huko Iganzo. Alisoma hapo mpaka darasa la sita
mwaka 1955.Hatimaye alipelekwa Suji Upper Primary darasa la Saba na la Nane.Aliendelea
na masomo yake 
katika kiwango cha darasa la tisa na
la kumi (Standard  9  and 
10).    
Ni 
sawa  na  kusema 
form  two  kwa 
lugha  ya  leo. 
Hatimaye  
alijiunga  na 
chuo  cha  Ualimu 
huko  Ikizu,  mkoani Mara.Alisoma 
Diploma ya ualimu kwa miaka miwili
hatimaye kwenda kuajiriwa mwaka 1962. Wakati huo aliamua kujiendeleza  na 
elimu  ya  kidato 
cha  nne  bado 
akiwa  kazini  kwa kusoma kwa njia ya binafsi (private).Alifanya
kazi kuanzia mwaka 1962 kwa miaka miwili hatimaye akaenda  kuchukua 
kozi  ya  miaka 
miwili  ya  Elimu 
ya  Afya  (Health Education) huko Hospitali ya Heri,
mkoani Kigoma.Huo ulikuwa ni mwaka 1964 hadi 1966.Hatimaye  ndipo 
alipoenda  kuchukua  mafunzo 
ya  kichungaji  mwaka 1967 hadi 1968 huko Bugema, Uganda.
Alipata diploma ya uchungaji.Safari yake ya elimu iliendelea mwaka 1985 hadi
1988 alipenda  India  katika 
chuo  cha  Poona 
Spicer  Memorial  College 
kwa  masomo  ya 
digrii  yake  ya 
kwanza.  Na  akahamia 
huko  Ufilipino kwa masomo yake ya
digrii ya pili. Alianza mwaka 1989 hadi 1991. Na kurejea Nyumbani.
KUAMINI KWAKE
 Marehemu mchungaji alipata imani kupitia kwa
mzungu mmoja aliyekuja 
kufanya kazi huko Misheni ya Iganzo.
Mchungaji Kajula alikuwa akifanya 
kazi kwake ya house boy. Ndipo  akawa 
mtu  wa  kwanza 
kupata  imani 
 katika 
familia  yao.Tunaweza  kusema 
kuamini  kwake  ndio 
chanzo  na  mlango 
wa  kuwafanya  ndugu 
zake  wote  watano 
kujiunga  na  kanisa 
hili la Waadventista WaSabato. Hatimaye mama yake alikuja kuamini
baadaye kabisa. Mchungaji Joshua Kajula alibatizwa mwaka  1952. 
Mchungaji  aliyembatiza  ni 
Mchungaji  Jacques aliyekuwa
mmishonari huko Mbeya.MAISHA YA NDOA Marehemu mchungaji Joshua Kajula alifunga
pingu za maisha tarehe 12 Septemba 1964 na Merry Justine Kimera (ni mtoto wa
mchungaji Justine Salimu Kimera). Ndoa hii ilifungwa na Mchungaji Rufoko
aliyekuwa ni mwenyeji wa Rwanda huko Heri Hospital ambako mchungaji Kajula
alikwenda kuchukua masomo ya elimu ya afya. Mungu  ameibariki 
familia  hii  kuwa 
na  watoto  watatu. 
Wa  kwanza Gloria, wa pili ni
Enidi, na watatu ni Suzzana.   Na kuwa na
wajukuu watano.KAZI YA UTUMISHI NDANI YA KANISA Marehemu  mchungaji 
Kajula  alianza  rasmi 
kazi  ya  utumishi 
ndani  ya  kanisa 
kama  mwalimu  huko 
Masoko,  Rungwe  Historia Ya Maisha Ya Marehemu mkoani Mbeya.
Alianza kufundisha shule hiyo ya kanisa mwaka 1962. Hatimaye alihamishiwa
katika Shule ya msingi Iganzo mwaka huo mwishoni. Alifanya kwa awamu mbili ya
mwaka 1962 hadi 1964. Akaenda Heri Hospital na aliporudi mwaka 1966 alirudi
tena Iganzo kama mwalimu.Wito  wa  kichungaji: 
Marehemu  mchungaji  Kajula 
alikuwa  na wito huo kwa muda
mrefu ndipo alipopelekwa kusomea uchungaji katika chuo cha Bugema. Aliporudi alipangwa
kuwa mchungaji wa Morogoro kuanzia 1969 hadi 1971. Lindi mwaka 1972 – 1973. 
Songea mwaka 1973 kwa miezi sita tu.
Hatimaye alirudi Lindi tena mwaka 
1973 mwishoni mpaka 1975.
KUWEKEWA MIKONO: 
Marehemu mchungaji Kajula aliwekewa mikono ya kichungaji
Novemba 1974. Hii ni ngazi ya mwisho ya kichungaji kama uthibitisho wa kudumu
wa kutumika katika utumishi huo.Aliitwa kuwa mchungaji wa Zanzibar mwaka 1975
kwa wiki moja.  Alienda  kuripoti 
tu  hatimaye  akaambiwa 
abaki  Dar-es-Salaam kuwa
mchungaji wa Magomeni mwaka 1975 hadi 1977.Mwaka  1978 
hadi  1985  aliitwa 
kuwa  Mkurugenzi  wa 
Lay  Activities (Idara ya Huduma
za Washiriki) wakati huo  ikiwa pamoja na
vijana, Dorkas, AMO na nyinginezo.Hatimaye ndipo alipokwenda masomoni huko
India na Ufilipino Mwaka 1991 Disemba alirudi masomoni. Na Januari 1992
alipangwa kuwa mwalimu wa chuo cha TASC (Tanzania Adventist Seminary College)
kwa miezi sita tu. Mwaka huo huo alipelekwa kuwa Mwenyekiti wa Mara Conference
kuanzia 1992 hadi 1996. Hatimaye aliitwa huko Tanzania Union Mission, Arusha
makao  makuu  mwaka 
1996  kama  mkurugenzi 
wa  idara  ya 
Uchapaji na maeneo mapya ambapo alifanya kazi hiyo mpaka Januari mwaka
2000. Alipelekwa katika Field ya South West Tanzania kuwa mwenyekiti wake
kuanzia 2000 mpaka 2005. Mwaka 2005 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Union hiyo
ya  zamani  (Tanzania 
Union  Mission)  mwaka 
2005  mpaka  2010. 
Ndipo alipostaafu kazi ya utumishi ndani ya kanisa Novemba 2010.
JAMBO ATAKALOKUMBUKWA KATIKA UTUMISHI Marehemu mchungaji
Joshua Kajula atakumbukwa kwa mambo 
mengi  ambayo  ameyafanya 
wakati  alipokuwa  akitumika 
ndani  ya  kanisa   
kwa  moyo  wake 
wote.  Aliishi  maisha 
ya  kawaida na kiwango cha chini
kwa ajili ya kuwafikia waumini wote. Hakuwa na ubaguzi wa  kikabila wa kitabaka. Aliheshimika na watu
wote. Ndio maana hata alipokuwa anakaribia kustaafu rasmi 2006; bado kanisa likaona
ni vyema aendelee kulitumikia kwa muda wa ziada ya miaka mingine mitano ambayo
ilikuwa tayari ni nje ya miaka ya kustaafu. Kanisa litamkumbuka sana kwa
unyenyekevu wake na upole
 wake na pia swala la kuzielewa taratibu za
kanisa na kuzisimamia vyema.
 Jambo la pekee sana ni pale alipokuwa anapenda
kusali kwenye makanisa 
madogo madogo na makundi ya kanisa.
Ni jambo ambalo ni nadra sana kwa viongozi wa ngazi kama  yake 
kutenda  hivyo  kwa 
sababu  ya  majukumu 
mazito waliyonayo.
 Ndugu 
na  jamaa  nao 
wanamkumbuka  kama  kaka 
yao  ambaye  alikuwa 
na 
upendo  wa  dhati 
kwa  ndugu  wote. 
Mtiifu  kwa wazazi. Mlezi 
mwema kwa wazazi wake. Mdogo wake Steven  Kajula 
anasema Kaka  alifanya  mambo 
ambayo  kwa tamaduni na desturi za
wanaume wa Kinyakyusa hawafanyi.Alikuwa mfano wa kuigwa kama Mkristo kwa
familia yake na kwa  jamii  alimoishi. 
Alikuwa  mcheshi  anayechangamana  na watu. 
Anakumbukwa  pia  kama 
mtu  aliyekuwa  na 
hobby  ya kuendesha gari. Pamoja
na umri mkubwa alikuwa na uwezo wa kuendesha gari kutoka Dar-es-Salaam hadi
Mbeya bila kuchoka katika uzee wake huu. Pia alikuwa mtu anayejali sheria za  barabarani 
kwani  mpaka  anafariki 
hajawahi  kupata  ajali kwa 
maisha  yake  yote. 
Alikuwa  makini  sana 
barabarani.  Ni jambo la kujifunza
kwetu sote.MAJUKUMU MENGINE BAADA YA KUSTAAFU KWAKE Marehemu mchungaji Kajula
alijishughulisha na shughuli zake ndogo ndogo kwani hakupenda kukaa tu nyumbani
bila kazi.Alifanya shughuli ndogo ndogo kama mtu ambaye amezoea kufanya  kazi 
muda  wote.  Lakini 
bado  kanisa  lake 
alilokuwa 
 anasali, alianza kusali bado likiwa kundi tu
hatimaye likapangwa kuwa 
kanisa. Alifanya ushirika na kanisa
la Kunduchi tarehe  6  Mei 
2012.  
Na 
kuanzia  mwaka  2013 
mpaka  mauti  inapomkuta alikuwa na majukumu 
ya uzee wa kanisa, kiongozi wa uhuru
wa Dini, na pia kwa hekima yake alichaguliwa awe mshauri  wa 
wazee  wa  kanisa 
akishirikiana  na  mchungaji 
wa  mtaa. Alifanya kazi hiyo huku
akionyesha utii wa kuhudhuria semina 
mbalimbali  zilizoitwa  na 
viongozi  wa  juu 
bila  kujali  
aliwahi  kuwa 
kiongozi  mkubwa  wa 
kanisa  katika  ngazi ya Union
Na huku akiunga mipango mikutano yote iliyopangwa na ngazi
za juu kwa kusimamia vyema katika utekelezaji.
MATATIZO YA KIAFYA NA KIFO CHAKE
Marehemu mchungaji Joshua Kajula alianza kuugua
mwishoni  mwa  utumishiwake 
ugonjwa  wa  kisukari. 
Lakini  aliweza  kupata tiba miaka michache akapona kwani
sukari yake ilirudi katika hali ya kawaida kutokana na matibabu aliyoyapata
kutoka       sehemu mbalimbali.Mnamo  mwaka 
jana  alianza  kupata 
tatizo  la  joto 
la  mwili  kupanda juu sana bila kushuka. Ndipo
alipolazwa katika hospital ya 
Rabinisinia iliyoko maeneo ya Tegeta
mwezi wa Disemba tarehe 24 hadi 25.
 Baadaye iligundulika kuwa ilikuwa ni malaria
iliyosababisha joto kupanda sana.
Alitibiwa malaria na Alitoka akawa na udhaifu wa miguu ikawa
imepoteza nguvu ya kutembea. Hatimaye alianza kupata nafuu ya miguu. Lakini
ghaflatena mwezi machi mwanzoni joto la mwili likapanda tena.  Alipelekwa 
Rabinisia  ambako  alipimwa. 
Alilazwa  kwa  siku 
moja,aliporuhusiwa  alirudi  nyumbani. 
Usiku  huo  huo 
hali  yake  ilibadilika 
na  ndipo  alipopelekwa 
Muhimbili  kwa  matibabu 
zaidi.  Siku  ya 
jumatatu  alipelekwa  Muhimbili 
akapokelewa kama mgonjwa wa dharura (emergency patient) na kupelekwa
wodini siku ya jumanne mpaka alhamisi. Na hali yake ikazidi kuwa mbaya ndipo
alipoingizwa Chumba maalumu (ICU) siku ya
 Alhamisi jioni ambako alikaa mpaka Jumamosi
Jioni alipofariki hakutoka 
tena hapo.Hivyo marehemu mchungaji
Joshua Kamenya Kajula alifariki tarehe 19 MACHI 2016 SAA MOJA USIKU Hapo ndipo
ulipokuwa mwisho wa maisha ya Mtumishi wa Mungu Mchungaji Joshua Kamenya Kajula
KUZALIWA KWAKE
Mchungaji Joshua Kamenya Kajula alizaliwa tarehe 28 Disemba 1939; huko 
Maeneo ya Majengo wilaya ya Mbeya Mjini katika Mkoa wa Mbeya. Yeye ni 
mtoto wa Pili kuzaliwa kati ya watano kwa mama yake. Baba yake alikuwa 
na wake wawili.
Kwa upande wa mama yake ambaye ndiye alikuwa mke wa ndoa kwa baba 
walizaliwa wanaume watano. Alikuwa na ndugu wengine wawili waliozaliwa 
na baba yake kwa mke mwingine ambaye alirithiwa na baba yake baada ya 
kufiwa
na kaka yake. Hivyo, kwa ujumla anatoka katika familia ya watoto saba 
kwa baba na kwa mama watano. 
ELIMU YAKE
Marehemu mchungaji Kajula alipata elimu yake ya awali katika Shule ya 
kati (Middle School) huko Iganzo. Alisoma hapo mpaka darasa la sita 
mwaka 1955. 
 Hatimaye alipelekwa Suji Upper Primary darasa la Saba na la Nane. 
Aliendelea na masomo yake katika kiwango cha darasa la tisa na la kumi 
(Standard 9 and 10). Ni sawa na kusema form two kwa lugha ya leo. 
Hatimaye alijiunga na chuo cha Ualimu huko Ikizu, mkoani Mara. 
Alisoma Diploma ya ualimu kwa miaka miwili hatimaye kwenda kuajiriwa 
mwaka 1962. Wakati huo aliamua kujiendeleza na elimu ya kidato cha nne 
bado akiwa kazini kwa kusoma kwa njia ya binafsi (private). 
Alifanya kazi kuanzia mwaka 1962 kwa miaka miwili hatimaye akaenda 
kuchukua kozi ya miaka miwili ya Elimu ya Afya (Health Education) huko 
Hospitali ya Heri, mkoani Kigoma. 
Huo ulikuwa ni mwaka 1964 hadi 1966.Hatimaye ndipo alipoenda kuchukua 
mafunzo ya kichungaji mwaka 1967 hadi 1968 huko Bugema, Uganda. Alipata 
diploma ya uchungaji. 
Safari yake ya elimu iliendelea mwaka 1985 hadi 1988 alipenda India 
katika chuo cha Poona Spicer Memorial College kwa masomo ya digrii yake 
ya kwanza. Na akahamia huko Ufilipino kwa masomo yake ya digrii ya pili.
 Alianza mwaka 1989 hadi 1991. Na kurejea Nyumbani. 
KUAMINI KWAKE
Marehemu mchungaji alipata imani kupitia kwa mzungu mmoja aliyekuja 
kufanya kazi huko Misheni ya Iganzo. Mchungaji Kajula alikuwa akifanya 
kazi kwake ya house boy. Ndipo akawa mtu wa kwanza kupata imani katika 
familia yao.
Tunaweza kusema kuamini kwake ndio chanzo na mlango wa kuwafanya ndugu 
zake wote watano kujiunga na kanisa hili la Waadventista WaSabato. 
Hatimaye mama yake alikuja kuamini baadaye kabisa. Mchungaji Joshua 
Kajula alibatizwa mwaka 1952. Mchungaji aliyembatiza ni Mchungaji 
Jacques
aliyekuwa mmishonari huko Mbeya. 
MAISHA YA NDOA
Marehemu mchungaji Joshua Kajula alifunga pingu za maisha tarehe 12 
Septemba 1964 na Merry Justine Kimera (ni mtoto wa mchungaji Justine 
Salimu Kimera). Ndoa hii ilifungwa na Mchungaji Rufoko aliyekuwa ni 
mwenyeji wa Rwanda huko Heri Hospital ambako mchungaji Kajula alikwenda 
kuchukua masomo ya elimu ya afya. Mungu ameibariki familia hii kuwa na 
watoto watatu. Wa kwanza Gloria, wa pili ni Enidi, na watatu ni Suzzana.
 Na kuwa na wajukuu watano. 
KAZI YA UTUMISHI NDANI YA KANISA
Marehemu mchungaji Kajula alianza rasmi kazi ya utumishi ndani ya kanisa
 kama mwalimu huko Masoko, Rungwe Historia Ya Maisha Ya Marehemu
mkoani Mbeya. Alianza kufundisha shule hiyo ya kanisa mwaka 1962. 
Hatimaye alihamishiwa katika Shule ya msingi Iganzo mwaka huo mwishoni. 
Alifanya kwa awamu mbili ya mwaka 1962 hadi 1964. Akaenda Heri Hospital 
na aliporudi mwaka 1966 alirudi tena Iganzo kama mwalimu. 
Wito wa kichungaji: Marehemu mchungaji Kajula alikuwa na wito huo kwa 
muda mrefu ndipo alipopelekwa kusomea uchungaji katika chuo cha Bugema. 
Aliporudi alipangwa kuwa mchungaji wa Morogoro kuanzia 1969 hadi 1971. 
Lindi mwaka 1972 – 1973. Songea mwaka 1973 kwa miezi sita tu. Hatimaye 
alirudi Lindi tena mwaka 1973 mwishoni mpaka 1975. 
KUWEKEWA MIKONO:
Marehemu mchungaji Kajula aliwekewa
mikono ya kichungaji Novemba 1974. Hii ni ngazi ya mwisho ya kichungaji 
kama uthibitisho wa kudumu wa kutumika katika utumishi huo.
 
Aliitwa kuwa mchungaji wa Zanzibar mwaka 1975 kwa wiki moja. Alienda 
kuripoti tu hatimaye akaambiwa abaki Dar-es-Salaam kuwa mchungaji wa 
Magomeni mwaka 1975 hadi 1977. 
Mwaka 1978 hadi 1985 aliitwa kuwa Mkurugenzi wa Lay Activities (Idara ya
 Huduma za Washiriki) wakati huo ikiwa pamoja na vijana, Dorkas, AMO na 
nyinginezo. Hatimaye ndipo alipokwenda masomoni huko India na Ufilipino.
 
Mwaka 1991 Disemba alirudi masomoni. Na Januari 1992 alipangwa kuwa 
mwalimu wa chuo cha TASC (Tanzania Adventist Seminary College) kwa miezi
 sita tu. Mwaka huo huo alipelekwa kuwa Mwenyekiti wa Mara Conference 
kuanzia 1992 hadi 1996. Hatimaye aliitwa huko Tanzania Union Mission, 
Arusha makao makuu mwaka 1996 kama mkurugenzi wa idara ya Uchapaji na 
maeneo mapya ambapo alifanya kazi hiyo mpaka Januari mwaka 2000. 
Alipelekwa katika Field ya South West Tanzania kuwa mwenyekiti wake 
kuanzia 2000 mpaka 2005. Mwaka 2005 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa 
Union hiyo ya zamani (Tanzania Union Mission) mwaka 2005 mpaka 2010. 
Ndipo alipostaafu kazi ya utumishi ndani ya kanisa Novemba 2010. 
JAMBO ATAKALOKUMBUKWA KATIKA UTUMISHI
Marehemu mchungaji Joshua Kajula atakumbukwa kwa mambo mengi ambayo 
ameyafanya wakati alipokuwa akitumika ndani ya kanisa kwa moyo wake 
wote. Aliishi maisha ya kawaida na kiwango cha chini kwa ajili ya 
kuwafikia waumini wote. Hakuwa na ubaguzi wa kikabila wa kitabaka. 
Aliheshimika na watu wote. Ndio maana hata alipokuwa anakaribia kustaafu
 rasmi 2006; bado kanisa likaona ni vyema aendelee kulitumikia kwa muda 
wa ziada ya miaka mingine mitano ambayo ilikuwa tayari ni nje ya miaka 
ya kustaafu. Kanisa litamkumbuka sana kwa unyenyekevu wake na upole
wake na pia swala la kuzielewa taratibu za kanisa na kuzisimamia vyema. 
Jambo la pekee sana ni pale alipokuwa anapenda kusali kwenye makanisa 
madogo madogo na makundi ya kanisa. Ni jambo ambalo ni nadra sana kwa 
viongozi wa ngazi kama yake kutenda hivyo kwa sababu ya majukumu mazito
waliyonayo. 
Ndugu na jamaa nao wanamkumbuka kama kaka yao ambaye alikuwa na upendo 
wa dhati kwa ndugu wote. Mtiifu kwa wazazi. Mlezi mwema kwa wazazi wake.
 Mdogo wake
Steven Kajula anasema “Kaka alifanya mambo ambayo kwa
tamaduni na desturi za wanaume wa Kinyakyusa hawafanyi.”
Alikuwa mfano wa kuigwa kama Mkristo kwa familia yake na
kwa jamii alimoishi. Alikuwa mcheshi anayechangamana na
watu. Anakumbukwa pia kama mtu aliyekuwa na hobby ya
kuendesha gari. Pamoja na umri mkubwa alikuwa na uwezo
wa kuendesha gari kutoka Dar-es-Salaam hadi Mbeya bila kuchoka katika 
uzee wake huu. Pia alikuwa mtu anayejali sheria
za barabarani kwani mpaka anafariki hajawahi kupata ajali
kwa maisha yake yote. Alikuwa makini sana barabarani. Ni
jambo la kujifunza kwetu sote.
MAJUKUMU MENGINE BAADA YA KUSTAAFU KWAKE
Marehemu mchungaji Kajula alijishughulisha na shughuli zake
ndogo ndogo kwani hakupenda kukaa tu nyumbani bila kazi.
Alifanya shughuli ndogo ndogo kama mtu ambaye amezoea
kufanya kazi muda wote. Lakini bado kanisa lake alilokuwa
anasali, alianza kusali bado likiwa kundi tu hatimaye likapangwa kuwa 
kanisa. Alifanya ushirika na kanisa la Kunduchi tarehe 6 Mei 2012. Na 
kuanzia mwaka 2013 mpaka mauti inapomkuta alikuwa na majukumu ya uzee wa
 kanisa, kiongozi wa uhuru wa Dini, na pia kwa hekima yake alichaguliwa 
awe mshauri wa wazee wa kanisa akishirikiana na mchungaji wa mtaa. 
Alifanya kazi hiyo huku akionyesha utii wa kuhudhuria semina mbalimbali 
zilizoitwa na viongozi wa juu bila kujali aliwahi kuwa kiongozi mkubwa 
wa kanisa katika ngazi ya
Union. 
 Na huku akiunga mipango mikutano yote iliyopangwa na ngazi za juu kwa 
kusimamia vyema katika utekelezaji
wa kanisa lake mahalia. 
MATATIZO YA KIAFYA NA KIFO CHAKE
Marehemu mchungaji Joshua Kajula alianza kuugua mwishoni mwa 
utumishiwake ugonjwa wa kisukari. Lakini aliweza kupata tiba miaka 
michache akapona kwani sukari yake ilirudi katika hali ya kawaida 
kutokana na matibabu aliyoyapata kutoka sehemu mbalimbali.
 
Mnamo mwaka jana alianza kupata tatizo la joto la mwili kupanda juu sana
 bila kushuka. Ndipo alipolazwa katika hospital ya Rabinisinia iliyoko 
maeneo ya Tegeta mwezi wa Disemba tarehe 24 hadi 25. Baadaye 
iligundulika kuwa ilikuwa ni malaria iliyosababisha joto kupanda sana. 
Alitibiwa malaria na Alitoka akawa na udhaifu wa miguu ikawa imepoteza 
nguvu ya kutembea. Hatimaye alianza kupata nafuu ya miguu. Lakini 
ghaflatena mwezi machi mwanzoni joto la mwili likapanda tena. Alipelekwa
 Rabinisia ambako alipimwa. Alilazwa kwa siku moja,aliporuhusiwa alirudi
 nyumbani. Usiku huo huo hali yake ilibadilika na ndipo alipopelekwa 
Muhimbili kwa matibabu zaidi. Siku ya jumatatu alipelekwa Muhimbili 
akapokelewa kama mgonjwa wa dharura (emergency patient) na kupelekwa 
wodini siku ya jumanne mpaka alhamisi. Na hali yake ikazidi kuwa mbaya 
ndipo alipoingizwa Chumba maalumu (ICU) siku ya Alhamisi jioni ambako 
alikaa mpaka Jumamosi Jioni alipofariki hakutoka tena hapo. 
Hivyo marehemu mchungaji Joshua Kamenya Kajula alifariki tarehe 19 MACHI
 2016 SAA MOJA USIKU. 
Hapo ndipo ulipokuwa mwisho wa maisha ya Mtumishi wa Mungu Mchungaji 
Joshua Kamenya Kajula
Copy the BEST Traders and Make Money : http://ow.ly/KNICZ

0 comments:
Post a Comment