Pr Godwin Lekundayo mkiti wa NTUC ndiye anayeongoza ibada ya mazishi ktk kanisa la Mwenge. Kabla ya kuanza hubiri walioimba ni kwaya ya wachungaji wote na wake zao.
KUZALIWA KWAKE
Mchungaji Joshua Kamenya Kajula alizaliwa tarehe 28 Disemba 1939; huko
Maeneo ya Majengo wilaya ya Mbeya Mjini katika Mkoa wa Mbeya. Yeye ni
mtoto wa Pili kuzaliwa kati ya watano kwa mama yake. Baba yake alikuwa
na wake wawili.
Kwa upande wa mama yake ambaye ndiye alikuwa mke wa ndoa kwa baba
walizaliwa wanaume watano. Alikuwa na ndugu wengine wawili waliozaliwa
na baba yake kwa mke mwingine ambaye alirithiwa na baba yake baada ya
kufiwa
na kaka yake. Hivyo, kwa ujumla anatoka katika familia ya watoto saba
kwa baba na kwa mama watano.
ELIMU YAKE
Marehemu mchungaji Kajula alipata elimu yake ya awali katika Shule ya
kati (Middle School) huko Iganzo. Alisoma hapo mpaka darasa la sita
mwaka 1955.
Hatimaye alipelekwa Suji Upper Primary darasa la Saba na la Nane.
Aliendelea na masomo yake katika kiwango cha darasa la tisa na la kumi
(Standard 9 and 10). Ni sawa na kusema form two kwa lugha ya leo.
Hatimaye alijiunga na chuo cha Ualimu huko Ikizu, mkoani Mara.
Alisoma Diploma ya ualimu kwa miaka miwili hatimaye kwenda kuajiriwa
mwaka 1962. Wakati huo aliamua kujiendeleza na elimu ya kidato cha nne
bado akiwa kazini kwa kusoma kwa njia ya binafsi (private).
Alifanya kazi kuanzia mwaka 1962 kwa miaka miwili hatimaye akaenda
kuchukua kozi ya miaka miwili ya Elimu ya Afya (Health Education) huko
Hospitali ya Heri, mkoani Kigoma.
Huo ulikuwa ni mwaka 1964 hadi 1966.Hatimaye ndipo alipoenda kuchukua
mafunzo ya kichungaji mwaka 1967 hadi 1968 huko Bugema, Uganda. Alipata
diploma ya uchungaji.
Safari yake ya elimu iliendelea mwaka 1985 hadi 1988 alipenda India
katika chuo cha Poona Spicer Memorial College kwa masomo ya digrii yake
ya kwanza. Na akahamia huko Ufilipino kwa masomo yake ya digrii ya pili.
Alianza mwaka 1989 hadi 1991. Na kurejea Nyumbani.
KUAMINI KWAKE
Marehemu mchungaji alipata imani kupitia kwa mzungu mmoja aliyekuja
kufanya kazi huko Misheni ya Iganzo. Mchungaji Kajula alikuwa akifanya
kazi kwake ya house boy. Ndipo akawa mtu wa kwanza kupata imani katika
familia yao.
Tunaweza kusema kuamini kwake ndio chanzo na mlango wa kuwafanya ndugu
zake wote watano kujiunga na kanisa hili la Waadventista WaSabato.
Hatimaye mama yake alikuja kuamini baadaye kabisa. Mchungaji Joshua
Kajula alibatizwa mwaka 1952. Mchungaji aliyembatiza ni Mchungaji
Jacques
aliyekuwa mmishonari huko Mbeya.
MAISHA YA NDOA
Marehemu mchungaji Joshua Kajula alifunga pingu za maisha tarehe 12
Septemba 1964 na Merry Justine Kimera (ni mtoto wa mchungaji Justine
Salimu Kimera). Ndoa hii ilifungwa na Mchungaji Rufoko aliyekuwa ni
mwenyeji wa Rwanda huko Heri Hospital ambako mchungaji Kajula alikwenda
kuchukua masomo ya elimu ya afya. Mungu ameibariki familia hii kuwa na
watoto watatu. Wa kwanza Gloria, wa pili ni Enidi, na watatu ni Suzzana.
Na kuwa na wajukuu watano.
KAZI YA UTUMISHI NDANI YA KANISA
Marehemu mchungaji Kajula alianza rasmi kazi ya utumishi ndani ya kanisa
kama mwalimu huko Masoko, Rungwe Historia Ya Maisha Ya Marehemu
mkoani Mbeya. Alianza kufundisha shule hiyo ya kanisa mwaka 1962.
Hatimaye alihamishiwa katika Shule ya msingi Iganzo mwaka huo mwishoni.
Alifanya kwa awamu mbili ya mwaka 1962 hadi 1964. Akaenda Heri Hospital
na aliporudi mwaka 1966 alirudi tena Iganzo kama mwalimu.
Wito wa kichungaji: Marehemu mchungaji Kajula alikuwa na wito huo kwa
muda mrefu ndipo alipopelekwa kusomea uchungaji katika chuo cha Bugema.
Aliporudi alipangwa kuwa mchungaji wa Morogoro kuanzia 1969 hadi 1971.
Lindi mwaka 1972 – 1973. Songea mwaka 1973 kwa miezi sita tu. Hatimaye
alirudi Lindi tena mwaka 1973 mwishoni mpaka 1975.
KUWEKEWA MIKONO:
Marehemu mchungaji Kajula aliwekewa
mikono ya kichungaji Novemba 1974. Hii ni ngazi ya mwisho ya kichungaji
kama uthibitisho wa kudumu wa kutumika katika utumishi huo.
Aliitwa kuwa mchungaji wa Zanzibar mwaka 1975 kwa wiki moja. Alienda
kuripoti tu hatimaye akaambiwa abaki Dar-es-Salaam kuwa mchungaji wa
Magomeni mwaka 1975 hadi 1977.
Mwaka 1978 hadi 1985 aliitwa kuwa Mkurugenzi wa Lay Activities (Idara ya
Huduma za Washiriki) wakati huo ikiwa pamoja na vijana, Dorkas, AMO na
nyinginezo. Hatimaye ndipo alipokwenda masomoni huko India na Ufilipino.
Mwaka 1991 Disemba alirudi masomoni. Na Januari 1992 alipangwa kuwa
mwalimu wa chuo cha TASC (Tanzania Adventist Seminary College) kwa miezi
sita tu. Mwaka huo huo alipelekwa kuwa Mwenyekiti wa Mara Conference
kuanzia 1992 hadi 1996. Hatimaye aliitwa huko Tanzania Union Mission,
Arusha makao makuu mwaka 1996 kama mkurugenzi wa idara ya Uchapaji na
maeneo mapya ambapo alifanya kazi hiyo mpaka Januari mwaka 2000.
Alipelekwa katika Field ya South West Tanzania kuwa mwenyekiti wake
kuanzia 2000 mpaka 2005. Mwaka 2005 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa
Union hiyo ya zamani (Tanzania Union Mission) mwaka 2005 mpaka 2010.
Ndipo alipostaafu kazi ya utumishi ndani ya kanisa Novemba 2010.
JAMBO ATAKALOKUMBUKWA KATIKA UTUMISHI
Marehemu mchungaji Joshua Kajula atakumbukwa kwa mambo mengi ambayo
ameyafanya wakati alipokuwa akitumika ndani ya kanisa kwa moyo wake
wote. Aliishi maisha ya kawaida na kiwango cha chini kwa ajili ya
kuwafikia waumini wote. Hakuwa na ubaguzi wa kikabila wa kitabaka.
Aliheshimika na watu wote. Ndio maana hata alipokuwa anakaribia kustaafu
rasmi 2006; bado kanisa likaona ni vyema aendelee kulitumikia kwa muda
wa ziada ya miaka mingine mitano ambayo ilikuwa tayari ni nje ya miaka
ya kustaafu. Kanisa litamkumbuka sana kwa unyenyekevu wake na upole
wake na pia swala la kuzielewa taratibu za kanisa na kuzisimamia vyema.
Jambo la pekee sana ni pale alipokuwa anapenda kusali kwenye makanisa
madogo madogo na makundi ya kanisa. Ni jambo ambalo ni nadra sana kwa
viongozi wa ngazi kama yake kutenda hivyo kwa sababu ya majukumu mazito
waliyonayo.
Ndugu na jamaa nao wanamkumbuka kama kaka yao ambaye alikuwa na upendo
wa dhati kwa ndugu wote. Mtiifu kwa wazazi. Mlezi mwema kwa wazazi wake.
Mdogo wake
Steven Kajula anasema “Kaka alifanya mambo ambayo kwa
tamaduni na desturi za wanaume wa Kinyakyusa hawafanyi.”
Alikuwa mfano wa kuigwa kama Mkristo kwa familia yake na
kwa jamii alimoishi. Alikuwa mcheshi anayechangamana na
watu. Anakumbukwa pia kama mtu aliyekuwa na hobby ya
kuendesha gari. Pamoja na umri mkubwa alikuwa na uwezo
wa kuendesha gari kutoka Dar-es-Salaam hadi Mbeya bila kuchoka katika
uzee wake huu. Pia alikuwa mtu anayejali sheria
za barabarani kwani mpaka anafariki hajawahi kupata ajali
kwa maisha yake yote. Alikuwa makini sana barabarani. Ni
jambo la kujifunza kwetu sote.
MAJUKUMU MENGINE BAADA YA KUSTAAFU KWAKE
Marehemu mchungaji Kajula alijishughulisha na shughuli zake
ndogo ndogo kwani hakupenda kukaa tu nyumbani bila kazi.
Alifanya shughuli ndogo ndogo kama mtu ambaye amezoea
kufanya kazi muda wote. Lakini bado kanisa lake alilokuwa
anasali, alianza kusali bado likiwa kundi tu hatimaye likapangwa kuwa
kanisa. Alifanya ushirika na kanisa la Kunduchi tarehe 6 Mei 2012. Na
kuanzia mwaka 2013 mpaka mauti inapomkuta alikuwa na majukumu ya uzee wa
kanisa, kiongozi wa uhuru wa Dini, na pia kwa hekima yake alichaguliwa
awe mshauri wa wazee wa kanisa akishirikiana na mchungaji wa mtaa.
Alifanya kazi hiyo huku akionyesha utii wa kuhudhuria semina mbalimbali
zilizoitwa na viongozi wa juu bila kujali aliwahi kuwa kiongozi mkubwa
wa kanisa katika ngazi ya
Union.
Na huku akiunga mipango mikutano yote iliyopangwa na ngazi za juu kwa
kusimamia vyema katika utekelezaji
wa kanisa lake mahalia.
MATATIZO YA KIAFYA NA KIFO CHAKE
Marehemu mchungaji Joshua Kajula alianza kuugua mwishoni mwa
utumishiwake ugonjwa wa kisukari. Lakini aliweza kupata tiba miaka
michache akapona kwani sukari yake ilirudi katika hali ya kawaida
kutokana na matibabu aliyoyapata kutoka sehemu mbalimbali.
Mnamo mwaka jana alianza kupata tatizo la joto la mwili kupanda juu sana
bila kushuka. Ndipo alipolazwa katika hospital ya Rabinisinia iliyoko
maeneo ya Tegeta mwezi wa Disemba tarehe 24 hadi 25. Baadaye
iligundulika kuwa ilikuwa ni malaria iliyosababisha joto kupanda sana.
Alitibiwa malaria na Alitoka akawa na udhaifu wa miguu ikawa imepoteza
nguvu ya kutembea. Hatimaye alianza kupata nafuu ya miguu. Lakini
ghaflatena mwezi machi mwanzoni joto la mwili likapanda tena. Alipelekwa
Rabinisia ambako alipimwa. Alilazwa kwa siku moja,aliporuhusiwa alirudi
nyumbani. Usiku huo huo hali yake ilibadilika na ndipo alipopelekwa
Muhimbili kwa matibabu zaidi. Siku ya jumatatu alipelekwa Muhimbili
akapokelewa kama mgonjwa wa dharura (emergency patient) na kupelekwa
wodini siku ya jumanne mpaka alhamisi. Na hali yake ikazidi kuwa mbaya
ndipo alipoingizwa Chumba maalumu (ICU) siku ya Alhamisi jioni ambako
alikaa mpaka Jumamosi Jioni alipofariki hakutoka tena hapo.
Hivyo marehemu mchungaji Joshua Kamenya Kajula alifariki tarehe 19 MACHI
2016 SAA MOJA USIKU.
Hapo ndipo ulipokuwa mwisho wa maisha ya Mtumishi wa Mungu Mchungaji
Joshua Kamenya Kajula
Copy the BEST Traders and Make Money : http://ow.ly/KNICZ

Pr Godwin Lekundayo
mkiti wa NTUC
kwaya ya wachungaji wote na wake
zao wakiimba
0 comments:
Post a Comment