Mungu wetu ni mwema sana.Kanisa la Waadventista Wasabato Mbezi luisjijini Dar es salaam nchini Tanzania.Walijielekeza kwenda kufanya Matendo ya Huruma katika maeneo yafuatayo:
1.Gereza la Mkuza
2.Hospitali ya Tumbi-Kibaha
3.Kituo cha kulea watoto yatima -Donbosco Kimara Suka.
Matukio ya picha hapo chini ni washiriki ambao walijielekeza katika kituo cha kulea Watoto yatima cha DONBOSCO KIMARA SUKA .Tulifarijika sana kuwatembelea watoto hawa na tulizidi kuuona mkono wa Mungu.
Tuliweza kuwapatia fedha taslimu Tsh 100,000/=
1.Mafuta ya kupikia Ndoo ndogo 2 za lita 10.
2.Mafuta ya kupaka makubwa na madogo.
3.Sabuni za kufulia na za kuogea. nk
Mungu wetu atusaidie kuyatenda yanayompendeza kwa watu wote.
Safari ikaanza tukiongozwa na Roho wa Mungu.
Washiriki wakiimba wimbo katika ufunguzi wa Ibada.
Mwinjilisti Mashota,Mzee Nyinyimbe na Mchungaji Mapima
Usikivu makini wakati wa Ibada ikiendelea.
Huyo ni Mlezi wa kituo cha Docbosco Kimara Suka
Mwinjilisti MASHOTA akitoa Neno la Mungu
Vijana wakiwapatia wenzao zawadi walizokuwa wamewabebea
Picha ya pamoja baada ya kumaliza Ibada
KATIKA HOSPITALI YA TUMBI KIBAHA ILIKUWA HIVI
Viongozi wa kanisa la SDA Mbezi Luis Pr Kyanzi, mzee wa kanisa Zawadi
Mungereza, viongozi wa vijana Ngoda na Kulwa Jackson wakiongea na
viongozi wa Zamu wa Hospitali wakibadilishana mawazo na kupeana mikakati
ya kuboresha huduma kwa wagonjwa. Hatimaye mchungaji aliwaombea ili
wafanye kazi kwa moyo na Mungu awabariki kwa utumishi mwema. Ni katika
sabato ya matendo ya huduma, Jumamosi ya Leo.
0 comments:
Post a Comment