Subscribe:

Saturday, 16 January 2016

SIKU YA – 10: 

                      KRISTO AKIAKISIWA KWA MAJIRANI:

"Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi." Matendo 1:8

Anzeni kipindi cha maombi kwa kumsifu Mungu kwamba ni mwema, mwenye fadhili na mpole.
Mtukuze Mungu kwamba amechagua kukutumia wewe kuzifikia roho ambazo zina kiu ya maji ya uzima.

Kuungama na Kudai Ushindi dhidi ya dhambi.
Muombe Mungu akuonyeshe dhambi unazohitaji kuziungama kwa wazi na zile unazohitaji kuziungama kwa siri.
Dai ushindi Wake dhidi ya dhambi hizo.
Omba kwa ajili ya msamaha kwa nyakati ambazo uliona haya kushiriki imani yako kwa wengine.
Muombe Mungu akupatie ujasiri na upendo kupitia Kristo kukaa ndani yako.
Mshukuru Mungu kwamba anakusamehe kulingana na 1Yohana 1:9

Sala na Maombezi. Muombe Mungu akupatie mzigo wa kuongoa roho na upendo kwa watoto Wake waliopotea.
Muombe Mungu aweke katika mioyo ya majirani zako njaa na kiu Yake.
Muombe Bwana akujaze na Roho wake Mtakatifu na akufundishe jinsi ya kuwafikia majirani kupitia matendo yako ya upendo, kwa kuhudumia mahitaji yao, kwa wao kukuamini, na kwa kuwaalika kumfuata Yesu.
Omba ili uweze kushiriki uzoefu wa furaha ya kumtangaza Yesu.
Omba kwa ajili ya tabia yenye kupendeza, tabia kama ya Kristo ambayo itawavuta watu kwa Yesu.
Omba ili Mungu akufundishe jinsi ya kuwaelekeza watu kwa Yesu na si kwako mwenyewe.
Omba kwa ajili ya matumizi zaidi ya vitabu vya Kikristo kwa washiriki wote na kwa mkazo zaidi katika uinjilisti wa vitabu, kupitia kwa nakala zilizochapishwa na ambazo ziko katika namna ya kielektroniki.
Omba kwa ajili ya mkazo mpya juu ya umuhimu mkubwa wa kuhudhuria Shule ya Sabato, ambayo inalenga katika ushirika, utume, kujifunza Biblia na huduma nje ya kanisa.
Omba kwa ajili ya mkazo zaidi kwa vikundi vidogo vya kutoa huduma nje ya kanisa, ili washiriki wote waweze kujihusisha katika ushuhudiaji binafsi na kutangaza ukweli mkuu wa Mungu katika siku hizi za mwisho.
Omba ili viongozi wa kanisa (mchungaji wako wa Mtaa, wachungaji wa konferensi, unioni, divisheni na Makao Makuu ya Kanisa waweze kuwa mashahidi wazuri kwa majirani zao.

Utume katika miji Mikuu –
omba kwa ajili ya divisheni ya Inter-Europian na miji waliyoichagua kuifanyia kazi: Geneva, Prague, Vienna. Inua katika maombi pia Unioni za Middle East na North Africa na miji 43 wanayopanga kuifikia katika miaka mine hadi mitano ijayo.
Ombea washiriki wanaofanyia kazi miji hii.
Muombe Mungu kwa ujasiri wa kumshuhudia Yeye katika mazingira yo yote yale.
Omba kwa ajili ya kukua kwa lengo katika huduma ya vyombo vya habari vya kanisa, vikiongoza katika uinjilisti mkubwa wa ushuhudiaji kote duniani.
Omba kwa ajili ya watu saba au zaidi katika orodha yako ili kwamba waone hitaji lao na kufungua mioyo yao kwa Roho Mtakatifu.
Omba kwa ajili ya mahitaji binafsi uliyo nayo.

Shukrani
Mshukuru Mungu kwamba anatenda kazi katika maisha ya watu wa familia yako, marafiki na majirani.
Mshukuru Mungu kwamba anao watu katika kila mji ambao wanatazama mbinguni kwa shauku kuu!
Mshukuru Mungu kwamba anafanya kazi katika mioyo ya wale ambao umekuwa ukiwaombea.

Mapendekezo ya Nyimbo:
Tawala ndani yangu no.147, Taa yangu ndogo nitaiangaza, Walio kifoni no.56, Kuwatafuta wasioweza no.100 

"Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. Matendo 1:8

Watoto wa Mungu wanaitwa wawakilishi wa Kristo, wakionyesha wema na rehema za Bwana. Kama Yesu alivyotufunulia tabia ya kweli ya Baba Yake, nasi tunapaswa kumfunua Kristo kwa ulimwengu ambao haujui upendo Wake wenye upole na huruma. “Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni,” alisema Yesu, “nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.” “Mimi ndani yao, nawe ndani yangu;…..ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma.” Yohana17:18,23. Mtume Paulo anawaambia wanafunzi wa Yesu, “Mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo,” inajulikana na kusomwa na watu wote.” 2Wakorintho3: 3, 2. Katika kila mtoto wa Mungu, Yesu anatuma barua kwa ulimwengu. Kama wewe ni mfuasi wa Kristo, anatuma kupitia kwako barua kwa familia, kijijini, barabarani, mahali unapoishi. Yesu, ndani yako, anatamani kuongea na mioyo ya wale ambao hawamtambui. Huenda labla hawasomi Biblia, au hawaisikii sauti inayoongea nao katika kurasa za Biblia; hawaoni upendo wa Mungu kupitia kwa kazi Zake, lakini wewe ni mwakilishi wa kweli wa Yesu, yaweza kuwa kupitia wewe, wataongozwa kuelewa jambo fulani la wema Wake na kuvutwa kumpenda na kumtumikia Mungu.

Tembelea majirani zako na onyesha kujali wokovu wa roho zao. Amsha kila uwezo wa kiroho katika utendaji. Waambie wale unaowatembelea kwamba mwisho wa mambo yote u karibu. Bwana, Yesu Kristo atafungua milango ya mioyo yao na atafanya katika akili zao mvuto utakaodumu. Hata wakati wanapojishughulisha na kazi zao za kila siku, watu wa Mungu wanaweza kuongoza wengine kwa Kristo. Na wakati wanapofanya hili, watakuwa na uhakika wenye thamani kwamba Mwokozi yupo karibu nao. Hawahitaji kufikiri kwamba wameachwa kutegemea juhudi zao dhaifu. Kristo atawapatia maneno ya kuongea ambayo yataburudisha na kutia moyo na kutia nguvu walio maskini, na roho zinazotaabika katika giza. Imani yao wenyewe itatiwa nguvu wanapotambua kwamba ahadi ya Mwokozi inatimizwa. Wao sio tu mbaraka kwa wengine, bali kazi wanayoifanya huleta mbaraka kwao wenyewe.

Mvuto wako hufikia nafsi; unagusa waya ambao si waya wa kawaida bali waya unaotetema kwenda kwa Mungu…. Ni wajibu wako kuwa Mkristo wa viwango vya juu vya neno, “kama Kristo”. Ni kupitia kwa mistari isiyoonekana inayokuvuta kwa akili za watu wengine ambao unakutanishwa pamoja nao, kwamba kama unadumu katika muunganiko na Mungu, utaacha mivuto ambayo itakufanya kuwa “harufu ya uzima iletayo uzima” Bali, kama wewe ni mbinafsi, kama unajiinua mwenyewe, kama akili yako ni ya kidunia, haijalishi nafasi uliyo nayo, wala uzoefu ulio nao, au kiasi unachojua, kama hauna sheria ya wema katika kinywa chako, harufu nzuri ya upendo inayotiririka kutoka katika moyo wako, huwezi kufanya cho chote kama ipasavyo.

Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba, yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake. (1Yohana 4:20, 21)

Mwonekano wa sura yenye ukweli, uaminifu ya dada au kaka au rafiki ikitolewa kwa namna iliyo ya kawaida kabisa, inayo nguvu ya kufungua milango ya mioyo ambayo inahitaji harufu njema ya maneno yenye kufanana na Kristo na mguso rahisi wa roho ya upendo wa Kristo.

Kote kutuzunguka kunasikikika mayowe ya huzuni iliyopo duniani. Kila mahali wako wahitaji na walio taabuni. Ni sisi tunaohitaji kuongoza katika kuwapoza na kurahisisha magumu ya maisha na huzuni zake. Mahitaji ya roho, ni upendo pekee wa Kristo unaoweza kutosheleza. Kama Kristo atakaa ndani yetu, mioyo yetu itajazwa kwa huruma ya kimbingu. Vijito vilivyofungwa vya upendo wa dhati wakufanana na Kristo vitafunguliwa.

Ni utamu kiasi gani ulitiririka kutoka katika uwepo halisi wa Kristo! Roho hiyo hiyo itaonekana kwa watoto Wake. Wale ambao Kristo anakaa ndani yao watazingirwa na uwepo wa kimbingu. Mavazi yao meupe ya usafi yatakuwa harufu yenye manukato kutoka katika bustani ya Bwana. Nyuso zao zitaakisi nuru kutoka Kwake, zikiangaza njia kwa miguu inayojikwaa na iliyochoka.

Maswali ya Kujitathmini:

 
1.Je, unatamani kujazwa na upendo wa Kristo na kujazwa na huruma kwa ulimwengu unaoangamia?
2.Ni kwa namna gani za kiutendaji unaweza ukashuhudia kwa majirani zako?

0 comments:

Post a Comment