Wednesday, 13 January 2016
SIKU YA – 7:
MAISHA AMBAYO HUBARIKI WENGINE:
“Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Yohana 7:38
Mapendekezo ya utaratibu wa maombi Kusifu (dakika 10) Anzeni kipindi chenu cha maombi kwa kumsifu Mungu kwa jinsi aliyo (tabia Yake). Yeye ni Mungu wa milele, Mungu mvumilivu na mwenye upendo. Mungu ndiye nguvu yetu (Zaburi 27:1) na Yeye ndiye mahali petu pa kupumzika. (Yeremia 50:6). Mtukuze Mungu kwa utayali wake wa kututumia kubariki wengine, hata kama tuna mapungufu na makosa. Mtukuze Mungu kwamba sio sisi ambao tunagusa na kubariki maisha ya watu bali ni Kristo ndani yetu Kuungama na Kudai Ushindi dhidi ya dhambi Muombe Mungu akuonyeshe dhambi utakazoziungama hadharani na zile za kuungama faraghani. Dai ushindi Wake dhidi ya dhambi hizo. Muombe Mungu akusamehe katika nyakati ambazo maisha yako hayakuwa mbaraka kwa wengine. Muombe Mungu msamaha katika nyakati ambazo ulijali zaidi mafaniko yako kuliko kumtumikia Yeye. Mshukuru Mungu kwamba anakusamehe kulingana 1Yohana 1:9. Sala na
Maombezi Mwombe Mungu akupe imani hata pale ambapo shetani hujaribu kukukatisha tamaa usiwahudumie wengine. Muombe Mungu akupe mzigo wa roho za watu wengine na upendo kwa watoto wa Mungu waliopotea. Omba kwa ajili ya tabia inayopendeza, tabia ya kufanana na Kristo itakayowavuta watu kwa Yesu. Omba kwa ajili ya kila mshiriki kuhisi mzigo wa kuongoa roho na kutambua kwamba mbingu inamhitaji kila mmoja kufuata kielelezo cha Kristo kwa kushiriki imani yake akiongozwa na Mungu. Omba kwa ajili ya kutumia vyanzo vyote vya habari vitakavyofaa katika kushiriki ujumbe wa malaika wa tatu katika namna mpya na yenye ubunifu kwa watu wenye shughuli nyingi wa siku hizi. Omba ili idadi iongozeke ya washiriki wote na kujiunga na uinjilisti na taasisi wanapounga mkono utume wa kanisa unaoendelea.
Utume katika Miji Mikuu - Omba kwa ajili ya Divisheni ya Inter-American na miji wanayotamani kuileta kwa Kristo: Mexico, Caracas, Bogatá, Nassau, Belize, Georgetown, Cali, Cayenne, Guatemala, Quetzaltenango, Port-au-Prince, Tegucigalpla, Mérida, kisiwa chote cha Puerto Rico. Santiago de los Caballeros na Maracaibo. Omba ili washiriki waendeleze mikakati ya kufikia miji mikubwa. Omba juu ya kuanzishwa kwa maelfu ya “vyanzo vya vivutio” (makanisa, vituo vya afya, shule za kutwa, mahali vitabu vinapouzwa, vituo vya kuhudumia jamii, vikundi vya vijana, migahawa ya vyakula visivyo na nyama, zahanati na mengineyo) haswa katika miji mikubwa duniani, omba pia vituo hivi vifanye tofauti kubwa katika maisha ya watu wanapopata uzoefu wa ukweli wa Mungu kupitia huduma ya Kikristo. Omba ili kwamba watu saba au zaidi katika orodha yako waone hitaji lao na kufungua mioyo yao kwa Roho Mtakatifu. Omba kwa ajili ya mahitaji binafsi uliyo nayo.
Shukrani (takribani dakika 10) Mshukuru Mungu kwamba anataka kututumia sisi wala sio malaika kuwa watendakazi pamoja Naye kubariki wengine. Mshukuru Mungu kwamba Yesu ametupatia kielelezo cha jinsi ya kuwa mbaraka kwa watu wengine. Mshukuru Mungu kwamba anatuma Roho wake Mtakatifu kufanya kazi katika mioyo ya wale unaowaombea.
Mapendekezo ya Nyimbo: Popote Mashamba Yajaa no. 94
MAISHA AMBAYO HUBARIKI WENGINE
Kila mtu ambaye Kristo anakaa ndani yake, kila ambaye ataonyesha upendo Wake kwa ulimwengu, ni mtendakazi pamoja na Mungu kwa ajili ya kubariki wanadamu wengine. Kadiri mtu huyo anapopokea kutoka kwa Mwokozi neema ya kuwapatia wengine, kutoka katika utu wake wote kunatiririka wimbi la maisha ya kiroho.
Mwanafunzi wa Yesu aliye mnyenyekevu na maskini zaidi anaweza kuwa mbaraka kwa wengine. Watu kama hao wanaweza wasitambue kama wanafanya jema lo lote, lakini kwa mvuto wao bila kutambua wanaweza wakaanzisha mawimbi ya mibaraka ambayo itapanuka na kuzama chini, na matokeo yenye baraka wanaweza wasiyajue hadi wakati wa thawabu ya mwisho. Watu hao hawajisikii wala hawajui kama wanafanya jambo lililo kuu, hawahitaji kujichosha kwa wasiwasi wa kupata mafanikio. Wanahitaji tu kwenda mbele kimya, wakifanya kwa uaminifu kazi ambayo uongozi wa Mungu unaagiza, na maisha yao hayatakuwa bure. Roho zao wenyewe zitakuwa zikikua zaidi na zaidi katika kufanana na Kristo; wao ni watendakazi pamoja na Mungu katika maisha haya, na hivyo wanastahili kazi iliyo bora zaidi na furaha isiyo na kivuli ya maisha yajayo.
Bwana anatuita tuamke katika kutambua wajibu wetu. Mungu amempatia kika mwanadamu kazi yake, hivyo kila mmoja anaweza kuishi maisha yenye manufaa. Hebu tujifunze yote tuwezayo na hatimae tuwe mbaraka kwa wengine kwa kuwapatia maarifa ya ukweli. Hebu kila mmoja atende kwa uwezo wake wote, kwa mamnbo mabalimbali kwa hiari akisaidia wengine kubeba mizigo.
“Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.”
Waweza kuwa mbaraka mkubwa kwa wengine kama utajitoa mwenyewe kikamilifu kwa ajili ya huduma ya Bwana. Utapewa nguvu kutoka juu kama utasimama upande wa Bwana. Kupitia Kristo unaweza kuepuka ufisadi ulioko duniani katika tamaa na kuwa kielelezo cha uadilifu wa kile ambacho Kristo anaweza kufanya kwa wale wanaoshirikiana Naye. Mungu anatamani wanaume kwa wanawake kuishi maisha yaliyo bora.
Mungu anawapatia wanadamu mafanikio ya maisha, si kwa sababu tu ya kupata tu utajiri, bali kuboresha uwezo wao wa juu kwa kufanya kazi ambayo amewakabidhi wanadamu – kazi ya kutafuta kujua na kuleta nafuu kwa mahitaji ya msingi ya wanadamu wenzao. Mtu anapaswa kufanya kazi si kwa manufaa yake binafsi lakini kwa manufaa ya kila anayemzunguka, akiwabariki wengine kwa mvuto wake na matendo mema. Makusudi haya ya Mungu hudhihirika katika maisha ya Yesu., “Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu”. Yakobo 4:6.
Tunapokuwa wanyenyekevu na kusimama tukiwa na hisia za toba tunajiweka mahali ambapo Mungu anaweza na atajifunua mwenyewe kwetu. Yeye hupendezwa sana pale ambapo tunapodai rehema na mibaraka tuliyopewa kipindi kilichopita kama sababu ya Yeye kutumwagia mibaraka mikubwa zaidi. Mungu atatimiza zaidi ya matarajio ya wale ambao wanamtumainia Yeye kikamilifu. Bwana wetu Yesu Kristo anajua kile hasa watoto wake wanachohitaji, na uweza wa uungu kiasi gani ambayo utahitajika kwa mbaraka wa wanadamu; na anatupatia yote ambayo tutahitaji katika kubariki wengine na kuinua roho zetu sisi wenyewe.
Wale ambao wanampenda Mungu kwa dhati watatamani vivyo hivyo kuboresha talanta ambazo amewapatia, ili waweze kuwa mbaraka kwa wengine, na siku kwa siku milango ya mbinguni itafunguliwa wazi kabisa ili kuwaruhusu waingie na kutoka katika mdomo wa Mfalme wa Utukufu baraka zitaanguka katika masikio yao kama muziki wenye nguvu, “Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa kwa ulimwengu.” Mathayo 25:34
Maswali ya Kujitathmini:
1. Ni mambo gani madogo unayoweza kufanya ili yawe mbaraka kwa wale wanaokuzunguka?
2. Mara nyingi ni rahisi kuwa mbaraka kwa watu walio mbali kuliko kwa familia yako. Je wawezaje kuwa mbaraka kwa wale walio karibu nawe?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment