Subscribe:

Wednesday, 13 January 2016



SIKU YA – 6:

         FURAHA YA UTII:

Nami nitajifurahisha sana kwa maagizo yako, ambayo nimeyapenda. Zaburi 119:47

Mapendekezo ya utaratibu wa maombi
Kusifu (dakika 10)
Anzeni kipindi chenu cha maombi kwa kumsifu Mungu kwa jinsi alivyo (Tabia Yake), Yeye ni yote katika yote, mfariji, Mhuishaji n.k
Mshukuru Mungu kwa ajili ya Yesu, ambaye ametuonyesha maana ya kuwa na furaha ya utii.
Mshukuru Mungu kwamba kuna shangwe, amani na furaha katika kumtii Kristo.
Kuungamana na Kudai Ushindi dhidi ya dhambi (dakika 5)
Muombe Mungu akuonyeshe dhambi unazohitaji kuziungama faraghani, dai ushindi dhidi ya dhambi hizo.
Mshukuru Mungu kwamba anakusamehe kulingana na 1Yohana 1:9.
Sala na Maombezi (dakika 35)
Je unayo furaha katika kutenda yale Mungu anayokuagiza? Omba kwamba Mungu akupe uhiari wa kumtii Yeye na furaha katika kufanya cho chote anachoagiza.
Omba ili kwamba upendo wa Mungu uweze kukamilishwa katika kanisa Lake.
Omba kwa ajili ya mkazo zaidi katika fundisho la kipekee la uumbaji katika Biblia – kwamba dunia yetu iliumbwa kwa siku halisi sita, zinazofuatana kwa neno la Mungu.
Omba kwa ajili ya ongezeko kubwa katika utegemezaji wa vijana wa Kiadventista ambao wanasoma katika shule za umma. Omba kwamba vijana hao waweze kuwa wamishenari wenye nguvu ambao watahudumia vijana wenzao katika vyuo vya kawaida na vyuo vikuu vya kiserikali.
Omba kwa ajili ya ushirikiano wenye nguvu na umoja katika mfumo wa kanisa na huduma za kanisa zinazounga mkono uinjilisti katika jamii.
Msihi Bwana aweze kulea na kujipatia viongozi wacha Mungu, wanaokuwa tayari kufundishwa na wanyenyekevu kwa ajili ya kipindi kijacho, viongozi ambao wataonyesha mfano wa uongozi ambao kiini chake ni Kristo, wakati kanisa la Mungu linapotimiza wajibu wake toka mbinguni wa kutangaza ujumbe wa malaika wa tatu na haki ya Kristo kama msingi Wake.
Utume katika Majiji – Omba kwa ajili ya Divisheni ya Amerika ya Kaskazini: New York, Calgary, Indianapolis, St. Louis, Seattle, San Francisco, Oakland, Tampa, jiji la Oklahoma. Omba pia kwa ajili ya Divisheni ya Northern Asia-Pacific na miji wanayokusudia kuifikia: Tokyo, Daegu, Daejon, Wuxi, Ulaanbaatar, Taipei. Omba kwa ajili ya Roho wa Mungu kufanya kazi kwa nguvu katika miji hii.
Omba ili washiriki wa kanisa na jamii waelewe umuhimu wa matengenezo ya afya kama sehemu ya kilio kikuu kuwarejesha wanadamu katika sura ya Mungu kupitia kwa haki ya Kristo. Omba kwamba watu wote waweze kuukubali mtindo wa maisha wenye afya na kiasi na kwamba miili yetu itunzwe kama mahekalu ya Roho Mtakatifu, ili kutusaidia kupokea maono muhimu kutoka kwa Mungu.
Omba ili kwamba watu saba au zaidi katika orodha yako waweze kuona hitaji lao na kufungua mioyo yao kwa Roho Mtakatifu.
Omba kwa ajili ya mahitaji yako binafsi. Shukrani
Mshukuru Mungu kwamba kupitia Kristo waweza kusema, kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu (Zaburi 40:8).
Mshukuru Mungu kwamba anao watu wake katika kila mji ambao wanaotazama mbinguni kwa shauku kubwa!
Mshukuru Mungu kwamba anainua viongozi wacha Mungu, wanyenyekevu na walio tayari kufundishwa kwa ajili ya wakati ujao.
Mapendekezo ya Nyimbo
Namwandama Bwana no. 128, Yesu Mwokozi kwa Hakika no. 51, Ni salama Rohoni Mwangu no.127, Mwanga Umo Moyoni no. 45
FURAHA YA UTII
Nami nitajifurahisha sana kwa maagizo yako, ambayo nimeyapenda. Zaburi 119:47
Bwana amekusudia kwamba kila roho inayotii neno Lake itakuwa na Furaha Yake, amani Yake, na nguvu yake inayodumu katika kutunza. Wanaume na wanawake watiio kama hao daima huvutwa karibu Naye, si wakati tu wanapopiga magoti kuomba, bali wakati hata wakiendelea na shughuli zao za maisha. Mungu ameandaa kwa ajili yao sehemu ya kukaa ndani Yake, mahali ambapo maisha hutakaswa toka katika uchafu wote na machukizo yote. Kwa ushirika huu pamoja Naye, wanafanywa watendakazi pamoja Naye katika maisha yao yote.
Kristo anapokaa ndani ya moyo, roho itajazwa na upendo Wake, na kwa sababu ya furaha ya ushirika pamoja Naye, ambayo itachoma moyo wake na katika kumtafakari Yeye, ubinafsi utasahauliwa. Upendo kwa Kristo utakuwa sababu ya utendaji. Wale ambao wanaohisi upendo wenye nguvu wa Mungu, hawaulizi ni kiasi gani kidogo kinachoweza kutolewa ili kutimiza matakwa ya Mungu; hawaulizii viwango vya chini, lakini hulenga katika uliganifu kamili wa nia ya Mwokozi wao. Wakiwa na shauku ya dhati hutii yote na kudhihirisha faida linganifu na thamani ya jambo lile wanalolitafuta.
Ni roho ile yenye utii, yenye kukubali mafundisho ambayo Mungu huitaka. Kile kinachofanya ombi liwe bora ni ukweli kwamba linatoka katika moyo wenye upendo na utii.
Mkinipenda mtazishika amri zangu. (Yohana 14:15).
Mtu yule ambaye anajaribu kuzishika amri za Mungu kutokana na kutii wajibu tu, kwa sababu anahitajika kufanya hivyo –kamwe hataingia katika furaha ya utii, kwani hatii. Wakati matakwa ya Mungu yanapohesabiwa kuwa mzigo, kwa sababu yanapingana na mazoea ya kibinadamu, tunaweza kutambua kwamba maisha hayo si maisha ya Kikristo. Utii wa kweli ni matokeo ya kanuni ambayo imo ndani. Hutiririka kutoka katika upendo wa haki, upendo kwa sheria ya Mungu. Kiini cha haki yote ni uaminifu kwa Mwokozi wetu. Hii itatuongoza katika kufanya mambo sahihi kwa sababu mambo hayo ni sahihi – kwa sababu kufanya mambo sahihi ni kumpendeza Mungu.
Tuko katika dunia hii ili tuwe msaada na mbaraka kwa kila mmoja wetu, tukiunganishwa na Kristo katika juhudi ya kurejesha sura ya Mungu kwa mwanadamu. Ili kufanya kazi hii, ni lazima tujifunze kutoka kwa Yesu. “Jitieni nira yangu,” anasema “mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo: nanyi mtapata raha nafsini mwenu.” Katika ahadi hii hakuna “kama”. Wale ambao wamepata uzoefu wa kujitia nira ya Kristo ya kujitawala na utii wanajua kwamba inamaanisha kupata pumziko na amani katika Yeye. Katika utii kuna furaha na farijiko. Malaika watakatifu huwazingira watiifu ili kuwatunza katika njia za amani.
Hakuna imani iokoayo katika Kristo pekee kama ambayo inadhihirishwa katika utii. Kila mwanadamu yupo chini ya wajibu mkubwa wa kumtii Mungu. Uwepo wa Mungu na furaha ya milele inategemea na utii wa hiari wa mtu kwa matakwa ya mbingu. Nia ya mtu na matakwa yake yapaswa yasalimishwe kwa Mungu. Wakati hilo linapofanyika, mtu atashirikiana na Mungu akionyesha kwa mwenendo na kwa kielelezo kuwa amechagua kuwa chini ya utawala wa Muumbaji wake katika njia zake zote. Mungu anafurahi wakati ambapo, kama Musa, watoto wake wanaamua kuchagua kumtumikia Yeye badala ya kufarahia anasa za dunia hii. Kama pazia lingeweza kufunuliwa, kama wanadamu wangeweza kuona jeshi la malaika wakimtukuza Mungu kwa nyimbo za shangwe na furaha, wangetambua kwamba utii daima huleta furaha na kutokutii huleta huzuni. Mungu na malaika hushangilia juu ya kila ushindi apatao Mkristo; lakini jaribu linapoishinda nafsi, kunakuwepo huzuni mbinguni.
Tunaupeleka uongo kwenye ukweli na kumtukuza shetani pale ambapo tunatembea tukiwa na huzuni na majonzi kwa sababu tunadhani kwamba matakwa yanayohitajika kwetu katika maisha ya Kikristo ni mengi kuliko vile tuwezavyo. Mkombozi wako anakupenda, na anakupatia furaha za umilele katika maisha ya utii. Hakuna ambaye amewahi kuonja furaha ya utii mkamilifu na wa hiari kwa Mungu, ambaye hakupata amani, furaha na uthibitisho wa pendo Lake.

Maswali ya Kujitathmini:
Je unapitia uzoefu wa utii kwa Kristo?
Je kuna jambo lo lote linalokuzuia kupata furaha katika kumtii Mwokozi wako mpendwa?

0 comments:

Post a Comment