BADO KAZI YA KUTANGAZA INJILI INAENDELEA RWANDA NA CONGO:
Mikutano hii ya Injili inayoendeshwa Nchini Rwanda na Congo imekuwa ikiwabariki sana watu wa Mungu kwa kuweza kulisikia Neno lake.
Mungu amekuwa akitenda miujiza ya pekee sana na amekuwa akizidi kuwa Nuru kwa watu wote.
Watu 30,000 wamebatizwa hadi sasa tangu kuwepo
kwa ushirikishwaji huu wa wanachama ambapo shughuli hii ya Mikutano mikubwa ya
Injili ilianza mwezi Mei. Mei 28 , 2016, Nchini Rwanda kutakuwa na Ubatizo
Mkubwa sana siku ya kuhitimisha ambayo itakuwa ni ya Sabato. Tunamshukuru Mungu
kwa nguvu zake za ajabu katika maisha ya watu wengi.
Mch TED WILSON akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa Makanisa mbalimbali.
Watu waliojitoa kwa Kubatizwa wakijiweka tayari kwa tukio la Ubatizo
Eneo la kufanyia Ubatizo likiwa linaonekana katika madhari nzuri na yenye Utukufu.
Wabatizwa wakifanya kiapo juu ya kufuataNeno la Mungu kabla ya kubatizwa.
Ubatizo ukiwa umeanza na watu wakiendelea kubatizwa.
Ubatizo ukiendelea katika eneo la Ziwa KIVU.
Urafiki wa kweli na wa Kudumu daima.Kazi ya Mungu ndivyo inavyopaswa kufanywa.
Mke wa Mch TED WILSON yaani NANCY TED WILSON akihakikisha rafiki yake MARTHA ambaye ameamua kumpokea Yesu kwa njia ya kufanyiwa Ubatizo.
Wakati MARTHA akiwa anafanya ukubali wa kulishika agizo la Mungu kwa njia ya kiapo.
MARTHA ambaye ana Umri wa miaka 89 akiwa anasindikizwa kwenda kubatizwa.
Tayari MARTHA amebatizwa ni furaha kubwa Duniani na Mbinguni pia. Mungu atukuzwe.
0 comments:
Post a Comment