Hivi karibuni imefanya mabadiliko ya viongozi na watendaji wa taasisi za kanisa hilo.
Kupitia taarifa iliyotolewa leo kwa wafanyakazi wa Morning Star Radio na Morning Star Televisheni na Mshauri na mlezi wa Taasisi hizo Mchungaji Robson Nkoko kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya unioni Mchungaji Magulilo Mwakalonge ambaye ndiye mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato katika Union hiyo, imemteua Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Unioni hiyo Mchungaji Robson Nkoko kusimamia utendaji wa vyombo vya habari vya kanisa hilo.
Na aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari vya Kanisa hilo, Mchungaji Musa Mika ameitwa kufanya kazi ya kufasiri katika kiwanda cha uchapishaji cha kanisa (TAP) kilichopo mjini Morogoro.
Aliyekuwa Mhazini wa Tanzania Adventist Press Bwana Mathias Mavanza
amechaguliwa kushika nafasi ya aliyekuwa Mhazini wa Taasisi ya Vyombo
vya Habari vya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania, Koheleth
Manumbu, ambaye ameitwa kuwa Mhasibu wa Kitengo cha Huduma ya Nyumbani,
Elimu na Maisha Bora (HHES) kilichopo Morogoro.
Kanisa la Waadventista wasabato nchini Tanzania inamiliki Morning Star Radio, Studio ya Redio ya Waadventista Ulimwenguni na Morning Star Radio.
Picha ya kwanza ni Mch Robson Nkoko akizungumza na wafanyakazi wa Morning Star Radio na TV picha ya Pili ni Mathias Mavanza(mwenyemiwani)katika picha na baadhi ya wafanyakazi