Subscribe:

Sunday, 12 June 2016

MKUTANO WA TAiN-DODOMA WAISHA KWA NAMNA YAKE:

Ule Mkutano wa wana mawasiliano katika makanisa ya waadventista wasabatoTanzania ulihitimishwa jana katika kanisa la waadventista wasabato Dodoma kati.
Mkutano huu ambao ulikuwa na lengo kubwa la kuweza kukuza Injili ya Yesu kwa UBUNIFU ZAIDI kwa njia ya MAWASILIANO.
Mungu azidi kututangulia pale ambapo mimi na wewe tumedhamiria kuifanya kazi ya Mungu kwa kutumia mitandao ya kijamii yaani "FACEBOOK, WHATSAPP, nakadhalika.

 Mr. Mark Imori ambaye ni karani wa kanisa la Dodoma kati Aibuka kuwa amshidi kwa Tanzania nzima kwa kuingiza majina ya washiriki wote Wa kanisa la Dodoma kati katika Mfumo wa ACMS.
Pembeni yake ni Mke wake.


Saturday, 11 June 2016

IBADA YA LEO ILIVYOFANA:

SOMO:NJIA YA KUUFIKIA UKUU "UNYENYEKEVU"
MNENAJI: MCH PRINCE BAHATI.

                                    Kwaya ya UJASIRI wakitubariki kwa wimbo.


 NJIA SABA ZA UNYENYEKEVU:

1.Ulimwengu huu sio wa kwako.
2.Huna uwezo wa kuwa kila mahali katika ulimwengu huu.
3.Huna uwezo usio na Ukomo.."Kisa cha Naamani "2 Wafalme 5:11"
4.Haujui kila kitu ,Yeyote anaweza kuchukua nafasi yako.
5.Wewe unapita na unapotea,Wewe sio wa milele "Zaburi 90:9".
6.Kuwa Mnyenyekevu usijisifie kila mara "Zaburi 146:1"
7.Wewe ni Mdhambi uliyeokolewa na Neema ya Mungu "2 Wakorintho 12:9"



ULE MJADALA WA KUJIFUNZA BIBLIA ULIFANIKIWA KUFANYIKA KWA NAMNA HII:

Katika Sabato ya leo ndani ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Dodoma kati kumefanyika mjadala wa lesson na kumejadiliwa mambo mbalimbali yakiwemo kumuinua Kristo katika kipindi hiki cha siku za mwisho.Fungu la kukariri likitoka kitabu cha:

Mathayo 23:12  "Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa."






IBADA YA LEO HAPA DODOMA KATIKA KUFUNGA MKUTANO WA TAiN:

Ni Ibada ya kumsifu Mungu na kumtukuza kwa yale makuu ambayo ametutendea takribani wiki nzima ambapo tulikuwa katika Mkutano Mkubwa wa WANAMAWASILIANO -TAiN-DODOMA.

Endelea kuwa nasi kufahamu ambayo yatajiri siku nzima ya leo.
Endelea pia kuombea IBADA ya leo.

        Guheni Mbwana ,Dr Mbwambo ,Mch Steven Bina wakiwakilisha sauti ya NNE.

        Viongozi mbalimbali wa kanisa wakiweka umakini katika kusikiliza Ibada ya leo.



      Uncle Bulengela akifanya jambo la Uimbishaji wa Nyimbo za kusifu katika asubuhi ya leo.

                                  Hapo ni kusifu kwa Nyimbo na kuabudu.


Friday, 10 June 2016

KAMBI LA VIJANA MASASI LIKIWA LINAENDELEA KWA KASI:

Mungu wetu ni mwema sana kwa makuu ambayo anazidi kuwatendea vijana hawa wa kanisa la Waadventista Wasabato ambao wameamua kabisa na kudhamiria kuifanya kazi ya Mungu kwa juhudi kubwa sana.
Mafunzo ambayo wanayapata wawapo huko MASASI ni mazuri ambapo wanakuwa wakakamavu na makini pale ambapo wanaifanya kazi ya Mungu kwa sababu kazi ya Mungu haifanywi kwa ulegevu.
Tuzidi kuwakumbuka katika Maombi sana.





WANA MKUTANO WA TAiN-DODOMA WAKIWA KATIKA ZIARA YA BUNGENI:

Wana TAiN Wakiwa Nje ya Ukumbi wa Bunge hii Leo Baada yakusikiliza Mjadala wa Wizara ya Fedha Uliyo kuwa ukiendelea.
Mikutano Ya TAiN iliyo anza tarehe 05/06/2016 inategemea kuisha kesho na hatimaye Jumapili watu watakuwa wakitawanyika kuelekea Pande Nne za Nchi ya Tanzania.
 Endelea kutuombea sana..
 




Thursday, 9 June 2016

MKUTANO WA TAiN-DODOMA WAFANYA JAMBO KUBWA KWA JAMII:
 


Zawadi hii imetolewa na Mchungaji David Makoye(aliye kulia) Katibu mkuu wa Unioni ya kusini mwa Tanzania na Watatu kutoka kulia ni Mchungaji Rabson Nkoko Katibu Mkuu wa Unioni ya kusini mwa Tanzania Mr
Haggai Abuto IT Manager wa Division

Ndugu Paulo ametokea Kanisa la Mugaja Bunda Mkoa wa Mara kama mkuu wa mawasiliano wa kanisa.
 
 
 Zawadi hii imetolewa na Mchungaji David Makoye(aliye kulia) Katibu mkuu wa Unioni ya kusini mwa Tanzania na Watatu kutoka kulia ni Mchungaji Rabson Nkoko Katibu Mkuu wa Unioni ya kusini mwa Tanzania Mr
Haggai Abuto IT Manager wa Division