Subscribe:

Tuesday, 7 June 2016

MAADILI YA MWANA MAWASILIANO:

MNENAJI: MCH STEVEN BINA



Mchungaji Steven Bina, Mkurugenzi wa Mawasiliano Mstaafu - ECD Amefundisha Maadili 10 ya Mawasiliano kwa kanisani la waadventista wa Sabato. Amesema hayo hii leo katika mkutano wa TAiN Dodoma katika kipindi kilicho isha sasa hivi. 
  1. Hakikisha Kila unacho wasiliana kiwe kinamtukuza Mungu
2. Hakikisha Unatoa Ujumbe wa Upendo wa Matumaini wa Marejeo ya Yesu
3.Hakikisha unazingatia ethos (desturi) , beliefs(Imani) , na Values(mambo tunayo yadhamini)
4. Hakikisha uko tayari kushirikiana, kuunga Mkono vyombo vya habari, Ungamkono Ujumbe, heshimiana na wanahabari. Kwani huu ni wajibu wa Mwana Mawasiliano.
5 . Hakikisha una uhuru wa kuwasiliana kwa uadilifu, uwazi, ukiwa na kusudi, mwaminifu, makini, diversity and excellence.
6. Hakikisha unazingatia ukweli na Uaminifu.
7. Hakikisha nyumba zetu za Habari zielekeze juu ukweli unaotakiwa na kuhuisha wasikilizaji.
8. Kila mwana Mawasiliano ahakikishe anajiendeleza na kupanua uelewa wako.
9. Hakikisha Mawasiliano yako hayana mgongano wa masihara na upendeleo wakirafiki na kindugu.
10. Hakikisha shughuli zote za Mawasiliano zinazingatia Utambulisho wa kanisa.

0 comments:

Post a Comment