Our Greatest Gift to God: Our Being:
“I beseech you
therefore, brethren, by the mercies of God, that you present your bodies a
living sacrifice, holy, acceptable to God, which is your reasonable service.”
Rom. 12:1
Christ taught His disciples that the amount of divine
attention given to any object is proportionate to the rank assigned to it in
the creation of God. He called their attention to the birds of the air. Not a
sparrow, He said, falls to the ground without the notice of our heavenly Father.
And if the little sparrow is regarded by Him, surely the souls of those for
whom Christ has died are precious in His sight. The value of man, the estimate
God places upon him, is revealed in the cross of Calvary.
“God so loved the world, that He gave His only-begotten Son, that whosoever
believeth in Him should not perish, but have everlasting life.” And will not
God judge those who cause pain or disappointment to the ones for whom Christ
has given His life? Then let men be careful how, by word or action, they cause
one of God’s children sorrow or grief. (The Signs of the Times, Nov. 17, 1898)
Christ made a complete sacrifice in our behalf, when He gave
Himself as an offering for sin; and He asks us to give ourselves entirely to
Him. He asks for the whole heart; He will accept nothing less than the
undivided affections. “God is a Spirit, and they that worship Him must worship
Him in spirit and in truth.” (The Signs of the Times, Feb. 1, 1899)
What? know ye not that your body is the temple of the Holy
Ghost which is in you, which ye have of God, and ye are not your own? For ye
are bought with a price: therefore glorify God in your body, and in your
spirit, which are God’s. (1 Cor. 6:19, 20, KJV)
Whether we give ourselves to the Lord or not, we are His. Ye
are not your own; ye are bought with a price. We are the Lord’s by creation,
and we are His by redemption. Therefore we have no right to think that we can
do as we please. All we handle is the Lord’s. We have no right of ourselves to
anything, not even to an existence. All our money, time, and talents belong to
God, and are lent us by Him that we may accomplish the work He has given us to
do. He has given us the charge, “Occupy till I come.” Luke 19:13. (Our High
Calling, p. 42)
The love of Christ in the heart is what is needed. Self is
in need of being crucified. When self is submerged in Christ, true love springs
forth spontaneously. It is not an emotion or an impulse, but a decision of a
sanctified will. It consists not in feeling, but in the transformation of the
whole heart, soul, and character, which is dead to self and alive unto God. Our
Lord and Saviour asks us to give ourselves to Him. Surrendering self to God is
all He requires, giving ourselves to Him to be employed as He sees fit. Until we
come to this point of surrender, we shall not work happily, usefully, or
successfully anywhere. (Letter 97, 1898)
I see before me today those whom I know God can use if they
will put their dependence in Him. … It is an honor to follow the Saviour. And
it is by obeying the instructions that He has given that you are to be prepared
to meet Him when He comes. If you will ask God to help you to overcome what is
un-Christlike in your dispositions, He will prepare you for entrance into
heaven, where no sin can enter. Those who daily give the life to Jesus, and who
follow on to know Him, will be greatly blessed. Say, Christ gave His life for
me, and I must give my life for Him. If you give yourselves wholly to Him, you
will be conquerors in the warfare against sin. The Lord Jesus will be your
helper, your support, your strength, if you will receive and obey Him. (The
Youth’s Instructor, June 9, 1914)
In the parable the pearl is not represented as a gift. The
merchantman bought it at the price of all that he had. Many question the
meaning of this, since Christ is represented in the Scriptures as a gift. He is
a gift, but only to those who give themselves, soul, body, and spirit, to Him
without reserve. We are to give ourselves to Christ, to live a life of willing obedience
to all His requirements. All that we are, all the talents and capabilities we
possess, are the Lord’s, to be consecrated to His service. When we thus give
ourselves wholly to Him, Christ, with all the treasures of heaven, gives
Himself to us. We obtain the pearl of great price. (Maranatha, p. 72)
Questions for Personal Reflection:
1. You are so precious in God’s eyes that He did everything
to make you His own. How does this make you feel?
2. Think about what Jesus gave for you so that heaven could
be yours. Is it worth giving yourself daily to Him? Isn’t it the most
reasonable thing to do?
SIKU YA-2: UHAI WETU- ZAWADI YETU KUU KWA
MUNGU:
“Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake
Mungu, itoeni milli yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu,
ndiyo ibada yenu yenye maana.” Warumi 12:1
Mapendekezo ya Utaratibu wa Kipindi cha
Maombi Kusifu (kama dakika 10) Anzeni kipindi
cha maombi kwa kumsifu Mungu jinsi alivyo: Yeye ni mwaminifu, Yeye anajua yote
n.k. Msifu Mungu kwamba amesubiri kwa muda mrefu ili wewe uweze kumpatia moyo
wako wote. Mshukuru Mungu kwamba haitaji tu sehemu yako lakini anakuhitaji wewe
na talanta zako zote na mapungufu yako.
Msifu Mungu kwa namna ambazo
anakufundisha kukaa ndani Yake. Kuungama na Kudai Ushindi dhidi ya dhambi (kama dakika 5) Muombe Mungu akuonyeshe dhambi ambazo
unahitaji kuziunganma kwa uwazi na zile unazohitaji kuziungama faraghani. Dai
ushindi juu ya dhambi hizo. Muombe Mungu msamaha kama
hukuwa ukisalimisha maisha yako kila siku Kwake? Muombe Mungu msamaha kwa
nyakati ambazo ulitumia muda wako, pesa na talanta kwa ajili yako mwenyewe na
si kwa ajili Yake na kwa utukufu Wake. Mshukuru Mungu kwamba anakusamehe
kulingana na 1Yohana 1:9. Sala na Maombezi (takribani dakika 35) Muombe Mungu
aondoe cho chote kile ambacho ambacho kinakuzuia kusalimisha muda, fedha,
nguvu, uwezo, hofu na nia yako. Mwambie Mungu unataka kumilikiwa kikamilifu na
Kristo. Muombe ili Mungu akusaidie kuomba kama
Yesu, “walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke” (Luka 22:42) Je kuna
jambo lo lote linalokuzuia kumpa Yeye uhai wako na moyo wako wote? Mwambie Yeye
mambo hayo.
Muombe akufanye uwe radhi kuyasalimisha Kwake. Omba kwa ajili ya
wanafamilia yako na marafiki ambao hawajajitoa kikamilifu kwa Kristo. Muombe
awafanye wawe wawe radhi kusalimisha uhai wao Kwake. Omba kwamba mchungaji wako
wa mtaa na viongozi wa kanisa katika ngazi zote watoe maisha yao yote kwa Mungu. Omba kwa ajili ya vijana
wa kanisa letu kupata furaha katika kusalimisha maisha yao kwa Kristo na kumfuata. Wainue vijana wa
kanisa lako kwa majina yao
kupitia kwa maombi. Omba kwamba kila kiongozi wa kanisa duniani ashikilie kwa
kina mtazamo wa kiroho na wa kiinjilisti. Msihi Bwana awalinde wachungaji na
washiriki dhidi ya kupoteza utambulisho wa jinsi tulivyo kama
Kanisa la Waadventista Wasabato, kanisa la masalio la Mungu katika kipindi cha
mwisho. Utume Katika Miji Mikuu – Omba kwa ajili ya Divisheni ya Trans-Europian
na miji wanayojitahidi kuileta kwa Kristo: London,
Zagreb, Tallinn, Dublin, Copenhagen, Helsinki, Budapest, Bergen, Randstad, Warsaw, Belgrade, Gothenburg,
omba kwa ajili ya watu kupata njaa kali kwa ajili ya neno la Mungu. Omba ili
kwamba watu saba au zaidi katika orodha yako waone hitaji lao na kufungua mioyo
yao kwa Roho
Mtakatifu. Omba kwa ajili ya mahitaji binafsi uliyo nayo. Shukrani (takribani
dakika 10) Mshukuru Mungu kwamba atajibu kulingana na mapenzi Yake na kwa
wakati Wake. Mshukuru Mungu kwamba yupo tayari kuchukua moyo wako wenye dhambi
na kuufanya kuwa safi
na mtakatifu. Mshukuru Mungu kwamba Yesu alikuwa tayari kuishi na kufa, sio kwa
ajili Yake lakini kwa mapenzi yake Yule aliyemtuma. Mshukuru Mungu kwa
kujifunua kwa namna ya pekee katika maisha yako kwatika kipindi hiki cha siku
kumi.
Mapendekezo ya Nyimbo “Tawala Ndani Yangu”
no 147, “Nina Haja Nawe” no.126, Univute Karibu” no 148, “Yote Namtolea Yesu”
no 122, “Karibu Sana Univute no. 33.
Kristo aliwafundisha wanafunzi Wake kwamba
kiwango cha uangalifu wa kimbingu kwa kitu cho chote huwa sawia na kiwango cha
jukumu lililopo kwa kitu hicho katika uumbaji wa Mungu. Kristo alivuta usikivu
wa wanafuzi wake kwa mfano wa ndege wa angani. Hakuna shomoro, alisema haanguki
chini asipojua Baba wa mbinguni. Na kama ndege
huyo mdogo hutambuliwa na Mungu, kwa hakika roho za wale ambao Kristo aliwafia
ni za thamani mbele Zake. Thamani ya mtu, kiwango ambacho Mungu anakiweka juu
ya mwanadamu, hufunuliwa katika msalaba wa Kalvari. “Kwa maana jinsi hii Mungu
aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye
asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Je Mungu hatawahukumu wale ambao
wanasababisha maumivu au huzuni kwa wale ambao Kristo alitoa uhai Wake kwa
ajili yao?
Hivyo wanadamu sasa wawe waangalifu kwa namna ambavyo kwa maneno au matendo
wanawasababishia watoto wa Mungu huzuni na majonzi. Kristo alitoa kafari kamili
kwa niaba yetu, pale alipojitoia mwenyewe kama
sadaka ya dhambi na anatutaka sisi kujitoa kikamilifu Kwake, Yesu anahitaji
moyo wote; hatapokea pungufu ya upendo usiogawanyika. “Mungu ni Roho, na wote
wamwabuduo wamwabudu katika roho na kweli. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni
hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu
wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili
yenu. (1Wakorintho 6: 19,20) Iwe tunajitoa kwa Mungu au la, sisi ni Wake. Ninyi
si mali
yenu wenyewe; mlinunuliwa kwa thamani. Sisi ni mali
ya Bwana kwa uumbaji na sisi ni mali
Yake kwa ukombozi. Hivyo hatuna haki ya kufikiria kwamba tunaweza kufanya vile
tupendavyo. Yote tunayoshikilia ni mali ya Bwana. Hatuna haki sisi
wenyewe kwa jambo lo lote, hata kuwepo haipo. Fedha zako zote, wakati na
talanta vyote ni mali
ya Mungu na vimeazimwa kwetu na Yeye ili kwamba tukamilishe kazi ambayo
ametupatia. Ametupatia agizo, “Fanyeni biashara hata nitakapokuja” Upendo wa
Kristo katika moyo ndicho kinachohitajika. Ubinafsi wapaswa kusulubishwa.
Wakati ubinafsi unapozamishwa katika Kristo, upendo wa kweli utatiririka kwa
uhiari. Sio hisia wala msukumo lakini uamuzi nia iliyotakaswa. Haipo katika
hisia lakini katika kubadilishwa kwa moyo wote, roho na tabia, ambayo imefia
nafsi na kuishi kwa ajili ya Kristo. Bwana wetu na Mwokozi wetu anatuhitaji
tujitoe Kwake.
Kusalimisha ubinafsi wetu kwa Mungu ndiyo yote anayohitaji,
kujtoa kwake kutumika kama apendavyoYeye. Ni
hadi tutakapofika katika hatua hii ya kujisalimisha, ndipo tutaweza kufanya
kazi kwa furaha, kwa faida na kwa mafanikio po pote pale. Mbele yangu leo
ninaona wale ambao Mungu anaweza kuwatumia kama
watamtegemea Yeye ….Ni heshima kumfuata Mwokozi. Na ni kwa kutii maagizo
aliyotoa kwamba utaandaliwa kwa ajili ya kukutana Naye pindi ajapo. Kama utamwomba Mungu akusaidie kushinda tabia isiyo ya
Kikristo katika mwenendo wako, atakuandaa kwa ajili ya kuingia mbinguni, mahali
ambapo dhambi haiwezi kuingia. Wale ambao kila siku wanatoa maisha yao kwa Kristo, na wale ambao wanatafuta kumjua,
watabarikiwa sana.
Sema hivi, Kristo alitoa maisha Yake kwa ajili yangu, nami lazima nitoe maisha
yangu Kwake. Kama utajitoa kikamilifu Kwake,
utakuwa mshindi katika vita dhidi ya dhambi. Bwana Yesu Kristo atakuwa msaada
kwako, atakuwa mdhamini kwako, nguvu zako kama
utampokea na kumtii Yeye. Katika kisa, lulu haitolewi kama zawadi.
Mfanyabiashara aliinunua kwa gharama ya vyote alivyokuwa navyo. Maswali mengi
juu ya hili, Kristo anaelezewa katika Maandiko kama zawadi. Yeye ni zawadi,
lakini kwa wale tu ambao wanajitoa wenyewe, nafsi, mwili na roho, mwili, kwake
bila kuzuia cho chote. Tunapaswa tujitoe wenyewe kwa Kristo, kuishi maisha ya
utii wa hiari kwa matakwa Yake yote. Vile vyote tulivyo, talanta zetu na uwezo
wetu tulio nao ni vya Bwana, kuwekwa wakfu kwa huduma Yake. Tutakapojitoa
kikamilifu Kwake, Kristo pamoja na hazina zote za mbinguni, hujitoa mwenyewe
kwetu. Nasi tunapata lulu ya thamani.
Maswali ya Kujitathmini:
Wewe ni wa
thamani sana mbele za macho ya Mungu kiasi kwamba alifanya yote kukufanya uwe wake. Hili hukufanya ujisikieje?
Fikiri juu ya kile ambacho Yesu alikupatia ili
mbingu iwe yako. Je inakstahili kujitoa Kwake kila siku? Je msingi kufanya?
0 comments:
Post a Comment