Subscribe:

Saturday, 1 March 2014

       MORNING STAR TELEVISHENI YAPATA KIBALI CHA KURUSHA MATANGAZO




Mkurugenzi wa Vyombo vya Habari wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania Mchungaji Musa Mika (pichani) kupitia radio ya Morning star ametangaza rasmi kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeipa Kanisa hiyo kibali cha kurusha matangazo ya Televisheni tarajiwa ya Morning Star.

Mchungaji Musa Mika pia amesema uzinduzi wa Morning Star Televisheni utafanyika hivi karibuni na wakati ukifika watatangaza king'amuzi kitachokuwa kinarusha matangazo ya kituo hicho kinachomilikiwa na Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania.

Mchungaji Mika pia alichukuwa fursa hiyo kwa kuwashukuru waumini wa kanisa hilo, wapenzi wa radio ya Morning Star na watanzania wote kwa ujumla kwa kuwa pamoja nao katika sala kwa muda mrefu wakati wakisubiri habari njema kama hii.

0 comments:

Post a Comment