Subscribe:

Tuesday, 18 March 2014

BAADHI YA MATUKIO YALIYOFANYWA NA WASHIRIKI WA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO MBEZI LUIS KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA DON BOSCO KIMARA SUKA SIKU YA MATENDO YA HURUMA TAREHE 15/3/2014.



 Hapo washiriki wa kanisa la Mbezi Luis wakisalimiana na Watoto wa kituo cha kulelea watoto
                     yatima kilichopo KIMARA SUKA jijini Dar es salaam.

       Godliver Chacha na Mrs Mganda wakizungumza machache juu ya Ukuu wa Mungu.

   Watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima Kimara Suka wakipata chakula cha Mchana.


     Baadhi ya Watoto wa Kanisa la Mbezi Luis na Malamba pamoja na watoto yatima
      wakishirikiana kuchukua chakula cha Mchana.

     Baadhi ya Watoto wa Kanisa la Mbezi Luis na Malamba pamoja na watoto yatima
      wakishirikiana kuchukua chakula cha Mchana.

  Watoto wa Kanisa la waadventista Mbezi luis na Malamba wakiwapatia zawadi watoto wenzao
                  wa kituo cha watoto yatima KIMARA SUKA jijini Dar es salaam.

 Watoto wa Kanisa la waadventista Mbezi luis na Malamba wakiwapatia zawadi watoto wenzao
                  wa kituo cha watoto yatima KIMARA SUKA jijini Dar es salaam.

  Zawadi mbalimbali zilizotolewa katika kituo cha kulelea watoto yatima KIMARA SUKA
                                                   jijini Dar es salaam.

            Kulwa Jackson na Happy wakipeleka zawadi kwenye kituo cha watoto yatima.


  Mchungaji Kyanzi akihojiwa na waandishi wa Habari Katika kituo cha kulelea watoto yatima Don Bosco.
                    Kwaya ya Vijana Mbezi luis wakimtukuza Mungu kwa njia ya Uimbaji.

Friday, 14 March 2014

           KUTENGA KUNDI LA MPIJI MAGOHE KUWA KANISA TAREHE 8/3/2014


Mchungaji: Joshua Kyanzi akizungumza jambo fulani kwa washiriki wa kanisa la MPIJI MAGOHE

Kwaya ya Mbezi Luis ikimtukuza Mungu kwa njia ya Uimbaji

Mchungaji:Tirumanywa akihutubia washiriki neno la Mungu

Katibu wa kanisa la Mbezi Luis:John Masuruli akizungumza jambo kwa Washiriki

Katikati ni Mchungaji:Tirumanywa akifanya jambo fulani 

Ni washiriki wa Kanisa la Waadventista wasabato Mpiji Magohe

Mafundi Mitambo: Charles Anton na George Gachu wakihakikisha usikivu unakuwepo.



Baadhi ya Washiriki wakipata chakula cha Mchana 

Kwaya ya Golani wakimtukuza Mungu kwa njia ya Uimbaji



Saturday, 1 March 2014

       MORNING STAR TELEVISHENI YAPATA KIBALI CHA KURUSHA MATANGAZO




Mkurugenzi wa Vyombo vya Habari wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania Mchungaji Musa Mika (pichani) kupitia radio ya Morning star ametangaza rasmi kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeipa Kanisa hiyo kibali cha kurusha matangazo ya Televisheni tarajiwa ya Morning Star.

Mchungaji Musa Mika pia amesema uzinduzi wa Morning Star Televisheni utafanyika hivi karibuni na wakati ukifika watatangaza king'amuzi kitachokuwa kinarusha matangazo ya kituo hicho kinachomilikiwa na Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania.

Mchungaji Mika pia alichukuwa fursa hiyo kwa kuwashukuru waumini wa kanisa hilo, wapenzi wa radio ya Morning Star na watanzania wote kwa ujumla kwa kuwa pamoja nao katika sala kwa muda mrefu wakati wakisubiri habari njema kama hii.
              PICHA ZA GARI LA MCHUNGAJI MICHAEL TWAKANIKI BAADA YA AJALI



                                           Gari la Mch Michael Twakaniki baada ya Ajali


Mch Michael Zacharia Twakaniki (katikati)akiwa hospitalini huko Dodoma kushoto mwenye tai ni Mhazini wa jimbo la Mashariki mwa Tanzania katika kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania Athanas Sigoma alipokuwaamemtembelea.


Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Dodoma Michael Zachariah Twakaniki alipata ajali Februari 25,2014 ya gari ambalo alikuwa akiliendesha akiwa na abiria wenzake 6,wawili wakiwa ni watoto wake,wajukuu wawili na rafiki zao wawili.
.
Ajali hiyo ilitokea eneo la Chamwino Dodoma,walipokuwa wakisafiri kuelekea Dodoma toka jijini Dar es salaam.

Ajali hiyo inaelezwa ilitokea baada ya kumkwepa mwendesha baiskeli na gari hilo kubiringita mara nne.