skip to main |
skip to sidebar
HABARI KWA KINA ZA HIVI PUNDE
1. Mwenyekiti- Mch. Magulilo John Mwakalonge-.
Ametenda kazi kama mwinjilisti mlei, Mchungaji wa Mtaa (SWTF- SHC).
Mkurugenzi wa Uwakili- ETC, Mkurugenzi wa Mawasiliano - Tanzania Union,
Mkurugenzi wa Huduma na Katibu wa Chama cha Wachungaji - Tanzania Unioni
na kisha akishika nyadhifa hizo hizo katika Divisheni yetu ya ECD.
Kabla ya wito huu alikuwa Mkurugenzi wa Vijana, Muziki, na Chaplensia wa
ECD.
2. Katibu Mkuu- Mch James Machage-
Ametenda Kazi Kama mchungaji wa mtaa, Mkurugenzi wa Chaplensia wa
Tanzania Union, Mwenyekiti wa Mara Konference Kwa miaka karibia 15 na
Katibu Mkuu wa Mara Konferensi. Wakati akiitwa Mch Machage alikuwa
Katibu Mwenza wa Tanzania Union.
3. Mhazini - Mr Jack Manongi-
Ametenda Kazi Kama Mhasibu Mkuu wa Tanzania Union kisha akijiunga na
kitengo cha huduma za Ukaguzi cha general Conference ambako ametenda
kazi kama mkaguzi wa hesabu za fedha mpaka wakati wa wito huu.
Tafadhali tuwaombee.
Tarehe 5-6 /12/ 2013 Wajumbe Kutoka makanisa yote ya Unioni Misheni ya
Tanzania Kusini watakutana Dar es salaam kuchagua wakurugenzi wa unioni
hii.
Tarehe 3-4/12/2013 Wajumbe toka Makanisa yote ya Unioni
Konferensi ya Tanzania Kaskazini watakutana Arusha kuchagua Viongozi na
Wakurugenzi wa Union hiyo. Tuendelee Kuombea zoezi hilo.
HAO NDIO VIONGOZI WAPYA WA UNION MISHENI YA TANZANIA KUSINI.
0 comments:
Post a Comment