Subscribe:

Thursday, 2 July 2015

Ni katika kambi la Vijana la Waadventista wasabato lililofanyika MBEYA-Chimala lililokuwa limeanza Tarehe 22/6/2015 na kuhitimishwa Tarehe 27/6/2015.Hayo ni baadhi ya matukio yaliyofanyika huko kwa vijana wa kanisa la waadventista wasabato Mbezi Luis.
Mungu azidi kuwaneemesha vijana katika kuyafanya yaliyo mapenzi yake.

 Ni vijana wa Watafuta njia wakiwa katika picha ya pamoja na Mwl Bernad Masatu




 Ni kijana John Mtengeti akiwa anapanda Mlima.

 Ni Mwl Kurwa Jackson akiwa anapanda Mlima taratibu.

 Ni vijana wa kanisa la waadventista wasabato Mbezi Luis wakiwa katika picha ya pamoja.


 Naam ni vijana wetu wakivuka mto.



 Ni kijana Mussa Bright katika huo mwonekano hapo.



Monday, 22 June 2015

MUNGU ANAZIDI KUWA NASI TUNAPOANZA MIKUTANO YETU HAPA ARUSHA

Ni katika kanisa la waadventista wasabato Arusha Mjini kati.Ndipo ambapo tumekusanyika hapa kwa ajili ya Mkutano wa TANZANIA ADVENTIST INTERNET NETWORK (TAIN).





 Mafundi mitambo wakiweka mambo sawa tayari kwa kuanza Mkutano wetu.


Mchungaji HARUNI KIKIWA akiwa anaongoza Uimbaji katika Mkutano wetu.


Pr/Dr. Godwin Lekundayo president wa NTUC akiendesha somo la asubuhi ya leo



Mtangazaji Maduhu akipewa Tuzo ya TAIN katika kuiwakilisha tasnia ya ICT.


Mtangazaji Maduhu akizungumza jambo fulani katika Mkutano wa TAIN.


Mr Haggai Abuto akiwa anapokea Tuzo ya TAIN 


Hao ni wanakamati kutoka South East Conference (SEC)


Mchungaji MUSSA MIKA akipokea Tuzo ya TAIN kwa kuutambua mchango wake.


Hao ndio wanatimu wote wa TAIN hapo ni baada ya kumaliza Mkutano.



Sunday, 14 June 2015

Ilikuwa ni tarehe 13/6/2015 katika kanisa la waadventista wasabato Mbezi Luis ambapo palifanyika SABATO YA WAGENI na mnenaji Mkuu alikuwa Mch ENOSI MWAKALINDILE ambaye ni Mkurugenzi katika Konferensi ya SEC jijini Dar es salaam.



        Kwaya ya Uinjilisti Mbezi Luis wakifanya huduma ya uimbaji.

   Kwaya ya vijana UVUVIO wakifanya huduma ya uimbaji.

Wabatizwa wakila kiapo cha kufanya maamuzi ya kumfuata Yesu katika maisha yao yote.

       Watu wakiwa wamefurika katika Ubatizo siku hiyo.


        Mch ENOSI MWAKALINDILE akifanya huduma ya Ubatizo siku hiyo.

    Kwaya ya kamati ya Efoti ya wiki mbili ambayo ilihitimishwa na sabato ya wageni siku hiyo.



    Wageni waalikwa walipata nafasi ya kupata zawadi siku hiyo ya sabato ya wageni.


 Mungu azidi kutubariki tunapojitolea kuifanya kazi yake kwa bidii zote.

Tuesday, 28 April 2015

ILIKUWA NI SIKU YA PEKEE SANA KATI YA JACKSON TRAYPHONE MLYATU NA SARAH GEORGE AMBAO SASA WAMEKUWA MWILI MMOJA:
Tukio hili lilifanyika mnamo Tarehe 26/4/2015 katika kanisa la waadventista wasabato mbezi luis jijini Dar es salaam.









Wednesday, 1 April 2015

Umewahi kusikia wakiimba??????
Ni Mbezi Luis UVUVIO s.d.a Choir.......
Hivi karibuni itawafikia kaa mkao wa kuipata na endelea kuwaombea......


Monday, 9 March 2015

NI WANA WA KIKE WA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO--MBEZI LUIS:

Ilikuwa ni siku njema sana ya tarehe 7/3/2015 katika kanisa la waadventista wasabato mbezi luis jijini Dar es salaam.Takribani miaka kumi sasa ndio mwana wa kike wa kwanza kusimama kuhubiri wakati wa ibada kuu.Mungu atuongoze kwa kila jambo.
 Mwenyekiti: Mama Mchungaji ANNA KYANZI



Kwaya ya wana wa kike wakiimba wakati wa ibada kuu

 Dr HAPPY RANGE :Mhubiri