Subscribe:

Friday, 9 January 2015

NI TUKIO LILILOFANYIKA JANA LA KUIGAWA KONFERENSI YA MASHARIKI MWA TANZANIA YA WAADVENTISTA WASABATO.





 

Tukio hilo ambalo lilikuwa ni kwa ajili ya kupanga konferensi mbili mpya litatanguliwa na kuvunjwa rasmi kwa konferensi ya mashariki ,zoezi lililo simamiwa na Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Kanda ya Afrika Mashariki na Kati Dr Nathaniel Walemba. 
                                          ======================
Konferensi zilizopangwa ni Konferensi ya Kusini Mashariki mwa Tanzania (SEC) na Konferensi ya Mashariki na Kati mwa Tanzania (ECT). Akiongea na Morning Star Radio hii leo Katibu Mkuu wa ETC Mchungaji Sadock Butoke amesema konferensi hiyo ina makanisa 305 ambalo ni ongezeko la asilimia 26 ukilinganisha na miaka mitatu iliyopita,mitaa 81,makundi 373 na jumla ya washiriki 67,928 Mchungaji Butoke ameyataka makanisa mahalia yote kuwa na makundi kwa uchache kila kanisa liwe na makundi yasiyopungua matatu.
                                           ======================

Viongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato kanda ya Afrika Mashariki na Kati baada ya kuvalishwa skafu picha nyingine ni mgeni Maalumu Dr. Brasiuos Ruguri akikagua gwaride la vijana kutoka Kanisa la Waadventista wa Sabato Tabata Kimanga.
WAFAHAMU VIONGOZI WA KONFERENCE MBILI MPYA:



Hatimaye Konferensi ya Mashariki  Kati mwa Tanzania katika kanisa la Waadventista Wa Sabato imepata viongozi wake ni hawa wafuatao;-

Mwenyekiti: Mchungaji Joseph Mngwabi
Katibu:Mchungaji Samwel Katengu
Mhazini:Athanas Sigoma
Mkurugenzi wa Huduma:Mchungaji Mshola
Vijana:Mchungaji Emmanul Sumwa
Elimu:Devota Shimbe
Afya na Familia:Dr.Josia Tayari
Mawasiliano:Mchungaji Christopher Ungani

Wafutao ni viongozi wa Konferensi mpya ya Kusini Mashariki mwa Tanzania katika kanisa la Waadventista Wa Sabato ambao ni;-

Mwenyekiti: Mch. Mark Walwa Malekana
Katibu:Hebert Nziku
Mhazini:Yusuph Zege
Mkurugenzi wa Huduma:Mch Toto Kusaga
Vijana:Wilfred Mafwimbo
Elimu na Mawasiliano:Abrahamu Youze
Afya na Familia:Mwaibasa Whatson
Huduma za wanawake:Bernais Luuha

Tuesday, 30 December 2014

 MKUTANO WA VIJANA BARATONI UMEKWISHA...

Zifuatazo ni picha za siku maalum vijana hawa wakiimba wimbo wa Mkutano ukiwa na Moto "TURNING CITIES UPSIDE DOWN"














Wednesday, 24 December 2014

MKUTANO WA VIJANA WA BARATON-KENYA UMEANZA RASMI HAPO JANA NA LEO IKIWA NI SIKU YA PILI

 







 

Friday, 21 November 2014

"PANGA KUMFANYIA MUNGU KAZI KWA KUMJENGEA HEKALU TAKATIFU"



Monday, 3 November 2014

YALIYOKUWA YAMEJIRI KATIKA SABATO YA WAGENI MBEZI LUIS S.D.A CHURCH:

Tunamshukuru Mungu kwa uweza wake wa pekee kwa kuweza kuhitimisha siku hii ya wageni ambayo ilifuatiwa na Effort ya Nyumba kwa Nyumba takribani wiki 2 na kuweza kuhitimishwa kwa siku hii ya SABATO ya WAGENI tarehe 1/11/2014.
Bwana awabariki wote walioweza kufanikisha shughuli hii.

       Tayari kwa IBADA KUU ndani ya Kanisa la Waadventista wasabato Mbezi Luis.


Kijana wa Mungu Chediel Rusanyu akiwa anatoa Neno wakati wa Ibada

  Mwinjilisti Zephania akinena na watumishi wa Mungu katika Ibada kuu.

        Washiriki wakiwa katika Ibada ndani ya Kanisa.

 Watoto nao hawakukosa katika tukio hili la Sabato ya Wageni huku wakimsifu Mungu.

 Kwaya ya Uinjilisti Mbezi Luis wakiwa wanatoa huduma ya Nyimbo wakati wa Ibada kuu.

Watu waliokuwa wamejitoa tayari kwa Ubatizo wakati wa mahubiri.


Watumishi wa Mungu wakiwa wanajipanga kufanya jambo fulani.

 Hafla ilifana huku washiriki wakilishwa KEKI na kiongozi wa Shule ya Sabato Bi Grace Mgeni.


Ni wawakilishi wa WAGENI walioweza kuwawakilisha wenzao katika tukio la kukata KEKI.

Monday, 13 October 2014

SEMINA KWA WAJUMBE WA BARAZA LA KANISA TOKA MSTV NA MCHANGANUO WA HITAJI LA MILION 225.


MR.MATHIAS MAVANZA MHAZINI WA TANZANIA ADVENTIST MEDIA CENTER SIKU YA SABATO YA TAREHE 11 OCTOBA,2014 KANISANI MWENGE SDA AMEELEZA HATUA NA MCHAKATO WA UFANIKISHAJI WA KURUSHWA KWA MATANGAZO YA MSTV NA AKITO MSISITO KWA WAJUMBE KUCHUKUA KADI MAALUM ZA KUCHANGIA KWA MPANGO AMBAPO MDAU HUYU ATAPA TAARIFA NA HABARI TOKA MSTV NA ATAKUWA AMESAIDIA UINJILISTI KUFIKIA WATU WENGI KWA NJIA YA RUNINGA HII.

Tangu kuanza kwa mradi mzima wa runinga ya Morning Star Televisheni ambayo ilikuwa ametengewa kiasi cha milioni 500 gharama ambayo ingejumuisha yafuatayo;

Matengenezo ya Studio ya televisheni
Ununuzi wa vifaa na mitambo.
Malipo ya lesseni ya kurushia matangazo kutoka kwa mamlaka ya serikali.
Uendeshaji wa televisheni kwa miezi 6,hii ni pamoja na kulipia gharama ya kurusha matangazo kupitia kwa wenye ving'amuzi.
Kununua vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya kurekodi vipindi na kurusha matangazo hewani ambavyo ni vya kisasa tena vinavyokwenda na wakati.
Kutengeza studio ya kisasa ambayo itatumika kwa ajili ya kutayarishia vipindi mbalimbali.
Baada ya kupata vifaa na kupata studio,matangazo ni lazima yarushwe hewani,na yafuatayo ni mahitaji kwa ajili ya kurushwa matangazo kwa miezi mingine 6.
Btl(urushwaji wa matangazo
AGAPE FEES(urushaji wa matangazo)
TCRA FEES(malipo kwa serikali)
Agape deposit(kama dhamana ya mkataba)
(vifaa vya matangazo)
(gari kwa ajili ya uzalishaji).