Tukio hilo ambalo lilikuwa ni kwa ajili ya kupanga konferensi mbili mpya litatanguliwa na kuvunjwa rasmi kwa konferensi ya mashariki ,zoezi lililo simamiwa na Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Kanda ya Afrika Mashariki na Kati Dr Nathaniel Walemba.
======================
Konferensi zilizopangwa ni Konferensi ya Kusini Mashariki mwa Tanzania (SEC) na Konferensi ya Mashariki na Kati mwa Tanzania (ECT). Akiongea na Morning Star Radio hii leo Katibu Mkuu wa ETC Mchungaji Sadock Butoke amesema konferensi hiyo ina makanisa 305 ambalo ni ongezeko la asilimia 26 ukilinganisha na miaka mitatu iliyopita,mitaa 81,makundi 373 na jumla ya washiriki 67,928 Mchungaji Butoke ameyataka makanisa mahalia yote kuwa na makundi kwa uchache kila kanisa liwe na makundi yasiyopungua matatu.
======================
Viongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato kanda ya Afrika Mashariki
na Kati baada ya kuvalishwa skafu picha nyingine ni mgeni Maalumu Dr.
Brasiuos Ruguri akikagua gwaride la vijana kutoka Kanisa la Waadventista
wa Sabato Tabata Kimanga.