Subscribe:

Monday, 13 October 2014

SEMINA KWA WAJUMBE WA BARAZA LA KANISA TOKA MSTV NA MCHANGANUO WA HITAJI LA MILION 225.


MR.MATHIAS MAVANZA MHAZINI WA TANZANIA ADVENTIST MEDIA CENTER SIKU YA SABATO YA TAREHE 11 OCTOBA,2014 KANISANI MWENGE SDA AMEELEZA HATUA NA MCHAKATO WA UFANIKISHAJI WA KURUSHWA KWA MATANGAZO YA MSTV NA AKITO MSISITO KWA WAJUMBE KUCHUKUA KADI MAALUM ZA KUCHANGIA KWA MPANGO AMBAPO MDAU HUYU ATAPA TAARIFA NA HABARI TOKA MSTV NA ATAKUWA AMESAIDIA UINJILISTI KUFIKIA WATU WENGI KWA NJIA YA RUNINGA HII.

Tangu kuanza kwa mradi mzima wa runinga ya Morning Star Televisheni ambayo ilikuwa ametengewa kiasi cha milioni 500 gharama ambayo ingejumuisha yafuatayo;

Matengenezo ya Studio ya televisheni
Ununuzi wa vifaa na mitambo.
Malipo ya lesseni ya kurushia matangazo kutoka kwa mamlaka ya serikali.
Uendeshaji wa televisheni kwa miezi 6,hii ni pamoja na kulipia gharama ya kurusha matangazo kupitia kwa wenye ving'amuzi.
Kununua vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya kurekodi vipindi na kurusha matangazo hewani ambavyo ni vya kisasa tena vinavyokwenda na wakati.
Kutengeza studio ya kisasa ambayo itatumika kwa ajili ya kutayarishia vipindi mbalimbali.
Baada ya kupata vifaa na kupata studio,matangazo ni lazima yarushwe hewani,na yafuatayo ni mahitaji kwa ajili ya kurushwa matangazo kwa miezi mingine 6.
Btl(urushwaji wa matangazo
AGAPE FEES(urushaji wa matangazo)
TCRA FEES(malipo kwa serikali)
Agape deposit(kama dhamana ya mkataba)
(vifaa vya matangazo)
(gari kwa ajili ya uzalishaji).

Saturday, 30 August 2014

MAKAMBI YA MTAA WA MBEZI YALIVYOFANA NA ROHO ZA WATU 42 ZIKIMKIRI YESU KUWA BWANA WA MAISHA YAO YOTE KWA NJIA YA UBATIZO:30/8/2014


                                                             Wakati Ibada kuu ikiendelea.
                                           Mchungaji Mganga akifanya Huduma ya Ubatizo.
                          Watoto nao hawakuwa mbali katika Kubarikiwa na Neno la Mungu.

                                    Kwaya ya Waadventista wasabato Mbezi Luis Uinjilisti
                                          Kwaya ya Waadventista wasabato Malamba mawili

                                               Kwaya ya UFUFUO Mbezi Luis{Vijana}

Tuesday, 26 August 2014

PANGA KUWEPO ILI UBARIKIWE NA NENO LA MUMGU:


Wednesday, 20 August 2014

 SEMINA YA VIJANA KANISA LA WAADVENTISTA MBEZI LUIS TAREHE 17/8/2014.



 semina ya vijana iliyofanyika kanisani Mbz Luis tar 17 08 2014 saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni.

Friday, 15 August 2014

JE, UNAVIFAHAMU VITU ALIVYOVITUMIA NABII MAMA ELLEN G WHITE?

 Hivi ni baadhi ya vifaa alivyotumia mama Ellen G. White, mwanamke anayeaminiwa na kanisa la waadventista wasabato kama nabii wa Mungu...vifaa vilivyobaki kama makumbusho katika nyumba aliyopata kuishi huko nchini Marekani.
Endelea kufuatana nasi ili ujifunze kitu.

Kibao kinachoonesha nyumba aliyoishi Mama Ellen na Mume wake James White mwaka 1856-1863 

                                                           Nyumba waliyoishi wawili hao

                                        Kitanda alichokuwa analalia Enzi za Uhai wake.

 Meza na Kiti alichokuwa akitumia wakati akiandika Njozi mbalimbali alizokuwa akipokea

                                             Kalamu na Taa aliyokuwa akitumia kuandika.

Meza na Taa yake

Saturday, 9 August 2014

MCHUNGAJI DR BLASIUS RUGURI AFIKA MWANZA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI WA JENGO LA KIRUMBA SDA CHURCH.

 Dr. Ruguri akihutubia washiriki katika kambi la Kirumba Mwanza mara baada ya kuweka jiwe la msingi

 Kutoka kushoto ni Ndugu Mayani mhazini wa konferensi ya nyanza kusini, Ndugu Gideon Msambwa mkurugenzi wa idara ya mawasiliano union konferensi ya kaskazini wa Tanzania na Ndugu Eliamini Kisimbo mhazini wa Shule ya Sekondari ya Nyanza iliyopo jijijni Mwanza wakiimba wimbo katika ibada ya Kambi la mtaa wa kirumba mara baada ya Dr. Blasious Ruguri kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo jipya la kanisa la Kirumba

 Dr. Blasious Ruguri akifungua jiwe la msingi wa jengo la kanisa la kirumba Mwanza

 Dr. Ruguri (wapili toka kushoto waliovaa kofia) akionyeshwa ramani ya jengo ya jipya la kanisa la Kirumba

MAKAMBI 2014 - HATIMAYE BWANA KAJITWALIA ROHO ZA WATU KWA NJIA YA UBATIZO HUKO MOROGORO.

 Kupitia mikutano ya makambi inayoendelea sehemu mbalimbali, hatimaye watu wengi wameendelea kumpokea Yesu kama BWANA na Mwokozi wao kwa njia ya ubatizo baada ya watu wapatao 32 kubatizwa katika mitaa miwili iliyopo mkoani Morogoro yaani mtaa wa Misufini na Kihonda.
Wakati mtaa wa Misufini chini ya Mch. D. Mmbaga na kwaya ya Ubungo Hill ukibatiza watu wapatao saba (7), mtaa wa Kihonda chini ya Mch. S. Singo na kwaya ya Yombo Dovya ulibatiza watu Ishirini na tano (25).
Makambi yote haya yanategemewa kuhitimishwa Jumamosi ya tarehe 09/08/2014 kwa sherehe kubwa.

                                            Mch. Mndambi akiendelea na huduma ya ubatizo.

                                      Mch. Mndambi akiendelea na huduma ya ubatizo
 Mch. Mndambi akiendelea na huduma ya ubatizo na watu wakishuhudia.

 Wanafamilia wakifurahia matendo makuu ya Mungu baada ya mmoja wa familia yao kupokea Yesu kwa njia ya ubatizo