Subscribe:

Wednesday, 8 June 2016

AINA ZA MAWASILIANO:
MNENAJI: MCH RICHARD KANIKI

 Mkutano unaoendelea katika kanisa la Dodoma Sda na ikiwa ni siku ya tatu tangu kuanza rasmi kwa mkutano huu wa mawasiliano na habari. Leo ibada ya ufunguzi imeletwa na Mchungaji Kaniki ambaye alifafanua aina za mawasiliano ambazo.


NJIA ZA MAWASILIANO NI:

 1. Maandishi

Hapa ni machapisho mbalimbali ambapo alisisitiza kuwa njia ya maandishi ndio ilisaidia kuipeleka injili mbele kwenye kipindi kama cha nabii Mama White watu walitoa machapisho yake mbalimbaliambayo pia yalisaidia injili kwenda mbele.
2. Mawasiliano kwa njia ya mdomo
mwanzo 1:28-20
- Mawasiliano haya yanamuhm sana kwa wanandoa na kwa nyanja nyingine ya watumiaji wa mawasiliano.
1Petro3:7
3.Mawasiliano ya kimya
 - Muonekano wa sura yake na vitendo vyake zinaashiria ujumbe au taarifa fulani juu jambo fulani.

Mwanzo 4:5-6
Dalili za mawasiliano ya mdomo
1. Usikilizaji
2 Mzungumzaji
3.Utawala wa mazungumzo.


Tuesday, 7 June 2016

FUNDI MWINJILISTI:
MNENAJI: HAGGAI ABUTO



Mr. Haggai Abuto(aliye vaa Koti) ambaye ni Chief Information Officer wa EDC katika kipindi cha "FUNDI MUINJILISTI"

 Amesisitiza kuwa hiki ni kipindi cha Millennia Hivyo Wazee na Vijana washirikiane katika magroup mbalimbali ya mitandao ya Kijamii ili kuleana na kuinjilisha habari njema za wokovu.

Mtafsiri ni Mr. Mazara Edward Matucha ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SHC
MAADILI YA MWANA MAWASILIANO:

MNENAJI: MCH STEVEN BINA



Mchungaji Steven Bina, Mkurugenzi wa Mawasiliano Mstaafu - ECD Amefundisha Maadili 10 ya Mawasiliano kwa kanisani la waadventista wa Sabato. Amesema hayo hii leo katika mkutano wa TAiN Dodoma katika kipindi kilicho isha sasa hivi. 
  1. Hakikisha Kila unacho wasiliana kiwe kinamtukuza Mungu
2. Hakikisha Unatoa Ujumbe wa Upendo wa Matumaini wa Marejeo ya Yesu
3.Hakikisha unazingatia ethos (desturi) , beliefs(Imani) , na Values(mambo tunayo yadhamini)
4. Hakikisha uko tayari kushirikiana, kuunga Mkono vyombo vya habari, Ungamkono Ujumbe, heshimiana na wanahabari. Kwani huu ni wajibu wa Mwana Mawasiliano.
5 . Hakikisha una uhuru wa kuwasiliana kwa uadilifu, uwazi, ukiwa na kusudi, mwaminifu, makini, diversity and excellence.
6. Hakikisha unazingatia ukweli na Uaminifu.
7. Hakikisha nyumba zetu za Habari zielekeze juu ukweli unaotakiwa na kuhuisha wasikilizaji.
8. Kila mwana Mawasiliano ahakikishe anajiendeleza na kupanua uelewa wako.
9. Hakikisha Mawasiliano yako hayana mgongano wa masihara na upendeleo wakirafiki na kindugu.
10. Hakikisha shughuli zote za Mawasiliano zinazingatia Utambulisho wa kanisa.
USALAMA WA MTANDAO:

MNENAJI: MCH MUSSA MIKA





ULINZI WA VITU VITATU: 
1.Faragha-Kwamba inatumiwa na wale tu wenye idhini ya kuitumia. 
2. Uadilifu-kulinda usahihi wake, ukamilifu wake, na michakato yako. 
3. Upatikanaji wake - Kwamba wote wenye idhini ya kuipata wanaipata kwa ukamilifu wake.
Pastor Musa Mika ameeleza hasara zipatikananzo kwa kukiuka

 ULINZI UKIKIUKWA: 
1.Heshima au hadhi inaweza kupotea. 
2. Hasara ya kifedha yaweza kutokea. 
3. Kupoteza haki za Ubunifu. 
4. Yawezekana kukabiliwa na hatua za kisheria. 
5. Kupoteza wateja. 
6. Kuingiliwa kibiashara 

HOTUBA YA ASUBUHI KATIKA MIKUTANO YA WANAMAWASILIANO: 07/06/2016



 
Mr. Atanus Sigoma Mhazini wa ECT akitoa Somo la asubuhi ya leo katika Mikutano ya TAiN inayo endelea hapa Dodoma .
Pamoja na mengi aliyo yasisitiza yafuatayo ni baadhi:

1. Huu ni wakati Wakwenda na Technology ili kwenda na kasi kubwa katika kuinjilisha Dunia.
2. Ulimwengu wa sasa Makarani wa Kanisa wanahitaji Kujua Kompyuta kwa matumizi ya utunzaji wa kumbukumbu za kanisa
3. Akionesha kuwa kuto endana na technology ni hasara akifafanua hili alisema Watu wengi wameshindwa kuendelea na Kazi au kupata kazi kwasababu ya kukosa ujuzi huu.
4. Akisisitiza swala la kwenda na technology alitahadharisha Waumini katika Matumizi sahihi ya technology nakwamba Mungu yuko juu ya technology kwani yeye ndiye Technology yenyewe.
5. Akisisitiza matumizi sahihi ya Mitandao alisema nimuhimu kujua Kuna mema na Mabaya hivyo tuchunge sana Macho yetu. Zaburi 119:37"Unigeuze Macho yangu nisitazame visivyofaa, Unihuishe katika njia yako."

Monday, 6 June 2016

MKUTANO WA WANAMAWASILIANO TAiN -DODOMA:

 UFUNGUZI: ANGELA KAIRUKI -Waziri ndiye ambaye amefungua Mkutano wa Wanamawasaliano Mjini Dodoma. 06/06/2016
 




 Waziri huyu akijibu Ombi la kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania juu ya Ombi la Kupewa siku Mbadala ya Usafi kwani Jumamosi ni siku ya ibada kwa Kanisa hili Waziri alisema Serikali itahakikisha uhuru wa kuabudu kwa madhehebu yote na lamuhimu katika siku hii ni usafi hivyo kwasababu jumamosi mko kanisani basi Waumini wahakikishe Jumamosi mazingira yao yote yanakuwa safi kabla ya sabato kama kawaida ya Waadventista WA sabato huandaa sabato mapema.

Waziri ametoa Rai kwa Wana TAiN na Kanisa la Waadventista kwa ujumla kuzingatia Maadili ya Matumizi sahihi ya mitandao mbalimbali ya habari kulingana na Sheria ya mtandao na habari.
Mikutano hii iliyo anza jana tarehe 05/06/2016 itaendelea hadi jumamosi ya tarehe 11/06/2016.
 





Sunday, 29 May 2016

HITIMISHO LA MIKUTANO YA INJILI HUKO RWANDA -GISENYI NA CONGO:

        "Maneno yaliyosemwa na Mch Ted Wilson baada ya kuhitimisha mikutano hii"


“Ni furaha iliyoje kubatizwa katika sehemu ya Kanisa la Mungu.Nguvu ya watu binafsi ilitumika ya kuhubiri Neno la Mungu na kufanya wito kwa kuleta watu wengine kwa Kristo. Watu hao walijiunga na kuweza kuendelea na madarasa ya kujifunza Biblia. Katika baadhi ya matukio , watakuwa wakipangwa katika makanisa mapya ya watu waliobatizwa hivi karibuni kuendelea kufanya kazi ya uinjilisti kwa bidii.Mungu atusimamie katika kuifanya kazi yake.”