Subscribe:

Wednesday, 23 March 2016

KUAGA MWILI WA MAREHEMU MCH KAJULA KANISA LA MWENGE S.D.A 23/3/2016

 Pr Godwin Lekundayo mkiti wa NTUC ndiye anayeongoza ibada ya mazishi ktk kanisa la Mwenge. Kabla ya kuanza hubiri walioimba ni kwaya ya wachungaji wote na wake zao.

KUZALIWA KWAKE Mchungaji Joshua Kamenya Kajula alizaliwa tarehe 28 Disemba 1939; huko Maeneo ya Majengo wilaya ya Mbeya Mjini katika Mkoa wa Mbeya. Yeye ni mtoto wa Pili kuzaliwa kati ya watano kwa mama yake. Baba yake alikuwa na wake wawili. Kwa upande wa mama yake ambaye ndiye alikuwa mke wa ndoa kwa baba walizaliwa wanaume watano. Alikuwa na ndugu wengine wawili waliozaliwa na baba yake kwa mke mwingine ambaye alirithiwa na baba yake baada ya kufiwa na kaka yake. Hivyo, kwa ujumla anatoka katika familia ya watoto saba kwa baba na kwa mama watano. ELIMU YAKE Marehemu mchungaji Kajula alipata elimu yake ya awali katika Shule ya kati (Middle School) huko Iganzo. Alisoma hapo mpaka darasa la sita mwaka 1955. Hatimaye alipelekwa Suji Upper Primary darasa la Saba na la Nane. Aliendelea na masomo yake katika kiwango cha darasa la tisa na la kumi (Standard 9 and 10). Ni sawa na kusema form two kwa lugha ya leo. Hatimaye alijiunga na chuo cha Ualimu huko Ikizu, mkoani Mara. Alisoma Diploma ya ualimu kwa miaka miwili hatimaye kwenda kuajiriwa mwaka 1962. Wakati huo aliamua kujiendeleza na elimu ya kidato cha nne bado akiwa kazini kwa kusoma kwa njia ya binafsi (private). Alifanya kazi kuanzia mwaka 1962 kwa miaka miwili hatimaye akaenda kuchukua kozi ya miaka miwili ya Elimu ya Afya (Health Education) huko Hospitali ya Heri, mkoani Kigoma. Huo ulikuwa ni mwaka 1964 hadi 1966.Hatimaye ndipo alipoenda kuchukua mafunzo ya kichungaji mwaka 1967 hadi 1968 huko Bugema, Uganda. Alipata diploma ya uchungaji. Safari yake ya elimu iliendelea mwaka 1985 hadi 1988 alipenda India katika chuo cha Poona Spicer Memorial College kwa masomo ya digrii yake ya kwanza. Na akahamia huko Ufilipino kwa masomo yake ya digrii ya pili. Alianza mwaka 1989 hadi 1991. Na kurejea Nyumbani. KUAMINI KWAKE Marehemu mchungaji alipata imani kupitia kwa mzungu mmoja aliyekuja kufanya kazi huko Misheni ya Iganzo. Mchungaji Kajula alikuwa akifanya kazi kwake ya house boy. Ndipo akawa mtu wa kwanza kupata imani katika familia yao. Tunaweza kusema kuamini kwake ndio chanzo na mlango wa kuwafanya ndugu zake wote watano kujiunga na kanisa hili la Waadventista WaSabato. Hatimaye mama yake alikuja kuamini baadaye kabisa. Mchungaji Joshua Kajula alibatizwa mwaka 1952. Mchungaji aliyembatiza ni Mchungaji Jacques aliyekuwa mmishonari huko Mbeya. MAISHA YA NDOA Marehemu mchungaji Joshua Kajula alifunga pingu za maisha tarehe 12 Septemba 1964 na Merry Justine Kimera (ni mtoto wa mchungaji Justine Salimu Kimera). Ndoa hii ilifungwa na Mchungaji Rufoko aliyekuwa ni mwenyeji wa Rwanda huko Heri Hospital ambako mchungaji Kajula alikwenda kuchukua masomo ya elimu ya afya. Mungu ameibariki familia hii kuwa na watoto watatu. Wa kwanza Gloria, wa pili ni Enidi, na watatu ni Suzzana. Na kuwa na wajukuu watano. KAZI YA UTUMISHI NDANI YA KANISA Marehemu mchungaji Kajula alianza rasmi kazi ya utumishi ndani ya kanisa kama mwalimu huko Masoko, Rungwe Historia Ya Maisha Ya Marehemu mkoani Mbeya. Alianza kufundisha shule hiyo ya kanisa mwaka 1962. Hatimaye alihamishiwa katika Shule ya msingi Iganzo mwaka huo mwishoni. Alifanya kwa awamu mbili ya mwaka 1962 hadi 1964. Akaenda Heri Hospital na aliporudi mwaka 1966 alirudi tena Iganzo kama mwalimu. Wito wa kichungaji: Marehemu mchungaji Kajula alikuwa na wito huo kwa muda mrefu ndipo alipopelekwa kusomea uchungaji katika chuo cha Bugema. Aliporudi alipangwa kuwa mchungaji wa Morogoro kuanzia 1969 hadi 1971. Lindi mwaka 1972 – 1973. Songea mwaka 1973 kwa miezi sita tu. Hatimaye alirudi Lindi tena mwaka 1973 mwishoni mpaka 1975. KUWEKEWA MIKONO: Marehemu mchungaji Kajula aliwekewa mikono ya kichungaji Novemba 1974. Hii ni ngazi ya mwisho ya kichungaji kama uthibitisho wa kudumu wa kutumika katika utumishi huo. Aliitwa kuwa mchungaji wa Zanzibar mwaka 1975 kwa wiki moja. Alienda kuripoti tu hatimaye akaambiwa abaki Dar-es-Salaam kuwa mchungaji wa Magomeni mwaka 1975 hadi 1977. Mwaka 1978 hadi 1985 aliitwa kuwa Mkurugenzi wa Lay Activities (Idara ya Huduma za Washiriki) wakati huo ikiwa pamoja na vijana, Dorkas, AMO na nyinginezo. Hatimaye ndipo alipokwenda masomoni huko India na Ufilipino. Mwaka 1991 Disemba alirudi masomoni. Na Januari 1992 alipangwa kuwa mwalimu wa chuo cha TASC (Tanzania Adventist Seminary College) kwa miezi sita tu. Mwaka huo huo alipelekwa kuwa Mwenyekiti wa Mara Conference kuanzia 1992 hadi 1996. Hatimaye aliitwa huko Tanzania Union Mission, Arusha makao makuu mwaka 1996 kama mkurugenzi wa idara ya Uchapaji na maeneo mapya ambapo alifanya kazi hiyo mpaka Januari mwaka 2000. Alipelekwa katika Field ya South West Tanzania kuwa mwenyekiti wake kuanzia 2000 mpaka 2005. Mwaka 2005 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Union hiyo ya zamani (Tanzania Union Mission) mwaka 2005 mpaka 2010. Ndipo alipostaafu kazi ya utumishi ndani ya kanisa Novemba 2010. JAMBO ATAKALOKUMBUKWA KATIKA UTUMISHI Marehemu mchungaji Joshua Kajula atakumbukwa kwa mambo mengi ambayo ameyafanya wakati alipokuwa akitumika ndani ya kanisa kwa moyo wake wote. Aliishi maisha ya kawaida na kiwango cha chini kwa ajili ya kuwafikia waumini wote. Hakuwa na ubaguzi wa kikabila wa kitabaka. Aliheshimika na watu wote. Ndio maana hata alipokuwa anakaribia kustaafu rasmi 2006; bado kanisa likaona ni vyema aendelee kulitumikia kwa muda wa ziada ya miaka mingine mitano ambayo ilikuwa tayari ni nje ya miaka ya kustaafu. Kanisa litamkumbuka sana kwa unyenyekevu wake na upole wake na pia swala la kuzielewa taratibu za kanisa na kuzisimamia vyema. Jambo la pekee sana ni pale alipokuwa anapenda kusali kwenye makanisa madogo madogo na makundi ya kanisa. Ni jambo ambalo ni nadra sana kwa viongozi wa ngazi kama yake kutenda hivyo kwa sababu ya majukumu mazito waliyonayo. Ndugu na jamaa nao wanamkumbuka kama kaka yao ambaye alikuwa na upendo wa dhati kwa ndugu wote. Mtiifu kwa wazazi. Mlezi mwema kwa wazazi wake. Mdogo wake Steven Kajula anasema “Kaka alifanya mambo ambayo kwa tamaduni na desturi za wanaume wa Kinyakyusa hawafanyi.” Alikuwa mfano wa kuigwa kama Mkristo kwa familia yake na kwa jamii alimoishi. Alikuwa mcheshi anayechangamana na watu. Anakumbukwa pia kama mtu aliyekuwa na hobby ya kuendesha gari. Pamoja na umri mkubwa alikuwa na uwezo wa kuendesha gari kutoka Dar-es-Salaam hadi Mbeya bila kuchoka katika uzee wake huu. Pia alikuwa mtu anayejali sheria za barabarani kwani mpaka anafariki hajawahi kupata ajali kwa maisha yake yote. Alikuwa makini sana barabarani. Ni jambo la kujifunza kwetu sote. MAJUKUMU MENGINE BAADA YA KUSTAAFU KWAKE Marehemu mchungaji Kajula alijishughulisha na shughuli zake ndogo ndogo kwani hakupenda kukaa tu nyumbani bila kazi. Alifanya shughuli ndogo ndogo kama mtu ambaye amezoea kufanya kazi muda wote. Lakini bado kanisa lake alilokuwa anasali, alianza kusali bado likiwa kundi tu hatimaye likapangwa kuwa kanisa. Alifanya ushirika na kanisa la Kunduchi tarehe 6 Mei 2012. Na kuanzia mwaka 2013 mpaka mauti inapomkuta alikuwa na majukumu ya uzee wa kanisa, kiongozi wa uhuru wa Dini, na pia kwa hekima yake alichaguliwa awe mshauri wa wazee wa kanisa akishirikiana na mchungaji wa mtaa. Alifanya kazi hiyo huku akionyesha utii wa kuhudhuria semina mbalimbali zilizoitwa na viongozi wa juu bila kujali aliwahi kuwa kiongozi mkubwa wa kanisa katika ngazi ya Union. Na huku akiunga mipango mikutano yote iliyopangwa na ngazi za juu kwa kusimamia vyema katika utekelezaji wa kanisa lake mahalia. MATATIZO YA KIAFYA NA KIFO CHAKE Marehemu mchungaji Joshua Kajula alianza kuugua mwishoni mwa utumishiwake ugonjwa wa kisukari. Lakini aliweza kupata tiba miaka michache akapona kwani sukari yake ilirudi katika hali ya kawaida kutokana na matibabu aliyoyapata kutoka sehemu mbalimbali. Mnamo mwaka jana alianza kupata tatizo la joto la mwili kupanda juu sana bila kushuka. Ndipo alipolazwa katika hospital ya Rabinisinia iliyoko maeneo ya Tegeta mwezi wa Disemba tarehe 24 hadi 25. Baadaye iligundulika kuwa ilikuwa ni malaria iliyosababisha joto kupanda sana. Alitibiwa malaria na Alitoka akawa na udhaifu wa miguu ikawa imepoteza nguvu ya kutembea. Hatimaye alianza kupata nafuu ya miguu. Lakini ghaflatena mwezi machi mwanzoni joto la mwili likapanda tena. Alipelekwa Rabinisia ambako alipimwa. Alilazwa kwa siku moja,aliporuhusiwa alirudi nyumbani. Usiku huo huo hali yake ilibadilika na ndipo alipopelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi. Siku ya jumatatu alipelekwa Muhimbili akapokelewa kama mgonjwa wa dharura (emergency patient) na kupelekwa wodini siku ya jumanne mpaka alhamisi. Na hali yake ikazidi kuwa mbaya ndipo alipoingizwa Chumba maalumu (ICU) siku ya Alhamisi jioni ambako alikaa mpaka Jumamosi Jioni alipofariki hakutoka tena hapo. Hivyo marehemu mchungaji Joshua Kamenya Kajula alifariki tarehe 19 MACHI 2016 SAA MOJA USIKU. Hapo ndipo ulipokuwa mwisho wa maisha ya Mtumishi wa Mungu Mchungaji Joshua Kamenya Kajula

Copy the BEST Traders and Make Money : http://ow.ly/KNICZ

 Pr Godwin Lekundayo mkiti wa NTUC

kwaya ya wachungaji wote na wake zao wakiimba 

Saturday, 19 March 2016

SIKU YA MATENDO YA HURUMA 19/03/2016 

Mungu wetu ni mwema sana.Kanisa la Waadventista Wasabato Mbezi luisjijini Dar es salaam nchini Tanzania.Walijielekeza kwenda kufanya Matendo ya Huruma katika maeneo yafuatayo:
1.Gereza la Mkuza
2.Hospitali ya Tumbi-Kibaha
3.Kituo cha kulea watoto yatima -Donbosco Kimara Suka.

Matukio ya picha hapo chini ni washiriki ambao walijielekeza katika kituo cha kulea Watoto yatima cha DONBOSCO KIMARA SUKA .Tulifarijika sana kuwatembelea watoto hawa na tulizidi kuuona mkono wa Mungu.
Tuliweza kuwapatia fedha taslimu Tsh 100,000/= 
1.Mafuta ya kupikia Ndoo ndogo 2 za lita 10.
2.Mafuta ya kupaka makubwa na madogo.
3.Sabuni za kufulia na za kuogea. nk

Mungu wetu atusaidie kuyatenda yanayompendeza kwa watu wote.

      Safari ikaanza tukiongozwa na Roho wa Mungu.

      Washiriki wakiimba wimbo katika ufunguzi wa Ibada.

     Mwinjilisti Mashota,Mzee Nyinyimbe na Mchungaji Mapima

         Usikivu makini wakati wa Ibada ikiendelea.

      Huyo ni Mlezi wa kituo cha Docbosco Kimara Suka

        Mwinjilisti MASHOTA akitoa Neno la Mungu

   Vijana wakiwapatia wenzao zawadi walizokuwa wamewabebea

Picha ya pamoja baada ya kumaliza Ibada 

KATIKA HOSPITALI YA TUMBI KIBAHA ILIKUWA HIVI

 Viongozi wa kanisa la SDA Mbezi Luis Pr Kyanzi, mzee wa kanisa Zawadi Mungereza, viongozi wa vijana Ngoda na Kulwa Jackson wakiongea na viongozi wa Zamu wa Hospitali wakibadilishana mawazo na kupeana mikakati ya kuboresha huduma kwa wagonjwa. Hatimaye mchungaji aliwaombea ili wafanye kazi kwa moyo na Mungu awabariki kwa utumishi mwema. Ni katika sabato ya matendo ya huduma, Jumamosi ya Leo.

Saturday, 16 January 2016

SIKU YA – 10: 

                      KRISTO AKIAKISIWA KWA MAJIRANI:

"Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi." Matendo 1:8

Anzeni kipindi cha maombi kwa kumsifu Mungu kwamba ni mwema, mwenye fadhili na mpole.
Mtukuze Mungu kwamba amechagua kukutumia wewe kuzifikia roho ambazo zina kiu ya maji ya uzima.

Kuungama na Kudai Ushindi dhidi ya dhambi.
Muombe Mungu akuonyeshe dhambi unazohitaji kuziungama kwa wazi na zile unazohitaji kuziungama kwa siri.
Dai ushindi Wake dhidi ya dhambi hizo.
Omba kwa ajili ya msamaha kwa nyakati ambazo uliona haya kushiriki imani yako kwa wengine.
Muombe Mungu akupatie ujasiri na upendo kupitia Kristo kukaa ndani yako.
Mshukuru Mungu kwamba anakusamehe kulingana na 1Yohana 1:9

Sala na Maombezi. Muombe Mungu akupatie mzigo wa kuongoa roho na upendo kwa watoto Wake waliopotea.
Muombe Mungu aweke katika mioyo ya majirani zako njaa na kiu Yake.
Muombe Bwana akujaze na Roho wake Mtakatifu na akufundishe jinsi ya kuwafikia majirani kupitia matendo yako ya upendo, kwa kuhudumia mahitaji yao, kwa wao kukuamini, na kwa kuwaalika kumfuata Yesu.
Omba ili uweze kushiriki uzoefu wa furaha ya kumtangaza Yesu.
Omba kwa ajili ya tabia yenye kupendeza, tabia kama ya Kristo ambayo itawavuta watu kwa Yesu.
Omba ili Mungu akufundishe jinsi ya kuwaelekeza watu kwa Yesu na si kwako mwenyewe.
Omba kwa ajili ya matumizi zaidi ya vitabu vya Kikristo kwa washiriki wote na kwa mkazo zaidi katika uinjilisti wa vitabu, kupitia kwa nakala zilizochapishwa na ambazo ziko katika namna ya kielektroniki.
Omba kwa ajili ya mkazo mpya juu ya umuhimu mkubwa wa kuhudhuria Shule ya Sabato, ambayo inalenga katika ushirika, utume, kujifunza Biblia na huduma nje ya kanisa.
Omba kwa ajili ya mkazo zaidi kwa vikundi vidogo vya kutoa huduma nje ya kanisa, ili washiriki wote waweze kujihusisha katika ushuhudiaji binafsi na kutangaza ukweli mkuu wa Mungu katika siku hizi za mwisho.
Omba ili viongozi wa kanisa (mchungaji wako wa Mtaa, wachungaji wa konferensi, unioni, divisheni na Makao Makuu ya Kanisa waweze kuwa mashahidi wazuri kwa majirani zao.

Utume katika miji Mikuu –
omba kwa ajili ya divisheni ya Inter-Europian na miji waliyoichagua kuifanyia kazi: Geneva, Prague, Vienna. Inua katika maombi pia Unioni za Middle East na North Africa na miji 43 wanayopanga kuifikia katika miaka mine hadi mitano ijayo.
Ombea washiriki wanaofanyia kazi miji hii.
Muombe Mungu kwa ujasiri wa kumshuhudia Yeye katika mazingira yo yote yale.
Omba kwa ajili ya kukua kwa lengo katika huduma ya vyombo vya habari vya kanisa, vikiongoza katika uinjilisti mkubwa wa ushuhudiaji kote duniani.
Omba kwa ajili ya watu saba au zaidi katika orodha yako ili kwamba waone hitaji lao na kufungua mioyo yao kwa Roho Mtakatifu.
Omba kwa ajili ya mahitaji binafsi uliyo nayo.

Shukrani
Mshukuru Mungu kwamba anatenda kazi katika maisha ya watu wa familia yako, marafiki na majirani.
Mshukuru Mungu kwamba anao watu katika kila mji ambao wanatazama mbinguni kwa shauku kuu!
Mshukuru Mungu kwamba anafanya kazi katika mioyo ya wale ambao umekuwa ukiwaombea.

Mapendekezo ya Nyimbo:
Tawala ndani yangu no.147, Taa yangu ndogo nitaiangaza, Walio kifoni no.56, Kuwatafuta wasioweza no.100 

"Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. Matendo 1:8

Watoto wa Mungu wanaitwa wawakilishi wa Kristo, wakionyesha wema na rehema za Bwana. Kama Yesu alivyotufunulia tabia ya kweli ya Baba Yake, nasi tunapaswa kumfunua Kristo kwa ulimwengu ambao haujui upendo Wake wenye upole na huruma. “Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni,” alisema Yesu, “nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.” “Mimi ndani yao, nawe ndani yangu;…..ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma.” Yohana17:18,23. Mtume Paulo anawaambia wanafunzi wa Yesu, “Mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo,” inajulikana na kusomwa na watu wote.” 2Wakorintho3: 3, 2. Katika kila mtoto wa Mungu, Yesu anatuma barua kwa ulimwengu. Kama wewe ni mfuasi wa Kristo, anatuma kupitia kwako barua kwa familia, kijijini, barabarani, mahali unapoishi. Yesu, ndani yako, anatamani kuongea na mioyo ya wale ambao hawamtambui. Huenda labla hawasomi Biblia, au hawaisikii sauti inayoongea nao katika kurasa za Biblia; hawaoni upendo wa Mungu kupitia kwa kazi Zake, lakini wewe ni mwakilishi wa kweli wa Yesu, yaweza kuwa kupitia wewe, wataongozwa kuelewa jambo fulani la wema Wake na kuvutwa kumpenda na kumtumikia Mungu.

Tembelea majirani zako na onyesha kujali wokovu wa roho zao. Amsha kila uwezo wa kiroho katika utendaji. Waambie wale unaowatembelea kwamba mwisho wa mambo yote u karibu. Bwana, Yesu Kristo atafungua milango ya mioyo yao na atafanya katika akili zao mvuto utakaodumu. Hata wakati wanapojishughulisha na kazi zao za kila siku, watu wa Mungu wanaweza kuongoza wengine kwa Kristo. Na wakati wanapofanya hili, watakuwa na uhakika wenye thamani kwamba Mwokozi yupo karibu nao. Hawahitaji kufikiri kwamba wameachwa kutegemea juhudi zao dhaifu. Kristo atawapatia maneno ya kuongea ambayo yataburudisha na kutia moyo na kutia nguvu walio maskini, na roho zinazotaabika katika giza. Imani yao wenyewe itatiwa nguvu wanapotambua kwamba ahadi ya Mwokozi inatimizwa. Wao sio tu mbaraka kwa wengine, bali kazi wanayoifanya huleta mbaraka kwao wenyewe.

Mvuto wako hufikia nafsi; unagusa waya ambao si waya wa kawaida bali waya unaotetema kwenda kwa Mungu…. Ni wajibu wako kuwa Mkristo wa viwango vya juu vya neno, “kama Kristo”. Ni kupitia kwa mistari isiyoonekana inayokuvuta kwa akili za watu wengine ambao unakutanishwa pamoja nao, kwamba kama unadumu katika muunganiko na Mungu, utaacha mivuto ambayo itakufanya kuwa “harufu ya uzima iletayo uzima” Bali, kama wewe ni mbinafsi, kama unajiinua mwenyewe, kama akili yako ni ya kidunia, haijalishi nafasi uliyo nayo, wala uzoefu ulio nao, au kiasi unachojua, kama hauna sheria ya wema katika kinywa chako, harufu nzuri ya upendo inayotiririka kutoka katika moyo wako, huwezi kufanya cho chote kama ipasavyo.

Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba, yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake. (1Yohana 4:20, 21)

Mwonekano wa sura yenye ukweli, uaminifu ya dada au kaka au rafiki ikitolewa kwa namna iliyo ya kawaida kabisa, inayo nguvu ya kufungua milango ya mioyo ambayo inahitaji harufu njema ya maneno yenye kufanana na Kristo na mguso rahisi wa roho ya upendo wa Kristo.

Kote kutuzunguka kunasikikika mayowe ya huzuni iliyopo duniani. Kila mahali wako wahitaji na walio taabuni. Ni sisi tunaohitaji kuongoza katika kuwapoza na kurahisisha magumu ya maisha na huzuni zake. Mahitaji ya roho, ni upendo pekee wa Kristo unaoweza kutosheleza. Kama Kristo atakaa ndani yetu, mioyo yetu itajazwa kwa huruma ya kimbingu. Vijito vilivyofungwa vya upendo wa dhati wakufanana na Kristo vitafunguliwa.

Ni utamu kiasi gani ulitiririka kutoka katika uwepo halisi wa Kristo! Roho hiyo hiyo itaonekana kwa watoto Wake. Wale ambao Kristo anakaa ndani yao watazingirwa na uwepo wa kimbingu. Mavazi yao meupe ya usafi yatakuwa harufu yenye manukato kutoka katika bustani ya Bwana. Nyuso zao zitaakisi nuru kutoka Kwake, zikiangaza njia kwa miguu inayojikwaa na iliyochoka.

Maswali ya Kujitathmini:

1.Je, unatamani kujazwa na upendo wa Kristo na kujazwa na huruma kwa ulimwengu unaoangamia?
2.Ni kwa namna gani za kiutendaji unaweza ukashuhudia kwa majirani zako?
SIKU YA 09:

       KRISTO AKIAKISIWA NDANI YA KANISA:
 
“Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi. (Yohana 17:23)

• Anzeni kipindi chenu cha maombi kwa kumsifu Mungu kwamba Yeye ni furaha, amani na uvumilivu n.k
• Mtukuze Mungu kwamba ameliita kanisa Lake la masalio kuwa nuru kwa ulimwengu.
• Mtukuze Mungu kwamba ataikamilisha kazi aliyoianzisha katika kanisa.
Kuungama na Kudai Ushindi dhidi ya dhambi (kama dakika 5)
• Muombe Mungu akuonyeshe dhambi unazohitaji kuziungama faraghani. Dai ushindi dhidi ya dhambi hizo.
• Muombe Mungu msamaha kwa nyakati ambazo uliruhusu wivu, kushuku au kutafuta makosa kwa ndugu zako ndani ya moyo wako. Omba kwa ajili ya moyo mpya ukijazwa na upendo pamoja na huruma.
Sala na Maombezi
• Muombe Mungu aandae moyo wako kumpokea Roho Mtakatifu.
• Omba kwa ajili ya familia yako ili iunganishwe na kwamba amani na upendo vitawale makanisa yetu.
• Omba ili Mungu atakase kanisa ili wageni wahisi uwepo wa Roho Mtakatifu.
• Omba ili viongozi wa kanisa (mchungaji wako wa mtaa, wachuganji wa konferensi, unioni, divisheni na Makao Makuu ya Kanisa) wafanye kazi kwa upendo, huruma na umoja katika kumaliza kazi waliyopatiwa na Kristo.
• Omba kwa ajili ya umoja kote ulimwenguni katika mikusanyiko ya kikanisa na upekee wa kanisa ukijengwa katika kuheshimu Neno la Mungu, maombi yenye unyenyekevu, nguvu ya Roho Mtakatifu, kuheshimu sera za kanisa zilizopitishwa na kujiingiza kikamilifu katika utume wa kanisa.
• Omba kwa ajili ya unyenyekevu katika maisha yetu ili tuweze kuunganishwa tunapojitoa katika kutii uongozi wa Mungu na mchakato wa kanisa katika kufanya maamuzi ambayo huamuliwa pamoja na kukubali mapendekezo yatakayopitishwa katika ngazi ya Makao Makuu ya Kanisa.
• Omba ili kwamba tuweze kutoa muda wetu zaidi katika mambo ya umiele kupitia kujifunza Biblia na maombi, ili kumruhusu Mungu kuongoza kwa ukamilifu watu wake kulingana na mapenzi Yake na sio mapenzi yetu. Hii itatusaidia kutuweka daima karibu na Mungu na kuruhusu nguvu ya Roho Mtakatifu kugeuza mazoea ya kiulimwengu ambayo huliweka matatani kanisa la Mungu na maisha yetu ya kila siku.
• Utume Katika Miji Mikuu – Omba kwa ajili ya divisheni yetu ya East –Central Africa na miji tuliyochagua kuifanyia kazi huko: Kinshasa, Dar-es-Salaam, Addis Ababa, Kampala, Kananga, Lodwar, Kigali, Lubumbashi, Goma, Magara na Juba. Omba ili ngome imara za shetani zivunjwe, mahusiano pamoja na Kristo yajengwe.
• Omba kwa ajili ya ulinzi kwa vijana na sisi sote kutoka katika mivuto inaoongezeka kila siku ya kidunia. Omba ili tuweze kuweka kipaumbele katika Neno la Mungu na huduma kwa wengine. Omba ili makanisa mahalia yaweze kudhamini vijana katika utume nje ya kanisa na fursa za kutoa huduma.
• Omba ili watu saba au zaidi katika orodha yako waone hitaji la kufungua mioyo yao kwa Roho Mtakatifu.
• Omba kwa ajili ya mahitaji binafsi uliyo nayo.
Shukrani (dakika 10)
• Mshukuru Mungu kwa kile alichofanya katika kanisa Lake na kile atakachokifanya katika kanisa.
• Mshukuru Mungu kwamba yuko tayari kusafisha, kutakasa na kuongoza kanisa.
• Mshukuru Mungu kwamba anafanya kazi katika mioyo ya wale ambao unawaombea.
Mapendekezo ya Nyimbo
Tutajenga juu ya Mwamba no. 72, Msingi wa Kanisa no. 195, Yote Namtolea Yesu no. 122,
KRISTO AKIAKISIWA NDANI YA KANISA
“Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi. Yohana 17:23
Hakuna kitu cho chote ambacho kinaweza kuhafifisha mvuto wa kanisa kama kukosekana kwa upendo….. Watu wa kidunia wanatuangalia ili kuona kile imani inachofanya katika tabia na maisha yetu. Wanaangalia kuona kama imani hiyo ina matokeo ya kuleta utakaso katika mioyo yetu, kama tumebadilishwa kufanana na Kristo. Wako makini kugundua kila dosari katika maisha yetu, kila kukosa msimamo katika matendo yetu, hebu tusiwape nafasi kukebehi imani yetu. Sio upinzani duniani ambao utatuweka hatarini bali ni uovu unaoendekezwa katikati yetu ambao huleta matokeo ya kutisha. Ni maisha ya watu wasiojitoa kikamilifu na kutoa mioyo yao nusu nusu ambayo huzuia kazi ya ukweli na kuleta giza katika kanisa la Mungu.
Hakuna njia yenye uhakika zaidi ya kutufanya tudhoofike katika mambo ya kiroho kama kuwa na wivu, hali ya kushuku, kujawa na kutafuta makosa na kupuuzia dhambi….Unapokuwa pamoja na watu wengine, linda maneno yako…. Kama kuipenda kweli kuko ndani ya moyo wako utaongea ile kweli. Utaongea juu ya tumaini lenye baraka ulilo nalo katika Yesu. Kama una upendo katika moyo wako utatafuta kumuimarisha na kumjenga ndugu yako katika imani iliyo takatifu zaidi. Kama neno litaponyoka katika midomo lenye kuharibu tabia ya rafiki au ndugu yako, usiendekeze uzungumzaji huo mbaya kwani hiyo ni kazi ya adui. Kwa upole mkumbushe mzungumzaji kwamba Neno la Mungu linakataa uzungumzaji wa namna hiyo. Tunapaswa kumimina kiini cha kila kitu ambacho kinalinajisi hekalu ya roho, ili Kristo aweze kukaa ndani. Mwokozi wetu ametuambia namna tunavyoweza kumfunua kwa ulimwengu. Kama tutadumisha Roho Wake, kama tutadhihirisha upendo Wake kwa wengine, kama tutalinda maslahi ya kila mmoja wetu, kama tutakuwa watu wema, wavumilivu, wastahimilivu, ulimwengu utakuwa na ushahidi wa matunda tutakayozaa kwamba sisi tu watoto wa Mungu. Ni umoja katika kanisa ambao huliwezesha kanisa kuufanyia kazi mvuto wenye ufahamu kwa waumini na wakazi wa dunia. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. Yohana 13:35.
Dini ya Kristo ni zaidi ya msamaha wa dhambi; humaanisha kwamba dhambi zimeondolewa na kwamba sehemu iliyobaki tupu imejazwa na Roho Mtakatifu. Inamaanisha kwamba akili hutiwa nuru ya mbinguni na moyo huondolewa ubinafsi wote na kujazwa na uwepo wa Kristo. Wakati hili linapofanyika kwa washiriki wa kanisa, kanisa litakuwa hai na lenye kufanya kazi. Tutakapoweka mioyo yetu katika umoja na Kristo na maisha yetu yakapatikana na kazi Yake, Roho ambaye alishuka wakati wa Pentekoste atamwagwa kwetu. Tutakuwa imara katika nguvu ya Kristo na kujazwa na ukamilifu wa Mungu……Tutajitoa kwa Kristo, na kuweka wakfu vyote tulivyo navyo, uwezo wetu wote katika huduma ya Kristo. Tutaitangaza imani yetu vyema, tutamtumikia Mungu kwa kuwahudumia wale wanaohitaji msaada wetu. Ndipo tutaruhusu nuru yetu kuangaza kwa matendo mema.
Kama wanafunzi wa Yesu walivyojazwa na nguvu ya Roho Mtakatifu, wakaenda kutangaza injili, hivyo hivyo watumishi wa Mungu wanatakiwa kwenda kutangaza injili. Kila ambaye anamulikiwa na nuru ya ukweli wa leo anapaswa kuamshwa kwa kuwahurumia wale walioko gizani. Kutoka kwa washiriki wote nuru yapaswa kuakisiwa katika mionzi iliyo wazi na ming’aavu. Kazi kama ile ile aliyoifanya Bwana kupitia kwa wajumbe wake baada ya siku ya Pentekoste anasubiri kuifanya hata leo. Katika kipindi hiki, wakati mwisho wa mambo yote umekaribia, ari ya kanisa yapaswa kuzidi ile ya kanisa la awali. Ari kwa ajili ya utukufu wa Mungu iliwafanya wanafunzi kubeba ushuhuda wa ukweli kwa nguvu nyingi. Je ari hii haipaswi kuichoma mioyo yetu kwa ajili ya kuwiwa kuhadithia kisa cha upendo uokoao wa Kristo aliyesulubishwa?

Maswali ya Kujitathmini:
1. Je wewe, mshiriki wa kanisa hai la Kristo, wawezaje kuhimiza umoja na upendo kwa ndugu zako?
2. Tafakari kwa maombi kama unahitaji kusamehe, au kuomba msamaha au kupatana na ye yote ndani au nje ya kanisa.

Wednesday, 13 January 2016

SIKU YA – 8:

     KRISTO AKIAKISIWA KATIKA FAMILIA:

“Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.” 1Yohana 4:7

Mapendekezo ya Utaratibu wa Kipindi cha Maombi
Kusifu (takribani dakika 10)
Anzeni kipindi cha maombi kwa kumsifu Mungu kwa jinsi alivyo (Tabia Yake). Yeye ni mwenye neema n.k
Msifu Mungu kwamba Yeye ni Baba wa familia ya wanadamu duniani.
Msifu Mungu kwamba anataka familia ya kibinadamu iakisi uzuri Wake na tabia Yake.
Kuungama na Kudai Ushindi dhidi ya dhambi
Muombe Mungu akuonyeshe dhambi unazohitaji kuziungama kwa siri. Dai ushindi juu ya dhambi hizo.
Muombe Mungu msamaha kwa nyakati ambazo hukumuakisi Mungu katika familia yako.
Muombe Mungu msamaha kwa nyakati ambazo hukuwaheshimu na kuwatii wazazi wako pamoja na ndugu mliozaliwa nao.
Mshukuru Mungu kwamba anakusamehe kulingana na 1Yohana 1:9.
Sala na Maombezi
Muombe Mungu ajaze moyo wako kwa Roho Mtakatifu na kukufanya kuwa mfano hai kwa familia yako
Muombe Mungu ili kila mwanafamilia katika famila yako avutwe karibu na Kristo
Muombe Mungu azilinde familia za Kiadventista dhidi ya mashambulio ya Shetani, zikiwemo familia katika kanisa lako mahalia. Muombe Mungu kwa ajili ya uponyaji pale inapohitajika.
Omba ili kwamba viongozi wa kanisa (mchungaji wako wa mtaa, wachungaji wa konferensi, unioni, divisheni na Makao Makuu ya Kanisa) pamoja na familia zao wamuakisi Kristo kwa ulimwengu.
Omba kwa ajili ya mavuno ya pekee ya roho kutokana na mbegu zilizopandwa wakati wa mradi wa usambazaji wa kitabu cha Tumaini Kuu katika mifumo yake yote.
Omba kwamba wazazi wamuakisi Kristo kwa watoto wao na kuwalea kwa ajili ya Ufalme.
Omba ili kwamba Mungu alete uelewa kamili wa njia aliyoitumia Kristo (huduma kamili ya uponyaji) ili kwamba washiriki wote wasaidie watu kwa kuwapatia mahitaji yao na kufuata kilelezo cha Kristo katika kuhudumia wengine.
Omba kwa ajili ya muunganiko wa harakati za uinjilisti na ushuhudiaji wa kila mwanaume, mwanamke na watoto wote wa Kiadventista kote duniani. Omba kwamba tujazwe na Roho Mtakatifu tunapojisalimisha kwa uongozi wake katika maisha yetu.
Msihi Bwana kwa niaba ya familia za Kiadventista ili ziwe kielelezo cha jinsi Kristo anavyoweza kuleta amani na upendo majumbani, kuondoa kila unyanyasaji na misongo kupitia kwa nguvu itakasayo ya haki ya Kristo na kuelekeza watu kwa kuja kwa Kristo kuliko karibu na hatimae kuungana na familia ya milele ya Mungu huko mbinguni.
Utume katika Miji Mikuu Omba kwa ajili ya Divisheni ya Euro-Asia na miji wanayoifanyia kazi: Moscow, Kiev, Kishinev, Donetsk, Kharkov, Minsk, St. Petersburg, Novosibirsk, Krasnoyarsk, Khabarovsk, Rostov -on-Don, Tbilisi, Yerevan na Almaty. Omba kwa ajili ya maelfu ya huduma za kuwafikia watu na matukio yanayoendelea ya uvunaji wa roho.
Omba ili kwamba watu saba au zaidi katika orodha yako waone hitaji lao na kufungua mioyo yao kwa Roho Mtakatifu.
Omba kwa ajili ya mahitaji binafsi uliyo nayo.
Shukrani (dakika 10)
Mshukuru Mungu kwamba anafanyia kazi mioyo ya wanafamilia wako.
Mshukuru Mungu kwamba yu tayari kukusafisha, kukutakasa na kukaa ndani yako na ndani ya familia yako.
Mshukuru Mungu kwamba Yesu ametupatia kielelezo cha jinsi ya kuwaheshimu wazazi wetu pamoja na kuwapenda ndugu tuliozaliwa nao.
Mapendekezo ya Nyimbo
Kuwa na Yesu Nyumbani no. 204, Panapo Pendo no.184, Upendo ni Furaha no. 199

 KRISTO AKIAKISIWA KATIKA FAMILIA:

“Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.” 1Yohana 4:7
Dini ya Kristo itatuongoza katika kufanya mambo yote mema kadiri iwezekanavyo, kwa watu wa daraja la juu na la chini, kwa matajiri na maskini, kwa wenye furaha na wale wanaoonewa. Lakini haswa itatuongoza katika udhihirisho wa wema katika familia zetu wenyewe. Dini hiyo itadhihirika katika matendo ya adabu, na upendo kwa baba, mama, mke na mtoto. Tunapaswa tumwangalie Yesu, kukamata roho Yake, kuishi katika nuru ya wema Wake na upendo na kuakisi utukufu Wake kwa wengine.
“Basi mtiini Mungu, Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.” Yakobo 4:7
Kama utajitoa kikamilifu kwa Yesu, ataumba ndani yako tamanio la kina kwa ajili ya urafiki na Mungu, nawe utajazwa shauku ya kuakisi wema Wake na upendo Wake katika maisha yako na tabia yako kwa familia yako na kwa wale wasioufahamu upendo Wake. Kwa kupanda uvumilivu, upole, ustahimilivu, kwa kuonyesha heshima na kuwapa utii mama yako na baba yako kama impendezavyo Bwana, utakuwa ukitoa ushuhuda katika maisha yako ya kila siku kwamba ukweli una nguvu ya kutakasa tabia.
Ni swala gumu kurekebisha mambo magumu katika familia, hata pale ambapo mume na mke wanatafuta kufanya hivyo kama wameshindwa kusalimisha mioyo yao kwa Mungu.
Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Yohana 7:38.
Kama mapenzi ya Mungu yatatimizwa, mume na mke wataheshimiana na kuotesha upendo na ujasiri. Cho chote kile ambacho chaweza kuharibu amani na umoja wa familia chapaswa kuzuiwa kwa uthabiti na utu wema pamoja na upendo vyapaswa kudumishwa. Mtu yule ambaye anadhihirisha roho ya upole, ustahimilivu na upendo atagundua kuwa roho ile ile itaakisiwa toka kwake. Mahali ambapo Roho wa Mungu anatawala, hakutakuwa na maongezi yasiyofaa katika mahusiano ya ndoa. Kama kweli Kristo atajengwa ndani kwa kina, tumaini la utukufu, kutakuwa na umoja na upendo nyumbani. Kristo akikaa katika moyo wa mke kutakuwa na makubaliano pamoja na Kristo anayekaa ndani ya moyo wa mume. Watafanya bidii pamoja kwa ajili ya kwenda katika makao ambayo Kristo amekwenda kuandaa kwa wale wampendao.
Lazima tuwe na Roho wa Mungu, au kamwe hatutakuwa na mwafaka nyumbani. Mke, kama ana roho wa Kristo atakuwa makini na maneno yake, atajizuia, atakuwa mtii na bado hatajisikia kana kwamba ni mtumwa, lakini mwenzi wa mumewe. Kama mume ni mtumishi wa Mungu, hatamtawala mke wake, hatakuwa dikteta na mkali. Hatutaweza kudumisha upendo nyumbani kwa kuwa waangalifu kupita kiasi, kwani Roho wa Bwana akiwepo nyumbani, panakuwa sehemu ya mbinguni……mmoja anapokosea, mwingine atafanyia mazoezi ustahimilivu kama wa Kristo badala ya kumpa kisogo mwenzake na kuondoka.
Kama unayo matazamio makubwa na kusudi la kufika katika kiwango cha juu, maisha ya nyumbani yanaweza kukupa adabu bora zaidi. Kama ukikosea nyumbani, utakosa katika kila lengo na kila jitihada. Anza nyumbani ili kukamilisha tabia ambayo Mungu ataikubali, tabia itakayofanya uwe mbaraka nyumbani, na utakapokuwa mbali na nyumbani, hautashindwa kuwa mbaraka kwa wale utakaokutana nao. Dini inayofanyiwa mazoezi nyumbani huakisi mbali zaidi ya wigo wa hapo nyumbani.

Maswali ya Kujitathmini:
1.Je unawezaje kuongoza familia yako kwa kielelezo cha maisha tele kwa Kristo?
2.Je daima umekuwa mwanafamilia mzuri? Je kuna mambo ambayo unahitaji kurekebisha? Je wahitaji kuifanya familia yako kuwa kipaumbele zaidi ya mambo mengine?

SIKU YA – 7:

        MAISHA AMBAYO HUBARIKI WENGINE:

“Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Yohana 7:38

Mapendekezo ya utaratibu wa maombi Kusifu (dakika 10) Anzeni kipindi chenu cha maombi kwa kumsifu Mungu kwa jinsi aliyo (tabia Yake). Yeye ni Mungu wa milele, Mungu mvumilivu na mwenye upendo. Mungu ndiye nguvu yetu (Zaburi 27:1) na Yeye ndiye mahali petu pa kupumzika. (Yeremia 50:6). Mtukuze Mungu kwa utayali wake wa kututumia kubariki wengine, hata kama tuna mapungufu na makosa. Mtukuze Mungu kwamba sio sisi ambao tunagusa na kubariki maisha ya watu bali ni Kristo ndani yetu Kuungama na Kudai Ushindi dhidi ya dhambi Muombe Mungu akuonyeshe dhambi utakazoziungama hadharani na zile za kuungama faraghani. Dai ushindi Wake dhidi ya dhambi hizo. Muombe Mungu akusamehe katika nyakati ambazo maisha yako hayakuwa mbaraka kwa wengine. Muombe Mungu msamaha katika nyakati ambazo ulijali zaidi mafaniko yako kuliko kumtumikia Yeye. Mshukuru Mungu kwamba anakusamehe kulingana 1Yohana 1:9. Sala na
Maombezi Mwombe Mungu akupe imani hata pale ambapo shetani hujaribu kukukatisha tamaa usiwahudumie wengine. Muombe Mungu akupe mzigo wa roho za watu wengine na upendo kwa watoto wa Mungu waliopotea. Omba kwa ajili ya tabia inayopendeza, tabia ya kufanana na Kristo itakayowavuta watu kwa Yesu. Omba kwa ajili ya kila mshiriki kuhisi mzigo wa kuongoa roho na kutambua kwamba mbingu inamhitaji kila mmoja kufuata kielelezo cha Kristo kwa kushiriki imani yake akiongozwa na Mungu. Omba kwa ajili ya kutumia vyanzo vyote vya habari vitakavyofaa katika kushiriki ujumbe wa malaika wa tatu katika namna mpya na yenye ubunifu kwa watu wenye shughuli nyingi wa siku hizi. Omba ili idadi iongozeke ya washiriki wote na kujiunga na uinjilisti na taasisi wanapounga mkono utume wa kanisa unaoendelea.
Utume katika Miji Mikuu - Omba kwa ajili ya Divisheni ya Inter-American na miji wanayotamani kuileta kwa Kristo: Mexico, Caracas, Bogatá, Nassau, Belize, Georgetown, Cali, Cayenne, Guatemala, Quetzaltenango, Port-au-Prince, Tegucigalpla, Mérida, kisiwa chote cha Puerto Rico. Santiago de los Caballeros na Maracaibo. Omba ili washiriki waendeleze mikakati ya kufikia miji mikubwa. Omba juu ya kuanzishwa kwa maelfu ya “vyanzo vya vivutio” (makanisa, vituo vya afya, shule za kutwa, mahali vitabu vinapouzwa, vituo vya kuhudumia jamii, vikundi vya vijana, migahawa ya vyakula visivyo na nyama, zahanati na mengineyo) haswa katika miji mikubwa duniani, omba pia vituo hivi vifanye tofauti kubwa katika maisha ya watu wanapopata uzoefu wa ukweli wa Mungu kupitia huduma ya Kikristo. Omba ili kwamba watu saba au zaidi katika orodha yako waone hitaji lao na kufungua mioyo yao kwa Roho Mtakatifu. Omba kwa ajili ya mahitaji binafsi uliyo nayo.
Shukrani (takribani dakika 10) Mshukuru Mungu kwamba anataka kututumia sisi wala sio malaika kuwa watendakazi pamoja Naye kubariki wengine. Mshukuru Mungu kwamba Yesu ametupatia kielelezo cha jinsi ya kuwa mbaraka kwa watu wengine. Mshukuru Mungu kwamba anatuma Roho wake Mtakatifu kufanya kazi katika mioyo ya wale unaowaombea.
Mapendekezo ya Nyimbo: Popote Mashamba Yajaa no. 94

MAISHA AMBAYO HUBARIKI WENGINE

Kila mtu ambaye Kristo anakaa ndani yake, kila ambaye ataonyesha upendo Wake kwa ulimwengu, ni mtendakazi pamoja na Mungu kwa ajili ya kubariki wanadamu wengine. Kadiri mtu huyo anapopokea kutoka kwa Mwokozi neema ya kuwapatia wengine, kutoka katika utu wake wote kunatiririka wimbi la maisha ya kiroho.
Mwanafunzi wa Yesu aliye mnyenyekevu na maskini zaidi anaweza kuwa mbaraka kwa wengine. Watu kama hao wanaweza wasitambue kama wanafanya jema lo lote, lakini kwa mvuto wao bila kutambua wanaweza wakaanzisha mawimbi ya mibaraka ambayo itapanuka na kuzama chini, na matokeo yenye baraka wanaweza wasiyajue hadi wakati wa thawabu ya mwisho. Watu hao hawajisikii wala hawajui kama wanafanya jambo lililo kuu, hawahitaji kujichosha kwa wasiwasi wa kupata mafanikio. Wanahitaji tu kwenda mbele kimya, wakifanya kwa uaminifu kazi ambayo uongozi wa Mungu unaagiza, na maisha yao hayatakuwa bure. Roho zao wenyewe zitakuwa zikikua zaidi na zaidi katika kufanana na Kristo; wao ni watendakazi pamoja na Mungu katika maisha haya, na hivyo wanastahili kazi iliyo bora zaidi na furaha isiyo na kivuli ya maisha yajayo.
Bwana anatuita tuamke katika kutambua wajibu wetu. Mungu amempatia kika mwanadamu kazi yake, hivyo kila mmoja anaweza kuishi maisha yenye manufaa. Hebu tujifunze yote tuwezayo na hatimae tuwe mbaraka kwa wengine kwa kuwapatia maarifa ya ukweli. Hebu kila mmoja atende kwa uwezo wake wote, kwa mamnbo mabalimbali kwa hiari akisaidia wengine kubeba mizigo.
“Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.”
Waweza kuwa mbaraka mkubwa kwa wengine kama utajitoa mwenyewe kikamilifu kwa ajili ya huduma ya Bwana. Utapewa nguvu kutoka juu kama utasimama upande wa Bwana. Kupitia Kristo unaweza kuepuka ufisadi ulioko duniani katika tamaa na kuwa kielelezo cha uadilifu wa kile ambacho Kristo anaweza kufanya kwa wale wanaoshirikiana Naye. Mungu anatamani wanaume kwa wanawake kuishi maisha yaliyo bora.
Mungu anawapatia wanadamu mafanikio ya maisha, si kwa sababu tu ya kupata tu utajiri, bali kuboresha uwezo wao wa juu kwa kufanya kazi ambayo amewakabidhi wanadamu – kazi ya kutafuta kujua na kuleta nafuu kwa mahitaji ya msingi ya wanadamu wenzao. Mtu anapaswa kufanya kazi si kwa manufaa yake binafsi lakini kwa manufaa ya kila anayemzunguka, akiwabariki wengine kwa mvuto wake na matendo mema. Makusudi haya ya Mungu hudhihirika katika maisha ya Yesu., “Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu”. Yakobo 4:6.
Tunapokuwa wanyenyekevu na kusimama tukiwa na hisia za toba tunajiweka mahali ambapo Mungu anaweza na atajifunua mwenyewe kwetu. Yeye hupendezwa sana pale ambapo tunapodai rehema na mibaraka tuliyopewa kipindi kilichopita kama sababu ya Yeye kutumwagia mibaraka mikubwa zaidi. Mungu atatimiza zaidi ya matarajio ya wale ambao wanamtumainia Yeye kikamilifu. Bwana wetu Yesu Kristo anajua kile hasa watoto wake wanachohitaji, na uweza wa uungu kiasi gani ambayo utahitajika kwa mbaraka wa wanadamu; na anatupatia yote ambayo tutahitaji katika kubariki wengine na kuinua roho zetu sisi wenyewe.
Wale ambao wanampenda Mungu kwa dhati watatamani vivyo hivyo kuboresha talanta ambazo amewapatia, ili waweze kuwa mbaraka kwa wengine, na siku kwa siku milango ya mbinguni itafunguliwa wazi kabisa ili kuwaruhusu waingie na kutoka katika mdomo wa Mfalme wa Utukufu baraka zitaanguka katika masikio yao kama muziki wenye nguvu, “Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa kwa ulimwengu.” Mathayo 25:34

Maswali ya Kujitathmini:
1. Ni mambo gani madogo unayoweza kufanya ili yawe mbaraka kwa wale wanaokuzunguka?
2. Mara nyingi ni rahisi kuwa mbaraka kwa watu walio mbali kuliko kwa familia yako. Je wawezaje kuwa mbaraka kwa wale walio karibu nawe?